Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Singida Big Stars tumefuzu Ligi Kuu Tanzania Bara, tupeni ushauri

Mfano mzuri ni timu yetu ya taifa, wachezaji ni wakawaida kabisa yani viwango vyao ni vidogo ndiyo maana hata kutoka nje ni changamoto.

Pili wachezaji wa Kitanzania 90% hawajitambui mfano:- Ibrahim Ajib.

Angalia Morrison licha ya ujinga ujinga wake ila anawatesa vigogo wa soka hapa nchini.
Viwango ni vidogo sii ndio tunarudi kwenye lile suala la kutoandaliwa. Sie tunataka mchezaji toka ndodo cup wapi uliona hiyo. Lazima tutambue kuwa the dedication and attention that goes into creating a professional footballer sio kitoto.

Tukiendelea kusema hawajitbui haitusaidi ndio kila leo tunaishia kuwa kichwa cha mwenda wazimu. Tufauate misimgi ya football basi. Haya mambo ya awezekana sana tuu. Ni nia. Watu walikuwa na hope kubwa na azam fc lakini nao zimeingia siasa za ajabu mpaka unashindwa elewa hii timu ni wanauza wachezaji au wanagombania ubungwa?

Huyo morrison ni talented player just like ajib but hana character ya kucheza professional football. Kwa nini wanawika hapa kwetu wakiend top leagues wanashindwa? Watu huku dnt entertain ujinga. Siwezi kukulipa million mia kwa wiki alafu unakuja umelewa au indiscipline ga aina yoyote ile.
 
Ushauri:-
1. Kati ya Kulwa na Ndoto msichague mmoja wa kumkazia.

2. Muwe watu wa kufanya fitna.

3. Msiwe watu wa porojo mitandaoni, wekezeni kwenye vitendo zaidi hapo ndo mtavuna mashabiki kwa wingi.

Asante kwa ushauri mzuri
 
Fikiria Biashara utd anashiriki kimataifa halafu anakosa nauli. Kushindwa kusafiri imewahi fanywa na Mtibwa pia.
Kwa hiyo jiandaeni mapema maana kitendo cha kushiriki ligi kuu muda wowote mnakuwa wawakilishi kimataifa.
Angalia mfano wa Coastsl union akichukua Azam shirikisho kwa kumfunga yanga anakuwa mwakilishi kimataifa , sasa kama hakujiandaa mapema ya akina Biashara utd yatajirudia.

Klabu nyingi za kibongo zikiwemo hizi Simba na Yanga hazina timu za vijana za kueleweka. Ni uhuni tu wanafanya wa kukusanya vijana mtaani kunapokuwa na mashindano ya timu za vijana.
Kama bajeti ipo nendeni kwa akina Asec mimosas mkajifunze jinsi ya kukuza vijana na kuwa professional. Hamtamani kuuza mchezaji kwa bilioni hata 2? Wenzenu Asec wameuza mchezaji kwa bilioni 6. Lakini mnafikiri mchezaji wa mtaani umlete ligi kuu halafu umuuze kwa bilioni 1? Ni ngumu sana na ndio maana tuna Samatta mmoja tu.

Kila la kheri ktk ligi kuu na huko kimataifa mkipata uwakilishi.
 
Fikiria Biashara utd anashiriki kimataifa halafu anakosa nauli. Kushindwa kusafiri imewahi fanywa na Mtibwa pia.
Kwa hiyo jiandaeni mapema maana kitendo cha kushiriki ligi kuu muda wowote mnakuwa wawakilishi kimataifa.
Angalia mfano wa Coastsl union akichukua Azam shirikisho kwa kumfunga yanga anakuwa mwakilishi kimataifa , sasa kama hakujiandaa mapema ya akina Biashara utd yatajirudia.

Klabu nyingi za kibongo zikiwemo hizi Simba na Yanga hazina timu za vijana za kueleweka. Ni uhuni tu wanafanya wa kukusanya vijana mtaani kunapokuwa na mashindano ya timu za vijana.
Kama bajeti ipo nendeni kwa akina Asec mimosas mkajifunze jinsi ya kukuza vijana na kuwa professional. Hamtamani kuuza mchezaji kwa bilioni hata 2? Wenzenu Asec wameuza mchezaji kwa bilioni 6. Lakini mnafikiri mchezaji wa mtaani umlete ligi kuu halafu umuuze kwa bilioni 1? Ni ngumu sana na ndio maana tuna Samatta mmoja tu.

Kila la kheri ktk ligi kuu na huko kimataifa mkipata uwakilishi.

Asante sana kwa mtazamo huu na tahadhari. Tupo makini na tunaendelea kujipanga vizuri mkuu. Mungu akubariki kwa kutuombea kheri.
 
Ingieni mkataba na vunjabei au supplier wa jezi tz nzima mdesign jezi nzuri afu muipe promo na pia mjaribu kuifanya team iwe karibu na mashabiki
Kwa mlivokuja kwa kasi basi naona mtamaliza top 4 basi mjiandae kwenda huko duniani though realistically ni kama haiwezekani..ila
Hii big stars mhhhhh
Bora jina hata AFC singida
Jina limekaa ajabu mkubwa
Welcome NBC tutakua pamoja hapa jf
 
Hongera Husein, naimani kwakupitia kipaji chako utaipatia support nzuri na kujaza mashabiki wenye kadi za Singida Big Stars
 
Kwan mwigulu anasemaje si anamiliki kampuni ya kubeti na pia mabasi sas mtashindwa nn pesa hzo tayari nyie kazaneni kupambanaa
 
View attachment 2263057

Watu wa Soka,

Naitwa Hussein Massanza. Ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano; Pia Afisa Habari na Msemaji wa Singida Big Stars FC (zamani DTB FC).

Timu yetu imefanikiwa kupanda daraja na kufuzu kucheza Ligi Kuu kuanzia msimu ujao wa 2022/2023, hivyo nitumie fursa hii kuwashukuru mashabiki wetu wote tangu tukiwa tunaitwa DTB FC, wanahabari na wadau wengine kwa sapoti mliyotupatia. Tuendako ni kuzuri zaidi, tunaomba muendelee kutusapoti kwa nguvu zaidi.

Kupitia uzi huu maalum; nitapokea maoni, ushauri na mapendekezo yatakanisadia mimi binafsi katika kutekeleza majukumu yangu, lakini pia yatakayoisadia timu yetu kufanya vizuri, ikizingatiwa sisi ni wageni Ligi Kuu na malengo yetu ni kufanya vizuri kama tulivyokimbiza kule Daraja la Kwanza (Championship).

Simu/WhatsApp: +255 713 475715

Karibuni sana.
Mkiruhusu bosi wenu MADELU aingilie utendaji wa timu mtapotea kama ilivyopotea singida utd, fei toto alisajiliwa singida utd msimu huohuo madelu akampeleka yanga, tatizo karia anamuogopa madelu akaruhusu ule uhuni mwisho wa siku singida chali
 
Swali zuri. Baada ya kufuzu Ligi Kuu, Benki ya DTB iliamua isiendelee na ushindani kwenye masuala ya soka, badala yake ijikite zaidi kwenye kazi zake za kibenki. Hiyo ndio sababu tukaona tubadili jina kutoka DTB na kuwa Singida Big Stars FC.
Jiiteni SINGIDA UTD au SINGIDA FC
 
Jiiteni SINGIDA UTD au SINGIDA FC
Nimeongea hapo juu. Singida Big Stars jamani ni bendi ya mziki au timu ya basketball?

Wabadili jina haraka kabla ligi haijaanza.

Kwani kuna ubaya gani hata wakaiita Singida FC au jina la zamani Singida United?
 
Nikupongeze kwa jambo jema hili la kutaka kupata moani ya wadau wa mchezo wa moira wa miguu.
Mie ningependekeza machache yafuatayo.

1) kuweni wazalendo...ni ujinga kujaza kikosi kizima kina jaa foreign players. Tunajua the man behind the team anapenda kuvaa scaff yenye rangi ya bendera yetu basi huo uzalendo usiishie kwenye scaff lekee yake bali uonyeshwe kwa vitendo kwa kuwaapa ajira vijana wa kitanzania.

2) acahane i na makocha wa kigeni. Tafuteni kocha mzawa mpeni timu na mumuamini. Zile story za mgeni mnalipa million ishiri i lakini kocha mzawa mnamkopa huu ni ujinga. So tafuteni makocha wazawa. Mfano mzuri ethiopia majuzi wamewapiga waarabu wakitumia wachezaji wanaocheza ligi yao na kocha mzawa.

3) ingieni na mentality kuwa ni ni project ya muda mrefu msitake pupa mapema mtakuwa frustrated. Build a club not a team.

Yangu ni hayo tuu.
Mbona Zanzibar team zao wanatumia local players na makocha Wazawa Ila hawafiki kokote
 
Kingine inabidi wasajili wachezaji wa ushindani katika ligi kuu!

Niliwafuatilia DTB wakiwa ligi daraja la kwanza, walikuwa wanacheza kawaida sana.

Sasa, jitahidini msajili ili mpate ushindi wa uhakika, mana ligi kuu siyo daraja la kwanza ambapo huko unamnunua tu mwamuzi na unashinda. Simaanishi mlinunua mechi, la hasha, ila tulipokuwa tunaenda uwanjani kutazama mechi, figisu figisu zilikuwa nyingi sana, mf, magoli ya offside!

Na kukuta Madelu ni mbabe na mzee wa fitina, waamuzi wanaweza kumuogopa na kuipa ushindi Singida FC, hali ambayo itachafua NBCPL, kwani mechi zinarushwa na Azam TV, tofauti na ligi daraja la kwanza.

Ushauri wangu kwenu umeishia hapa kwa mwezi huu, tukutane ligi ikianza
 
Jina Baya, kosa la kwanza Hilo mmeshaanza ligi na Boko na mmeshapoteza points hapo.


Mkiwa affiliated na CCM tayari mmeshapoteza points zingine 10.


Msimu ujao mnashuka Daraja. Mark this
 
Mbona Zanzibar team zao wanatumia local players na makocha Wazawa Ila hawafiki kokote
Hawafiki kokote wakati wametupea wakina fei toto bwana. Level ya investment pia zinatofautiana. Kufika mbali pia has to do with money.

Hawa simba wameweza fika mpaka robo final caf champions league ni kwasababu ya investment. Na wao pia ili waweze kufika final itabidi wawekeze zaidi
 
Back
Top Bottom