Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Sawa na hongereni kwa kupanda daraja, pia mawazo mengi yatakuja kipindi mkishaanza ligi kwa sasa watakaotoa mawazo ni wale waliokuwananyi bega kwa bega kuanzia chini.

Mimi binafsi nakiri sikuwafahamu sawa sawa nasubiri mkianza ligi nitakuwananyi pamoja kwa kila hatua hapo ndio tutaona mapungufu na ushauri juu ya nini mfanye au pongezi zetu.

Nawatakieni mafanikio mema katika msimu ujao.

Asante sana mkuu. Umeeleweka vema kabisa. Karibu tuwe pamoja.
 
Kwanini mlibadili jina?

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app

Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
 
Boresheni mapungufu yenu yaliyofanya mpaka mkashuka daraja

Then undeni scouting team nzuri za kutafuta vipaji cha wachezaji kwa maendeleo ya timu yenu

Epukeni sarakasi za ndugu wa Kariakoo.

Hatujawahi kushuka daraja kwa sababu hii ndio mara yetu ya kwanza tunaenda kushiriki Ligi Kuu, pengine unatuchanganya na Singida United kama wengine kwa sababu ilikuwa ni timu kutoka Singida pia.

Mengine tunayapokea na tutayafanyia kazi mkuu.

Asante kwa ushauri.
 
Nikupongeze kwa jambo jema hili la kutaka kupata moani ya wadau wa mchezo wa moira wa miguu.
Mie ningependekeza machache yafuatayo.

1) kuweni wazalendo...ni ujinga kujaza kikosi kizima kina jaa foreign players. Tunajua the man behind the team anapenda kuvaa scaff yenye rangi ya bendera yetu basi huo uzalendo usiishie kwenye scaff lekee yake bali uonyeshwe kwa vitendo kwa kuwaapa ajira vijana wa kitanzania.

2) acahane i na makocha wa kigeni. Tafuteni kocha mzawa mpeni timu na mumuamini. Zile story za mgeni mnalipa million ishiri i lakini kocha mzawa mnamkopa huu ni ujinga. So tafuteni makocha wazawa. Mfano mzuri ethiopia majuzi wamewapiga waarabu wakitumia wachezaji wanaocheza ligi yao na kocha mzawa.

3) ingieni na mentality kuwa ni ni project ya muda mrefu msitake pupa mapema mtakuwa frustrated. Build a club not a team.

Yangu ni hayo tuu.

Mkuu mzabzab, japo hatujaelewa unamlenga nani lakini nifafanue tu hakuna any man behind the team zaidi ya Sekretarieti na Kamati za Uongozi. Usajili wa timu uko public na haiko chini ya umiliki wa mtu binafsi.

Kinyume na hapo, mapendekezo yako ni ya msingi sana. Tunayachukua.
 
Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
mi naona mlibadili jina baada ya kuona nyinyi na mdhamini mkuu wa ligi mna mutual interest.
 
Mkuu mzabzab, japo hatujaelewa unamlenga nani lakini nifafanue tu hakuna any man behind the team zaidi ya Sekretarieti na Kamati za Uongozi. Usajili wa timu uko public na haiko chini ya umiliki wa mtu binafsi.

Kinyume na hapo, mapendekezo yako ni ya msingi sana. Tunayachukua.
Sawa cha msingi sii kuna uongozi. Ni vyema mkayafanyia kazi hayo mapendekezo. Its high time sasa vilabu vianze kutumia makocha wazawa na pia wachezaji wazawa.

Mkitekeleza hilo basi mtakuwa mfano wa kuigwa. Wekeni target kuwa in 5 to 7 years tunataka kushinda ligi kuu na kocha mzawa. This hould be the target.

Patrice motsepe aliweka target ya kushinda caf champions league na kocha mzawa na alifanikiwa. Tuwawezeshe makocha wetu na pia wachezaji wetu. Hivi vitu vinawezekana. U just have to hire the right people
 
Ushauri mzuri huu. Asante sana.
 
Mbona umejipa Vyeo vingi hivyo??yaani wewe ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,pia ni Afisa Habari na Msemaji wa Timu,una kiwango gani cha Elimu??una Shahada ya Mass Communications au ni kama Manara tu Vyeti ni mdomo wako??nadhani ungetafuta Msaidizi na sio kujipa Vyeo vyote peke yako
 
Sijajipa, nimepewa. Ndiyo, nina shahada ya Mass Communication + Public Relations.

Majukumu ya nafasi tajwa yanaingilia kwahiyo hakuna neno, nayamudu.

Asante kwa maoni mazuri mkuu.
 
Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
Kwahiyo kama DTB iliamua isiendelee na ushindani mdhamini wa club ni nani?
 
View attachment 2263057

Watu wa Soka,

Naitwa Hussein Massanza. Ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano; Pia Afisa Habari na Msemaji wa Singida Big Stars FC (zamani DTB FC).

Timu yetu imefanikiwa kupanda daraja na kufuzu kucheza Ligi Kuu kuanzia msimu ujao wa 2022/2023, hivyo nitumie fursa hii kuwashukuru mashabiki wetu wote tangu tukiwa tunaitwa DTB FC, wanahabari na wadau wengine kwa sapoti mliyotupatia. Tuendako ni kuzuri zaidi, tunaomba muendelee kutusapoti kwa nguvu zaidi.

Kupitia uzi huu maalum; nitapokea maoni, ushauri na mapendekezo yatakanisadia mimi binafsi katika kutekeleza majukumu yangu, lakini pia yatakayoisadia timu yetu kufanya vizuri, ikizingatiwa sisi ni wageni Ligi Kuu na malengo yetu ni kufanya vizuri kama tulivyokimbiza kule Daraja la Kwanza (Championship).

Simu/WhatsApp: +255 713 475715

Karibuni sana.
Msiendekeze utawi wa Utopolo ska Chura Africans Yanga.
 
Hussein Massanza mnahakika mmejipanga vizuri,mkipata mfadhili au muwekezaji akaweka Bilioni kadhaa kwenye timu yenu akitanuka kama ilivyokua Stendi Utd ya Kahama?
 
Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
Sababu dhaifu kabisa hii embu sema ukweli Masanza
 
Back
Top Bottom