TANZIA Singida: Watu tisa(9) wafariki, basi likigonga Lori

TANZIA Singida: Watu tisa(9) wafariki, basi likigonga Lori

Upo sahihi lakini pia Kuna tatizo la Tanroad na barabara zao ambazo hazina fail safe area, sehemu kama iyovi na msimba mikumi ikitokea gari limepata breakdown kwenye zile kona ni ngumu sana kuzuia ajali isitokee.
Bila Tanroads kufanya hivi kwenye barabara za kuunganisha mikoa mtaendela kufa hadi mkome.
images (9).jpeg
 
Watu tisa(9) wafariki papohapo na wengine 19 kujeruhiwa vibaya baadhi yao baada ya basi kampuni ya Lujiga walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kugonga Loli kwa nyuma lililokuwa limeegesha barabarani kwa kuharibika.

Ajali hiyo imetokea wilayani Iramba leo alfajiri 10:30 kijiji cha malendi kata ya mgongo.

========
UPDATE 1:

06:35pm

IDADI ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Lujiga Express lenye namba za usajili T 315 CXX iliyotokea wilayani Iramba mkoani Singida imefikia 9 na majeruhi 19.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Daniel Paul amesema kati ya majeruhi hao, watatu ambao walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba (Kiomboi) alikuwepo mwanamke mjamzito ambaye amefanyiwa operesheni na mtoto kukutwa amefariki tumboni.

Nipashe
Mwenyezi Mungu awafariji wategemezi na ndugu za marehemu
 
Taarifa haijakamilika rasmi, kama kuna yeyote atakaye pata updates zaidi, basi unaweza kutuletea taarifa iliyokamilika 🤝.

• MwenyeziMungu awaweke mahali pewa wale wote waliofikwa na umauti kwenye hiyo Ajali.

• MwenyeziMungu azidi kuwapa ustahimilivu kwa wale wote waliopata majerahaa sehemu mbali mbali za mwili.
---
Habari zilizotufikia hii leo Aprili 10, 2024 zinaeleza kwamba ajali mbaya imetokea wilayani Igunga Mkoa wa Tabora ambapo vifo vinasadikiwa kuwa ni vingi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imehusisha basi la Kampuni ya Lujiga Express ambalo limegonga lori kwa nyumba na kusagika vibaya.

Mashuhuda wanasema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni basi lililokuwa kwenye mwendo mkali kiasi cha kuingia nyuma ya tela la lori.

Bado Polisi hawajatoa taarifa kamili, lakini wapo eneo la tukio.​

 
Back
Top Bottom