View attachment 2263057
Watu wa Soka,
Naitwa Hussein Massanza. Ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano; Pia Afisa Habari na Msemaji wa Singida Big Stars FC (zamani DTB FC).
Timu yetu imefanikiwa kupanda daraja na kufuzu kucheza Ligi Kuu kuanzia msimu ujao wa 2022/2023, hivyo nitumie fursa hii kuwashukuru mashabiki wetu wote tangu tukiwa tunaitwa DTB FC, wanahabari na wadau wengine kwa sapoti mliyotupatia. Tuendako ni kuzuri zaidi, tunaomba muendelee kutusapoti kwa nguvu zaidi.
Kupitia uzi huu maalum; nitapokea maoni, ushauri na mapendekezo yatakanisadia mimi binafsi katika kutekeleza majukumu yangu, lakini pia yatakayoisadia timu yetu kufanya vizuri, ikizingatiwa sisi ni wageni Ligi Kuu na malengo yetu ni kufanya vizuri kama tulivyokimbiza kule Daraja la Kwanza (Championship).
Simu/WhatsApp: +255 713 475715
Karibuni sana.