Inaonekana hunijui vizuri, pitia post zangu karibia zote, msimamo wangu uko wazi kuhusu muda wa kiongozi wa kuchaguliwa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Siamini kiongozi yoyote wa kuchaguliwa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Kiongozi yoyote akikaa madarakani ya miaka 10 humaliza ubora wake na kuanza kutawala kwa mizengwe, mfano Nyerere, Mugabe, Gaddafi, Museveni nk. Kwenye list hiyo Mbowe yumo.
Toka uchaguzi wa 2015 Mbowe ampokee yule mzee tapeli wa kisiasa na kumpa nafasi ya kugombea urais, nilimpuuza kabisa. Na mimi ni mmoja wa washabiki wa CDM tunaosema wazi wazi kuwa Mbowe hastahili tena kuwa kiongozi wa CDM. Na sina popote ninapomsifia huyo Mbowe baada ya blunder ya Lowassa ile 2015.