Asante sana kwa taarifa hii muhimu sana kwa mustakabali wa uchaguzi mkuu wa 2025.
Kwa ruhusa yako naomba kutumia bandiko lako hili kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
Nawashauri Chadema wapunguze Populism Politics ya siasa za matukio, na badala yake wafanye Strategic Politics kwa kufanya siasa za strategia zenye SMART objectives.
Kwa vile the political game inachezwa kwenye the balot box, wakati huu wa kuboresha daktari Chadema wafanye mikutano ya hadhara kuwahamasisha watu wajiandikishe kwa wingi, huu ndio muda wa chopa ya Chadema kupasua anga. Uchaguzi is the game of numbers and numbers don't lie.
Niliwahi kulishauri hili huko nyuma
Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... humo nilishauri vitu vingi na leo tena ninashauri vitu vingi
1. Wapinzani msiwe ni watu wa kulalamika na kulaumu tuu kuhusu CCM kila wakati, bali sasa wajikite kueleza where CCM does wrong, lakini mkiingia nyinyi mtafanya nini tofauti na CCM, kwa kuangazia kero za wananchi na kuwaeleza ukichagua upinzani kitabadilisha nini, ili wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu, wapate sababu za msingi za kutoichagua CCM na kuwachagua wapinzani. Yaani Wapinzani wawape Watanzania, give reasons za not vote CCM kwa kuainisha maeneo ambayo CCM imeshindwa, ili kuwapa wananchi reasons za kuichagua Chadema na sio kuibadili tuu badala ya kuichagua CCM waichague Chadema for what?.
2. Mara baada ya uchaguzi wa 2010 na mafanikio makubwa upande wa Chadema, kwenye ile mada yangu ya
CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! niliwaeleza Chadema kuwa wao na wapinzani wengine wote bado wako kiuana harakati zaidi, yaani vyama vya kiuana harakati, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala tayari kwa kushika dola, lakini kuna wakati Chadema kupitia M4C, Chadema wanaonyesha dalili za kujipanga japo bado wanakabiliwa na madhaifu haya na yale, yakiwemo, lile koti la ukanda, udini, ukabila na ubinafsi wa "umimi" etc na baada ya kipigo cha 2020 sasa Chadema kimerejea kuwa ni chama cha kiharakati kikijikita kwenye siasa za matukio na mikutano ya hadhara na maandamano yasiyo na strategical with no SMART objectives.
3. Kwa leo naomba nisiingie tena kwenye udini, ukanda na ukabila wa Chadema, bali naomba nijikite kwenye ubinafsi au "umimi" kwa Chadema kujiamini kupita kiasi kuwa peke yao wataweza!, nilisema peke yao hawawezi, na leo nasema tena na tena, "Chadema peke yenu hamuwezi Kuiondoa CCM Madarakani" kwa sababu hili CCM ni dubwasha au dubwana kubwa sana kama mti wa mbuyu, ambalo haliwezi kung'oka bila umoja ambao ni nguvu ya Watanzania wote wenye kulitakia mema taifa hili, wakiwemo wana CCM Wazalendo ambao ni CCM contemporary!, wanaopenda kuiona CCM ikiwa checked na wapinzani wachache makini na sio kubaki CCM pekee.
4. Chadema na wapinzani wengine wote wa ukweli, ni lazima wa join forces kutafuta the common working grounds na wenzenu wengine wote mu work together towards a common enemy hata na nyinyi wenyewe kwa wenyewe lazima mkubali kushirikiana kwa kukubali kutokubaliana kwa hayo madogo madogo lakini lazima mkubaliane kwenye kubwa la msingi kwa kukubali "umoja ni nguvu" vinginevyo matokeo ya 2025 yatakuwa ni yale yale ya, vyama vile vile, na watu wale wale!.
5. Mfano, japo ACT ni mke wa CCM kwa upande wa Zanzibar, hiyo ni "marriage of convinience", hivyo inavunjika wakati wowote "conveniences" zikimalizika, hivyo Chadema inacho kibarua kigumu cha kum..ngoza huyu mke wa mtu kwa kumhakikishia akikubali kutoka nje ya ndoa, yeye 2025 hatakuwa mke tena, bali atageuka mume kule Zanzibar, ACT ndiye kidume cha Zanzibar 2025 na kumuoa huyo mume aliyenae sasa 2025 ategeuzwa mke!, kufuatia ukweli wa siasa za Zanzibar.
Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
6. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya ACT kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia njia nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2025, ni lazima ikubali kuisupport ya ACT kwa upande Zanzibar ili CUF nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na ACT waainishe maeneo ya strong holds za kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2025, kuepuka kumfaidisha kunguru kwa vita vya panzi!.
7. Voting statistics Tanzania: 2010 Presidential election results Updated January 2010 Registered Voters 20 137 303
Total votes 8 626 283
% Turnout 42.84
Valid votes 8 398 394
Spoilt votes 227 889
% Spoilt votes 2.64 Kwa mujibu wa data hizo, JK amechaguliwa kura milioni 5 tuu kati ya watu milioni 40!. Waliojiandikisha ni milioni 20, lakini waliopiga kura ni milioni 8 tuu!, hii inamaanisha kuna watu milioni 12, ambao walijiandikisha lakini hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwemo wale waliokata tamaa na kuona kupiga kura ni wastage of time, hata upige vipi kura, matokeo ni yale yale lazima CCM ishinde, hivyo kuliko kupoteza muda wakaachana kabisa na kupiga kura!. Chadema na wapinzani wasishughulike na wasihangaike na zile kura milioni 5 za CCM, bali wazitafute zile kura milioni 12 ambazo hazikupigwa.
8. Suppose 2025, Watanzania tutakuwa Milioni 66 wenye sifa za kupiga kura ni milioni 33, hawa wote wakihamasishwa kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura, mgombea wa CCM atajipatia kura zao zile milioni 10 za wanachama wao kwa mujibu wa tovuti ya CCM, halafu hizo kura milioni 23 zimuangukie mgombea wa upinzani, hata INEC ya CCM, wachakachue vipi, there will be no way out!, hivyo adui yetu mkubwa sio CCM, bali ni Watanzania wanaipigia kura CCM! na Watanzania wengi zaidi ambao hawajiandikishi na hata wakijiandikisha hawajitokezi kupiga kura!. The magic ni uhamasishaji na reaching out kuwafikia!.
9. Sasa ili kuwafikia Watanzania wote -haswa hawa grassroots level na kuwaamsha waliolala, Chadema haiwezi kuwafikia Watanzania wote kwa kutegemea maandamano na mikutano ya hadhara na mass media za wengine. Chadema lazima wawe na mass media yake ambayo ita propagate the message of "changing the mindset" ya Watanzania. Chadema wana all the resource kumiliki media yake lakini very unfortunately they are myopic, hawana vision ya kuona mbali kuangalia nje ya box and see a bigger picture. Hawajui kupanga priorities zao. Bei ya gari moja tuu la M4C linatosha kununua transmitter ya Digital ya redio na TV and convert chumba kimoja pale Mikocheni into an ultra modern digital studio!, kununua IP cameras za live stream na kuwa na YouTube Channel yake ya live stream na active interactive social media pages, Chadema bila media yake, ni kutwanga maji kwenye kinu! CCM ina media yake na TV yake ile ya TBCCM na TV za machawa wake, radio zake na magazeti yake, na machawa wake, na mitandao ya kijamii na kundi kubwa la ma socialites wa kutosha tukiwemo akina sisi na hii jf yetu!, kila alipo Maza, jf tupo!. Chadema bila media yake, ikulu wataendelea kuisikia tuu kwenye bomba, 2025 ni CCM tena, ni mitano tena kwa Mama, kama sauti hii ilikuwa ni sauti ya yeye na sio YEYE!.
10. NB. Declaration of Internet
Paskali ni mwanachama, mfuasi na mshabiki wa chama fulani cha siasa, and in fact ni kada!. Lakini ni kada Mzalendo contemporary mwenye kutanguliza mbele utaifa na maslahi ya taifa ndio maana licha ya kuwa kada wa chama kingine bado anawashauri vyama vingine the right thing to do.
Kuna wana CCM wengi wa type yangu ambao kwetu ni maslahi ya taifa mbele ndipo chama kinafuatia.
Paskali.