Sina lengo la kukashifu dini, ila Walokole mna kelele sana

Sina lengo la kukashifu dini, ila Walokole mna kelele sana

Status
Not open for further replies.
Na siku ya Pentekoste ilipowadia, Roho mtakatifu akawashukia na wote walipojazwa Roho mtakatifu kila mmoja akaongea kwa lugha yake mwenyewe.
Hili Neno unalielewaje mkuu?
 
Kama sio hizo kelele zao saa hizi ungekuwa mfugo wa wachawi au walishakufanya kitoweo mda mrefu, ni vema kutambua uwepo wao hata kama wanaharibu hiyo nguvu ya hirizi yako hapo mfukoni mwako.
 
Nyie vipaza sauti vyenu alfajiri, mchana saa saba, na jioni saa 12 na saa mbili usiku hmvisikii?
Allaaaaah Waakbaruallaaaaa....WAAAKBARU!!!!, Allaaaaaaaaaa Waaakbaruallaaaaaaah WAAAAKBARU....!!!!
 
Na siku ya Pentekoste ilipowadia, Roho mtakatifu akawashukia na wote walipojazwa Roho mtakatifu kila mmoja akaongea kwa lugha yake mwenyewe.
Hili Nenounalielewaje mkuu?
naelewa mantiki ya swali lako.

Hata kama kila mtu aongee kwa lugha yake sio shida, shida hapa ni kuna ulazima gani wa kuweka maspeaker na kuwasikilizisha majirani hizo lugha zenu?
 
Kama sio hizo kelele zao saa hizi ungekuwa mfugo wa wachawi au walishakufanya kitoweo mda mrefu, ni vema kutambua uwepo wao hata kama wanaharibu hiyo nguvu ya hirizi yako hapo mfukoni mwako.
Wachawi wapo makanisani na misikitini huko sio kwa watu kama sisi.
 
Wewe umeelewa nini, tufafanulie,na wapi walipoandika ukiwa unasali upige makelele na kulia
sio kila kinachopaswa kutendeka lazima kiwe kwenye maandiko ndipo kitendeke,unavyosema wapi imeandikwa "ulie" kumbuka kuna wakati kinywa kinashindwa kutamka yale uliyonayo moyoni,hivyo kulia sioni dhambi kwani machozi ni sala pia pale unaposhindwa kunena, (ndiyo maana Mungu anasema yeye huona sirini)na unavyosema "makelele" sidhani kama n kelele..kuna wakati kanisa linaingia kwenye maombi ya vita so usitegemee ukimya mda huo.Ni hivyo tu labda sjaelewa kelele unazozisemea
 
naelewa mantiki ya swali lako.

Hata kama kila mtu aongee kwa lugha yake sio shida, shida hapa ni kuna ulazima gani wa kuweka maspeaker na kuwasikilizisha majirani hizo lugha zenu?
Kwakweli siwezi kushangaa swala la uwepo wa speaker katika sehemu ya ibada kwasababu hata misikitini speakers zipo, Catholic, Anglican, Orthodox kote huko kuna speaker. Mantiki yako ipo kwenye point yakuwa hiyo ni residential area na uwepo wa kanisa mahali hapo unasababisha environmental noise hapo sawa.
All in all ni uwepo wa sera mbovu ambazo zimepelekea makanisa kuwepo katika maeneo ya makazi. Fanya uchunguzi hili utaligundua. Sasa sijui una maoni gani, kwamba unategemea wapunguze makelele wakati hiyo ndio style yao ya kusifu, kuabudu na mahubiri?🤓
 
Mkuu acha kabisa kweli wanakelele kuna mtaa mimi hama miaka miwil nyuma mzee wanasali saa usiku saa 6,saa 7 na saa 8 kelele hadi unashindwa kulala
Uwa kuna Imani kwamba muda wachawi wanaenda kuwanga sasa wao wanavunja zile roho za kichawi zikeinda mitoko na Fisi wao
 
sio kila kinachopaswa kutendeka lazima kiwe kwenye maandiko ndipo kitendeke,unavyosema wapi imeandikwa "ulie" kumbuka kuna wakati kinywa kinashindwa kutamka yale uliyonayo moyoni,hivyo kulia sioni dhambi kwani machozi ni sala pia pale unaposhindwa kunena, (ndiyo maana Mungu anasema yeye huona sirini)na unavyosema "makelele" sidhani kama n kelele..kuna wakati kanisa linaingia kwenye maombi ya vita so usitegemee ukimya mda huo.Ni hivyo tu labda sjaelewa kelele unazozisemea
Kelele ni pale mnapolazimisha hizo saut zenu zisikike mtaa mzima.
 
Sasa bila kutoa tafsiri ya hicho kifungu, utakuwa bado hujafanya lolote ndugu.
sawa, maana yake ni pale mtu anapokua na uhitaji wa jambo fulan basi aingie katika chumba chake cha maombi na kusema na Mungu, na katika maombi yako omba kile unachohitaji (ndo maana apo anasema msipayuke) hivyo unasema jambo unalolihitaji kama ni chakula unasema na sio unaenda kwenye maombi unakua kama unalalama ata ukiulizwa ulichokiomba ni nini hukumbuki,kwakua ulikua unapayuka na sio kuomba ndio maana Mungu anasema pia hapo.. kwamba yeye anayajua matatizo yetu kabla hata hatujayasema.[/QUOTE]
 
Kelele ni pale mnapolazimisha hizo saut zenu zisikike mtaa mzima.
ibada hufanyika kanisani na pia vyombo hutumika hivyo sauti ni lazima kuwa juu na hata nyie wa mtaa huo mtaskia tu, vivyo hivyo sidhani kama kuna ubaya kwani kila mtu anao uhuru wa kuabudu na kufurahi pia ndiyo maana kuna makanisa,misikiti na kumbi za starehe ata apo mtaani nanyi kelele zipo tu lakini kelele za kanisa ndio mnazisikia tu,inashangaza kwakweli.
 
Mimi ni mkristu. Ila naunga mkono hoja ya jamaa, hawa wenzetu walokoke ni washamba mno. Azana za msikitini hazina kelele kihivyo
Adhana yenyewe haifiki hata dakika tano, hata kama ni mara tano kwa siku, kwahiyo jumla ni dakika 25, hata ukipiga mara wiki nzima bado haifikii kelele za usiku wao mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona umeamka salama heri tu kumlilia Mungu na kumshukuru lakini sio kuwakashifu watu wake. Ukinyamaza ni heri kuliko ukaongea kwa kukosea. Kuna mmoja alisema hivo hivo, akajibiwa nawewe utakuja kulia ukifukuzwa kazi, kilichotokea ni hivyo, sasa lipi jema?
"Heri wanaolia sasa maana watapata faraja."
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom