Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu ambaye yuko Mkoani Singida kwa ajili ya Mikutano ya Kijiji kwa Kijiji, ametangaza hadharani kwamba, kuna watu wanaomfuatilia kila anapofanya mikutano yake ya hadhara na kwamba watu hao Hawajulikani kuwa miongoni mwa wanavijiji hivyo na kwamba, watu hao wakifika eneo la Mkutano hujificha ili wasionekane kirahisi.
Lissu amesema kwamba ni vema watu hao wakajitambulisha kama ni Polisi na waseme wametumwa na nani, kufanya nini ili iweje, Vinginevyo atawalipua kwa wananchi ambao wataamua cha kuwafanya.
Zaidi soma hapa
---
"Toka nimeanza ziara yangu kuna gari inatufatilia halafu wakifika kwenye mkutano wanajificha, nyinyi mnajua mimi nimeshambuliwa sasa nikiona hali kama hiyo ninaogopa, nataka niseme kama ni Askari mje mniambie ili niwe na amani msiposema kesho kwenye mkutano wangu nitawanyooshea kidole maana vijana wangu wameshawatambua" Tundu Lissu, akiwa kwenye mkutano katika kata ya Matumbo Jimbo la Singida Kaskazini. Leo Juni 5, 2024.
======
Pia soma:
- Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali