TANZIA Singida: Watu tisa(9) wafariki, basi likigonga Lori

Watu tisa(9) wafariki papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baadhi yao baada ya basi kampuni ya Lujiga walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kugonga Loli kwa nyuma lililokuwa limeegesha barabarani kwa kuharibika.

Ajali hiyo imetokea wilayani Iramba leo alfajiri 10:30 kijiji cha malendi kata ya mgongo.

========
UPDATE 1:

06:35pm

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Lujiga Express lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Daniel Paul amesema kati ya majeruhi hao, watatu ambao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye amefanyiwa operesheni na mtoto kukutwa amefariki tumboni.

Nipashe
Mganga mkuu wapi wakati ni muuguzi tu huyo
 
Bado nasema safari za usiku ni risk kubwa mtu unatembea 160 na wakati mbele vision imepungua kwanini usivamie vicheche, hatuja sahau bado tu yule dereva wa basi alie igonga locomotive mpaka ikatoka kwenye reli leo tena mtu kavamia roli na kwa speed aliyo ingia nayo kwenye roli karibia nusu nzima ya basi ilitaka ijae kwenye trailer ya roli.
 
Moja ya ajali mbaya sana ukitazama picha za tukio
 
Ukiachana na makosa ya kibinadamu, hili eneo la Malendi hadi Shelui kuna kitu cha kiroho kinazunguka.

Ni kama kipande cha Ikungi hadi Manyoni.

Msamvu hadi Nanenane Morogoro etc.

Ujumbe;
Tuziombeeni sana safari zetu kwa Mungu.
Mwanangu nipo hapa Cate hotel ndo nataka kurudi town. Nakiwaza sana hichi kipande cha nane nane mpaka Msamvu!! Na hizi pombe za Eid!!! Pale kama kuna Izraeli mtoa roho!!!
 
Ajali zinatokea kwa sababu ya weakness za watu ikiwemo uendeshaji usiozingatia sheria, gari mbovu, miundombinu mibovu n. k. Hakuna kitu kinachoitwa mungu na hakijawahi kuwepo.
Ni mtazamo wako.
 
Watu tisa(9) wafariki papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baadhi yao baada ya basi kampuni ya Lujiga walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kugonga Loli kwa nyuma lililokuwa limeegesha barabarani kwa kuharibika.

Ajali hiyo imetokea wilayani Iramba leo alfajiri 10:30 kijiji cha malendi kata ya mgongo.

========
UPDATE 1:

06:35pm

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Lujiga Express lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Daniel Paul amesema kati ya majeruhi hao, watatu ambao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye amefanyiwa operesheni na mtoto kukutwa amefariki tumboni.

Nipashe
Safari za usiku bado sio salama sana
 
Muhimu gari ikiharibika barabarani alama ziwekwe mara moja ili watumiaji wengine waone. Hata kama speed ni 80 kishindo chake cha kugonga lazima kitaleta madhara tu.
Mimi kwa uzoefu wangu wa kusafiri na mabasi, sidhani kama yanaspidi kali sana kushinda magari ya serikali au magari ya watu binafsi. Mara nyingi naona yanatupita
RIP
 
Hapo unaweza Kuta Lori tahadhali yake ni majani ya miti ndio reflector yake. Usiku huu unakuwa mtego wa panya. Watu wapewe tenda ya road rescue Kwa vipande yaani wawe kama fisinwa dar dakika tu gari imekwama wanakuja kukutoa Kwa nguvu.
 
Mwanangu nipo hapa Cate hotel ndo nataka kurudi town. Nakiwaza sana hichi kipande cha nane nane mpaka Msamvu!! Na hizi pombe za Eid!!! Pale kama kuna Izraeli mtoa roho!!!
Hapo nyumban kabisa yan kila baada yasiku kadhaa lazima kipande cha cate hotel to kingolwira damu imwagike
 
Upo sahihi lakini pia Kuna tatizo la Tanroad na barabara zao ambazo hazina fail safe area, sehemu kama iyovi na msimba mikumi ikitokea gari limepata breakdown kwenye zile kona ni ngumu sana kuzuia ajali isitokee.
Samahani mkuu, hii inakuaje? Nimejaribu ku google lakini sijapata maelezo mazuri..
 
Watu tisa(9) wafariki papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baadhi yao baada ya basi kampuni ya Lujiga walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kugonga Loli kwa nyuma lililokuwa limeegesha barabarani kwa kuharibika.

Ajali hiyo imetokea wilayani Iramba leo alfajiri 10:30 kijiji cha malendi kata ya mgongo.

========
UPDATE 1:

06:35pm

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Lujiga Express lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Daniel Paul amesema kati ya majeruhi hao, watatu ambao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye amefanyiwa operesheni na mtoto kukutwa amefariki tumboni.

Nipashe
Dah wapumzike kwa amani ndugu zetu
 
Back
Top Bottom