Analog
JF-Expert Member
- Apr 4, 2024
- 323
- 618
Watu tisa(9) wafariki papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baadhi yao baada ya basi kampuni ya Lujiga walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kugonga Loli kwa nyuma lililokuwa limeegesha barabarani kwa kuharibika.
Ajali hiyo imetokea wilayani Iramba leo alfajiri 10:30 kijiji cha malendi kata ya mgongo.
========
UPDATE 1:
06:35pm
IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Lujiga Express lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Daniel Paul amesema kati ya majeruhi hao, watatu ambao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye amefanyiwa operesheni na mtoto kukutwa amefariki tumboni.
Nipashe