Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Hiyo timu kama imeshatekwa na Mwigulu mjiandae kuwa njia ya kukuza wacezaji wa Yanga mpaka wapatikane kina feitoto wengine. Yaani mtabaki kuwa average club tuu chonde msime=wache mwigulu aiteke hiyo club
 
Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
Kwahiyo ndio kusema DTB wameiuza timu na sasa ina wamiliki wapya? Kama jibu ni ndio hao wamiliki wapya ni kina nani?
 
Mwendelezo uwe ni ule ule, msibweteke na kuijiona mmeshafanikiwa,as team jitahidini mno muwe na timu za under 17yrs&21yrs, muwekeze sana huko ili ziwe feeder kwa wachezaji wa first team, kuweni na scouts wazuri hasa ndani ya mkoa na Kanda yenu, pelekeni timu kwa wananchi ili wajione na wa feel proud kuwa sehemu ya team (supporting yao ni key hapa),nidhamu ndani ya team ni muhimu kuanzia uongozi hadi cleaner wa team, kila mtu aheshimiwe na mwisho good luck
Pesa hizo watatoa wapi?. Unafikiri hawatamshtukia kule?
 
View attachment 2263057

Watu wa Soka,

Naitwa Hussein Massanza. Ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano; Pia Afisa Habari na Msemaji wa Singida Big Stars FC (zamani DTB FC).

Timu yetu imefanikiwa kupanda daraja na kufuzu kucheza Ligi Kuu kuanzia msimu ujao wa 2022/2023, hivyo nitumie fursa hii kuwashukuru mashabiki wetu wote tangu tukiwa tunaitwa DTB FC, wanahabari na wadau wengine kwa sapoti mliyotupatia. Tuendako ni kuzuri zaidi, tunaomba muendelee kutusapoti kwa nguvu zaidi.

Kupitia uzi huu maalum; nitapokea maoni, ushauri na mapendekezo yatakanisadia mimi binafsi katika kutekeleza majukumu yangu, lakini pia yatakayoisadia timu yetu kufanya vizuri, ikizingatiwa sisi ni wageni Ligi Kuu na malengo yetu ni kufanya vizuri kama tulivyokimbiza kule Daraja la Kwanza (Championship).

Simu/WhatsApp: +255 713 475715

Karibuni sana.
Hongereni Sana na karibuni ligi kuu, tunaamini Moto wenu utakua ni ule ule....👊👊👊...

Kumbukeni kuwapa nafasi wachezaji vijana mlionao walioonyesha uwezo ili kuendelea kuwajengea morali na ari ya kujituma zaidi na kuweni makini na sajili zenu muhimu, tulieni na sajilini kulingana na mahitaji yenu ya timu acheni pupa.

msijisahau mkaingia kwenye siasa za Yanga na Simba (hata kama baadhi yenu ni washabiki/wanachama wa hivyo vilabu).

Ligi itakapoanza tumieni vizuri uwanja wenu wa nyumbani ili kujiongezea wigo wa mashabiki.

Mengine tutaendelea kujazana siku zinaposonga ila hongereni Sana na kila laheri.

Asante kwa kutuwekea namba, tutapeana mawazo ya hapa na pale.
 
Asante sana kwa maoni mazuri. Karibu tuyajenge muda wowote.
 
Hiyo timu kama imeshatekwa na Mwigulu mjiandae kuwa njia ya kukuza wacezaji wa Yanga mpaka wapatikane kina feitoto wengine. Yaani mtabaki kuwa average club tuu chonde msime=wache mwigulu aiteke hiyo club
Imetekwaje wakati timu ina bodi, menejimenti na kamati zake za utendaji?
 
Kama mtahitaji scouting ya wachezaji Nina viungo wawili very talented and promising naweza kuwapa number zako waje kuharibu trial

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo kama DTB iliamua isiendelee na ushindani mdhamini wa club ni nani?

Klabu kwa sasa inaendeshwa na bodi ya Singida Big Stars ambayo ina wajumbe wake na kamati zake za utendaji.
 
Tambueni kuwa bado mnasafari kubwa msije bweteka.
Mpira wa sasa ni biashara pia kwaiyo unaitaji uwekezaji mzuri ili kupata faida.
Aliye kupandisha anaweza kukushusha pia. Kwaiyo msidharau wachezaji wenu wapeni hamasa zaid za kufikia ndoto zao ili na ninyi mfikie malengo yenu.
Msichanganye mpira na siasa na rudia tena "MSICHANGANYE MPIRA NA SIASA"

Ni ayo tu
 
Bora mkawaomba tu TFF wawasaidie namna ya kulirejesha lile jina lenu la awali la Singida United.

Hilo jina la Singida Big Stars limekaa kitoto sana.

Singida United halikuwahi kuwa jina letu. Tumeshafafanua kuwa jina letu la awali ni DTB FC.

Asante kwa maoni mkuu.
 
Tambueni kuwa bado mnasafari kubwa msije bweteka.
Mpira wa sasa ni biashara pia kwaiyo unaitaji uwekezaji mzuri ili kupata faida.
Aliye kupandisha anaweza kukushusha pia. Kwaiyo msidharau wachezaji wenu wapeni hamasa zaid za kufikia ndoto zao ili na ninyi mfikie malengo yenu.
Msichanganye mpira na siasa na rudia tena "MSICHANGANYE MPIRA NA SIASA"

Ni ayo tu

Asante sana mkuu. Tumekuelewa.
 
Hatujawahi kushuka daraja kwa sababu hii ndio mara yetu ya kwanza tunaenda kushiriki Ligi Kuu, pengine unatuchanganya na Singida United kama wengine kwa sababu ilikuwa ni timu kutoka Singida pia.

Mengine tunayapokea na tutayafanyia kazi mkuu.

Asante kwa ushauri.
Daaaah hata mie binafsi naielewa Singida,,,,ulipotaja timu kupanda daraja akili ya wote na hata mie kuwa ni Singida united,,,,,Hakikisha hilo wadau wanalijua,,,,kuthibitisha hilo Kuna mchangiaji hapa nae amemtaja mvaa skafu ya bendera ya taifa ni mdau wa Singida united
 
Sijakosea mkuu, yule mvaa skafu ndie kainunua hii incase ulikuwa hujui.
 
Back
Top Bottom