Sinema sakata la LUGUMI: Mashine za utambuzi wa alama za vidole zaanza kufungwa kimya kimya

Sinema sakata la LUGUMI: Mashine za utambuzi wa alama za vidole zaanza kufungwa kimya kimya

Wakati sakata la kampuni ya LUGUMI Enterprises likiendelea kutikisa nchi, mashine za utambuzi wa alama za vidole, zimeanza kufungwa katika mikoa kadhaa ikiwamo ya Dodoma na Geita.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kwamba juzi mashine hizo zilifungwa katika vituo vya polisi vya wilaya za Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma na kazi hiyo ilitarajiwa kufanywa mjini Dodoma jana. Pia, vyanzo vya habari kutoka mkoani Geita vimeithibitishia Mwananchi kwamba mashine hizo zimefungwa katika vituo vitano vya polisi.

Kampuni ya LUGUMI iliingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011 kufunga mashine hizo kwenye vituo 108, lakini hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anamaliza ukaguzi, ni vituo 14 tu vilikuwa vimefungwa mashine hizo.

Taarifa hiyo ya CAG ililistua Bunge na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliunda kamati ndogo ili kuzunguka mikoani kuthibitisha taarifa hiyo ya mkaguzi mkuu.

Lakini wakati kamati hiyo ikiwa imepewa kazi hiyo, Mwananchi imeambiwa kuwa mashine hizo zinafungwa.

“Tulikuwa na LUGUMI hapa,” alisema mmoja wa watoa habari waliozungumza na Mwananchi.

“Vijana wa LUGUMI walikuwa wanafunga mashine, wameondoka kwenda Kongwa. Kesho (jana) watakuwa Dodoma.”

Imeelezwa kuwa vijana wanaofunga mashine hizo walikwenda Mpwapwa wakitokea Kibaha mkoani Pwani. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, katika Mkoa wa Geita, mashine hizo zimefungwa wilaya za Nyang’hwale, Chato, Geita, Bukombe na Mbogwe.

Alipotafutwa kutoa ufafanuzi wa kazi ya ufungaji mashine hizo, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Latson Mponjoli alisema suala hilo ni la kitaifa hivyo kutaka watafutwe viongozi wa kitaifa.

“Mimi nitazungumzia nini kuhusiana na LUGUMI? Suala hilo ni la kitaifa unaniuliza mimi? Hilo suala mtafute waziri mwenye dhamana au IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi) ndiyo wenye mamlaka ya kulizungumzia jambo hilo,” alisema Kamanda Mponjoli.

Lakini juhudi za kumpata IGP Ernest Mangu kwa simu hazikufanikiwa badala yake simu yake ilipokewa na msaidizi wake. Mwandishi alipoanza kuzungumza naye, simu yake ilikatika.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alisema hataki kujibu maswali yanayohusu kampuni hiyo na kwamba mwandishi awasiliane na kampuni hiyo. “Taarifa za LUGUMI kawaulizeni LUGUMI wenyewe, sipendi kujibu maswali ya kijinga na upumbavu, kwa sababu nimekwenda vituoni mwenyewe nimejionea,” alisema na kukata simu. Alipopigiwa simu tena ili aeleze amejionea nini hakupokea.

Hata hivyo, hakuna mtu yeyote kutoka LUGUMI ambaye amekuwa tayari kuzungumza ingawa vyanzo vya habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi vimesema kwamba utekelezaji wa kazi ya kufunga kompyuta hizo aina ya Dell umeanza.

“Unajua hili ni agizo na amri ya kamishna mmoja wa makao makuu. Kuna gari lililofuata vifaa hivyo makao makuu na kompyuta hizi zilifika hapa Jumatano na zikafungwa Alhamisi, lakini kama nilivyosema haziwaki na hata askari hawana mafunzo ya kuzitumia,” alisema mpashaji mwingine aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Mtoa taarifa huyo alisema uharaka wa kufunga mashine hizo unafanywa ili kujiandaa kwa ukaguzi wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wanaotarajiwa kupita wilayani na mikoani kuthibitisha uwepo wa mashine hizo. Kwamba watakapofika wakaguzi wadhani kwamba vifaa hivyo vilikuwapo tangu awali wakati si kweli.

‘’Ndugu yangu, huwezi kuamini kompyuta za LUGUMI zimewasili hapa mkoani kwetu (Geita), lakini sasa zimeletwa kwa lengo moja tu kuwahadaa wakaguzi kwamba zilikuwepo tangu awali wakati si kweli. Hizo kompyuta zililetwa Jumatano wiki iliyopita na zilifungwa Alhamisi na mbaya zaidi haziwaki, yaani ni mbovu,” alisema mtu huyo.

Mjumbe mmoja wa PAC aliwahi kulalamika kuwa kuna mchezo unachezwa wa kukwamisha kamati ndogo baada ya Bunge kuchelewa kutoa fedha za kuwezesha kazi ya ukaguzi kuanza kwa lengo la kutoa mwanya wa kufungwa kwa mashine hizo nje ya muda.

Juhudi za kumpata Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hillaly ili atoe ufafanuzi wa kazi hiyo kufanywa sasa tena na polisi wenyewe, hazikuzaa matunda. Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ndogo ya PAC iliyopewa jukumu la kuchunguza sakata la LUGUMI kwa siku 30, alisema mambo yote yatakuwa kwenye ripoti yao. “Kama wanafunga mashine au hawafungi hilo sijui, we subiri tu tumalize kazi tutatoa ripoti,” alisema.

Habari zinasema tayari kamati hiyo iliyogawanywa katika makundi matatu imekamilisha ukaguzi katika Mkoa wa Dodoma.

Kamati ya PAC ndiyo iliyoibua sakata hilo katika vikao vya kamati vya Aprili, ikinukuu ripoti ya CAG ya mwaka 2014/2015 kwamba kampuni hiyo iliyoingia mkataba na Polisi kufunga mashine hizo haikuwa imekamilisha kazi hiyo.

Pamoja na kutokamilisha ufungaji mashine hizo, LUGUMI ilishalipwa Sh34 bilioni sawa na zaidi ya asilimia 90 ya jumla ya malipo ya Sh37 bilioni za mkataba, jambo ambalo wabunge wanaona ni viashiria vya ufisadi katika Jeshi la Polisi.

Katika sakata hilo, pia anatajwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga akitakiwa ajiuzulu kwa madai kuwa ana hisa kwenye kampuni ya Infosys, ambayo ilitoa ushauri wa kitaalamu kwenye mradi huo, ikiwa imeombwa na kampuni ya Kimarekani ya Biometrica ambayo iliipa Dola 75,240 (sawa na zaidi ya S150 milioni).

Hata hivyo, Infosys imenukuliwa ikidai kuwa Kitwanga alishajiondoa kwenye uendeshaji wa kampuni hiyo mwaka 2010 na tangu wakati huo hajakanyaga kwenye ofisi zao.

Sasa kama hiyo ni kweli kwa nini Waziri bado yupo kazini, ina maana hajui maana ya conflict of interest regardless ya kuwa na shares kwenye kampuni au amekwisha toka, hili si jambo dogo halafu wanaendelea ku install mashine wakati mkataba wao unaonyesha kazi hiyo ilikamiliza siku nyingi zilizo pita - wapi mahadiri na uwajibikaji hapa, je tu na set precedent hipi kwa watu Watanzania wengine wenye dhamana ya kusimamia vitu vyetu muhimu vya kutuletea maendeleo, kila mtu atakuwa anajiona yuko huru kufanya lolote bila ya kuchukuliwa hatua yoyote mradi uwe na right connection utapeta tu!
 
Kamati ya bunge italeta report bungeni..

Hicho kihelehele cha kumtaka rais achukue maamuzi unakitolea wapi.

Ndio maana mnaitwa kuku wa kizungu.
Nyie ni vifaranga vya kanga lazima tuweke Tahadhali hamuaminiki kabsa kila kona Lugumi kapenyeza Rishwa hata Wewe umefuata nini hapo Kwa Lugumi Kama si njaa imekupeleka ukamtetee.
 
Mifumo hiyo kuifunga ni rahisi kinoma. Cha msingi ni networking tu ili mashine zote ziwe synchronised na server. Sasa siasa zenu za kihafishina ndio zinafanya muwe munauliza idiotic questions.
Ingekua rahisi kinoma angepewa baba ako azifunge mkuu

Kama huna data jitahd wakat mwngne kukaa kimya tu
 
Lugumi amesababisha mwandishi wa habari kutukanwa (mpumbavu na mjinga)...weee Lugumi weeee
 
Nyie ni vifaranga vya kanga lazima tuweke Tahadhali hamuaminiki kabsa kila kona Lugumi kapenyeza Rishwa hata Wewe umefuata nini hapo Kwa Lugumi Kama si njaa imekupeleka ukamtetee.
Mkateni kwanza lowasa kama tulivyomkata sisi ccm.
 
Sasa kama hiyo ni kweli kwa nini Waziri bado yupo kazini, ina maana hajui maana ya conflict of interest regardless ya kuwa na shares kwenye kampuni au amekwisha toka, hili si jambo dogo halafu wanaendelea ku install mashine wakati mkataba wao unaonyesha kazi hiyo ilikamiliza siku nyingi zilizo pita - wapi mahadiri na uwajibikaji hapa, je tu na set precedent hipi kwa watu Watanzania wengine wenye dhamana ya kusimamia vitu vyetu muhimu vya kutuletea maendeleo, kila mtu atakuwa anajiona yuko huru kufanya lolote bila ya kuchukuliwa hatua yoyote mradi uwe na right connection utapeta tu!
mkuu kuna jitihada nyingi zinafanyika kumwoka Kitwanga mojawapo ni wachakachuaji kuingia brela kumtoa kitwanga kwenye kampuni ya infosys na kuonyesha kuwa alitoka tokea zamani Yaani 2010, hivyo kujiondoa kwenye hiyo biashara , pili mashine zinafungwa chapchap kisha watazuga walizifunga zamani lakini wamepita kuzikagua tu, yaani badala ya kulisadia Taifa ili iwe mfano Kwa kampuni zingine wapo busy kumlinda Lugumi na kitwanga asitumbuliwe JIPU .
 
Sasa hii serikali iangushwe kwa kuwadharau Watanzania na kuwaambia uwongo kama wapumbavu. Watanzania wamedharauliwa sana na hii serikali na ndiyo sababu inafanya inachotaka bila kujali sheria na katiba ya nchi.

TUNAOMBA KATIBA MPYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11111

Wanasiasa wanalindana? Watumishi wa umma wanatumbuliwa.
 
Mkateni kwanza lowasa kama tulivyomkata sisi ccm.
Richmond ni ya Kikwete na ccm Kama ccm hawakumkataa Lowasa alikuwa na wafuasi wengi Dodoma , aliyemkata Lowasa ni Kikwete mwenyewe alikwenda na majina Mfukoni mwake akitaka Membe awe Rais lakini wajumbe Timu Lowasa wakaamua kumkomesha wakamchagua Magufuli ambaye hakuwa Chaguo la Kikwete ndiyo maana alipoingia ikulu kapiga pin baadhi ya Madili ya Kikwete likiwemo hili la Lugumi lakini Kikwete akaenda ikulu kulalamika ndipo Magufuli anahaha namna ya kumwoka Lugumi .
 
Wanasiasa wanalindana? Watumishi wa umma wanatumbuliwa.
Kuna jamaa anaitwa Lizabon sasa amekuwa Fisadi Kwa pesa za kuwatetea wezi yeye kutwa huzunguka Kwa Majipu kuchukua pesa Kwa ajili ya kuwatetea mitandaoni .
 
N
mkuu Lugumi yeye analindwa sana licha ya kupewa mapesa mengi kinyume na bei halisi bado wanabariki Uongo , Yaani anapita mda huu anafunga vifaa kwenye baadhi ya vituo kisha watakuja na maneno kuwa vilifingwa zamani tena vipo kwenye vituo vyote.
Ndio maana mob justice haitekelezeki kwake maana ana ulinzi wa wasimamizi wa sheria
 
Richmond ni ya Kikwete na ccm Kama ccm hawakumkataa Lowasa alikuwa na wafuasi wengi Dodoma , aliyemkata Lowasa ni Kikwete mwenyewe alikwenda na majina Mfukoni mwake akitaka Membe awe Rais lakini wajumbe Timu Lowasa wakaamua kumkomesha wakamchagua Magufuli ambaye hakuwa Chaguo la Kikwete ndiyo maana alipoingia ikulu kapiga pin baadhi ya Madili ya Kikwete likiwemo hili la Lugumi lakini Kikwete akaenda ikulu kulalamika ndipo Magufuli anahaha namna ya kumwoka Lugumi .
Kigezo cha ccm ni uadilifu na uchapakazi na siyo kuwa na wafuasi wengi..

Kigezo cha kuchukua mgombea hata Kama ni fisadi hutumiwa na chadema tu dunia nzima..

Shame on you chadema.
 
Namwomba Mungu amwezeshe Rais kuwa na ujasiri wa kuona maovu yote hasahasa makubwa ambayo yanapigiwa kelele sana. Asisite kutumbua hayo majipu makubwa.
mwombe akishatumbua ukupe usaha Wake, unaweza kukusaidia
 
mkuu kuna jitihada nyingi zinafanyika kumwoka Kitwanga mojawapo ni wachakachuaji kuingia brela kumtoa kitwanga kwenye kampuni ya infosys na kuonyesha kuwa alitoka tokea zamani Yaani 2010, hivyo kujiondoa kwenye hiyo biashara , pili mashine zinafungwa chapchap kisha watazuga walizifunga zamani lakini wamepita kuzikagua tu, yaani badala ya kulisadia Taifa ili iwe mfano Kwa kampuni zingine wapo busy kumlinda Lugumi na kitwanga asitumbuliwe JIPU .

Mkuu..
Mimi naungana Na waziri Kivuli/Mh.Lema..
Kua kunamchezo mchafu wakumchafua Mh.Kitwanga..
Mkuu Funza kwa ufupi jaribu kudadisi ni nani hasa Aliwalipua Lugumi na syndicate Lake..
 
Sasa huo ni ujeuri wa kupindukia dhidi yetu wanyonge jamani. Mungu kwanini sisi tuonewe hivi. Oh my dear God help us
Vumilia tu Mkuu! Poleee.... Watanzania ndo wametaka iwe hivyo, Watanzania Hawa ni tofauti na jamii yoyote duniani, wanazalishwa Tanzania tu! Na ni kwa matumizi ya Tanzania tu! Wakienda nje wanapata shida Sana, wenyewe hawajari......wewe tafuta tu ugali wa wanao! Ya wenye nchi waachie wananchi!
 
Kigezo cha ccm ni uadilifu na uchapakazi na siyo kuwa na wafuasi wengi..

Kigezo cha kuchukua mgombea hata Kama ni fisadi hutumiwa na chadema tu dunia
Kigezo cha ccm ni uadilifu na uchapakazi na siyo kuwa na wafuasi wengi..

Kigezo cha kuchukua mgombea hata Kama ni fisadi hutumiwa na chadema tu dunia nzima..

Shame on you chadema.

Shame on you chadema.
hicho kigezo umekikariri tu kichwani lakini Kikwete alitaka Membe awe Rais isipokuwa wafuasi wa Lowasa walimkomesha ndipo wakamchagua Magufuli lakini sasa kaanza kuharibu alianza Vizuri sana, kitendo cha kuanza kuwasikiliza nyie watetezi wa Wizi ndicho kitamharibia magufuli , nyinyi mnawatetea wezi wote , kaanzia NSSF , IPTL , Chenji ya Rada , bomba la Gesi , escrow , Lugumi na kila Aina ya wizi mnautetea Yaani Laana ya watanzania itawatafuna sana.
 
Sumu ya maendeleo ya Watanzania kwa sasa ni Lizabon na Timu yake ambao Kwa sasa wamekuwa Mafisadi wakubwa kupitia utetezi wa Wezi , kutwa wanazunguka Kwa Lugumi na Majipu mengine kuchukua pesa za kuwatetea .
 
Huu Uzi utanifanya nivunje sheria ya makosa ya mitandao, ngoja nnitoke humu......manake Kuna mashoga humu wanamtetea Lugumi!
 
Kama wangekuwa serious ni kazi ya miezi 8 mpaka mwaka ina maana mwaka 2012 walipaswa wawe wamekabidhi kazi ,

funza kama ww umeliona hili, nashangaa hd leo TAKUKURU na PPRA hawajatoa tamko lolote?

Tutajie vipengele vya Mkataba Baina ya Lugumi na Police juu ya ni lini haswa ukomo wa ufungwaji wa hizo mashine

labda ww utakuwa nazo!.
 
Back
Top Bottom