Sina lengo la kukashifu dini, ila Walokole mna kelele sana

Sina lengo la kukashifu dini, ila Walokole mna kelele sana

Status
Not open for further replies.
Nyie vipaza sauti vyenu alfajiri, mchana saa saba, na jioni saa 12 na saa mbili usiku hmvisikii?
Adhana huchukua dk 2 hadi 3 kwa siku tuna vipindi 5 vya swala 5 mara 3 utapata jibu mwenyewe ni dk ngapi ninyi hamna mchana wala usiku si siku za kazi wala weekend jibu unalo ila unaleta ushabiki tu jiulize kwanini malalamiko yanayohusu walokole ni mengi kuliko yanayohusu adhana?
 
Hao wanaofunga maporomondo makubwa mengi alfajiri, mchana na jion wanapga kelele mji mzima, na hao wanaokesha wanapga ma nyimbo na ugomvi na karaha na makelele ya kila namna, mbona sisi hatujasema, kwahyo kuweka ka kitega uchumi kako hapo ndo unataka watu wote wakuone wew nan, na unataka kuzuia watu wasifanye mambo yako kisa wew au?
Kweli usilolijua sawa na usiku wa giza, unajua maana ya Adhana,unajua faida anayoipata Muadhini,pole sana,lakini ukweli wako Utaupata siku ukija fumba macho,
 
Mm atanilidhani unaalalamika kwa kuvamiwa kwenye kiwanja chako kumbe sala tu ..acha kutuonea wacha watu wamlilie mungu ulitaki uliliwe wew
Huyo Mungu gani anayependa kelele? Hujiulizi kwanini watu wenye maombi makali huenda mahala tulivu kama milimani? Pia tunaambiwa maombi tulivu kama usiku wa manane huwa na nguvu zaidi?
 
Wachawi wanaogopa kelele za kumuomba Mungu.

Jina la Yesu likitajwa wanajificha uvunguni.

Injili iendelee kutandikwa kwa kelele mpaka wachawi wote wanyanyue mikono juu!
 
Nina kaeneo kangu nje kabisa ya mji, ambako ninalima na kufuga kiaina. Sifa moja ya huku ni ukimya wake. Hivyo niliamua kuweka kakibanda ambako ninalala siku nikiamua kuja, nina lala huku, ili kujitibu na kelele za mjini.

Sasa leo nimekuja, nakuta kelele za ajabu. Kumbe kuna kanisa limefunguliwa. Watu wanasali kwa kulia, kuimba na kupiga makelele.

Hivi walokole hamuwezi sali bila kupigia watu kelele?

Ndio maana wanaojiita manabii wanawaibia bila kupiga kelele kwa kupigwa uongo wa watoe pesa bwana atatenda miujiza. yaani wanatoaje na bwana anakaaje kimya bila kujibu!
 
Nina kaeneo kangu nje kabisa ya mji, ambako ninalima na kufuga kiaina. Sifa moja ya huku ni ukimya wake. Hivyo niliamua kuweka kakibanda ambako ninalala siku nikiamua kuja, nina lala huku, ili kujitibu na kelele za mjini.

Sasa leo nimekuja, nakuta kelele za ajabu. Kumbe kuna kanisa limefunguliwa. Watu wanasali kwa kulia, kuimba na kupiga makelele.

Hivi walokole hamuwezi sali bila kupigia watu kelele?
Sio walokole tu hata waislamu nao wana makelele sana mjini hasa hasa alfajiri wanapiga sana makelele na ule wakati wanafunga huwa wanapiga sana makelele mida ya saa tatu tatu usiku ile wanaita talaweli noma saana yaani.
 
Ukweli mchungu ni kwamba ndugu zetu Walokole mmekuwa too much manake utasema Mungu ni kiziwi!! Hivi na yale mangoma yanayopigwa usiku kucha yakisindikizwa na powerful speakers ni ibada ile?! Nyie mnaotetea ni kwa sababu mnapiga hayo makelele kwenye maeneo ya wenzenu! Mnatoka mtaa A ukiacha wanao wamelala kisha mnaenda kupiga makelele mtaa Y na kuwafanya wengine wasilale!!
 
Wachawi wanaogopa kelele za kumuomba Mungu.

Jina la Yesu likitajwa wanajificha uvunguni.

Injili iendelee kutandikwa kwa kelele mpaka wachawi wote wanyanyue mikono juu!
Nilisoma ushuhuda mmoja hapa kuwa, wachawi wote huwa ni wachamungu sana ili kutake cover! Nikukumbushe tu kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha mshikadini na muamini nguvu za giza, sababu watu hao wote huongozwa na imani na sio fikra yakinifu!
 
Naunga mkono hoja, Mimi nasali makanisa ya kilokole. Ukianzisha sehemu ya ibada mtaani anza kuwahibiria majirani zako kwanza, mkikesha ni vizuri sauti zisikwaze majirani kwani kumkwaza mtu ni dhambi inayo hitaji maombi ya rehema, ni kweli ufalme wa Mungu hutekwa na wenye nguvu lakini ni nguvu ya imani na kutenda mapenzi ya Mungu, kuutafuta uso wa Mungu na kujenga ufalme wa Mungu lakini neno la Mungu halitubii kujenga ufalme wa Mungu kwa makelele, ikiwa ni kwa siku chache sawa lakini kama ni taratibu za ibada za kila wiki kukesha kwa sauti kubwa na kukera majirani ni kujirekebisha haraka na kuomba toba.
 
Nilisoma ushuhuda mmoja hapa kuwa, wachawi wote huwa ni wachamungu sana ili kutake cover! Nikukumbushe tu kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha mshikadini na muamini nguvu za giza, sababu watu hao wote huongozwa na imani na sio fikra yakinifu!
watu kama nyie ndo mjengewe sanamu za ukumbusho aisee bonge la pointi mkuu
Wanadhani wachawi wanaogopa maombi thubutu kuna Huyo mama ni mwinjilisti village kwetu na anaomba sana sana ,lakini ni mwanga hatari alishikwa kwenye vilinge na wajuba wa ndumba!
 
Wodi za kuzalisha watoto hospitalini zina kelele nyingi za watoto waliozaliwa na furaha za wamama baada ya kumleta kiumbe mpya duniani.
Usije taka hii ward iwe kimya hilo haliwezikani. Ukitaka ukimya na utulive huku kabaridi ka umbali kakikupuliza, hali hiyo inapatika mortuary pekee.
Hamia huko utafarijika sana kwa utulivu.
 
Wewe ndugu ulisikia wapi wodini zikawekwa speaker ili majirani wasikie sauti za vichanga? Hata ukiwa geti la hospitali huwezi sikia sauti za watoto. Nyie kanisani kwanini mnaweka maspeaker mtupigie kelele tusiohusika?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom