Single Moms njooni tuelimishane kitu hapa

Single Moms njooni tuelimishane kitu hapa

Sitokuwa na uwezo wa kukitawala kizazi changu hasa Cha pili na Cha tatu.

Ila nature itafanya kazi yake kwa asiye jitambua na kujua nini afanye kwa muda gani?

Kifupi nitawaambia maisha ni mchezo ila ukicheza vibaya lazima ulie.

Maisha ni kioo, ukicheka na yenyewe yatakuchekea na ukinuna hutokuwa na furaha nayo.

Maisha ni mipango ila usipopanga basi utapangiwa

Maisha ni ndoto, usipofuata ya kwako basi utafuata ya mtu mwingine

La mwisho nitawaambia Kuna makosa ya aina tatu

1. Ya asili
Usipoheshimu wazee na tamaduni ulizofundishwa na ukoo wako, mababu utampata matatizo.

Na usipoheshimu muda na kuwa na haraka utaangukia pua.

2.Maumbile
Maumbile yako yana thamani kubwa ila kila sehemu kwenye mwili Ina muda wa matumizi yake ila ukitaka kuharakisha jiandae au ukitumia tofauti.

3.Mungu
Ukimkufuru subiri yatakayo kupata.

Sorry kama nimekukwaza
Amina
 
Hongera sana kwa kuzaa, lakini hongera nyingi kwa kulea , uzazi na malezi sio kazi nyepesi au inayoweza kuirahisisha, mengine vyote ni sehemu ya maisha , maisha hayana njia nyoofu ya moja kwa moja.
Kabisa,,milima na mabonde mkuu🙏🙏🙏
 
Mwenzenu huu usinglemom ulinikuta chap Kwa haraka...Yaan bila kutarajia...mtu niliyemwamini na niliyekuwa na malengo nae alinigeuka....nikisema iliingia Kwa bahati mbaya nitakuwa nadanganya...tulipanga Nami nilijiaminisha Kwa sababu Kuna hatua tulipitia ambazo nikajua yessss,nimelipata bwana!

We bwana wee...kumbe nimepatikana ...Yaan Ile kitu kutiki tu jamaa akasema "katoe mimba".....nyie wadada wenzangu mnaotupondea singlemoms...siyo Kwamba sikuweza kumeza P2 au miso-p au kwenda hospital kukwanguliwa...noo,ningeweza ila tu huyu kiumbe hakuwa na hatia.So mwishowe nikazaa huyu son wangu...jamaa alichoniambia ni kuwa...umezaa basi umejipanga kulea I mean hajawahi toa hata Senti kulea mwanangu then Leo hii anajitutumua eti anataka mwanaye.Teh!

Sasa point yangu ni ipi ya kuwakusanya wamama wenzangu...ni hivi...hatujaua,tumezaa,tunalea....na huenda tukawa tumebahatika kupata wanaume wema wanaotupenda siye na wanetu...sasa ninachokuuliza ..hivi wenzangu mnawezaje kuendelea kuwasiliana na mwanaume aliyeshindwa kukupa thamani ya kuweka ndani na akakuacha na mtoto....mnawezaje kuvua nguo tena Kwa mwanaume ambaye si mumeo Yaan Ex tena aliyekudharaulisha? Aisee,mwenzenu nimeshindwa....nilimwambia nitakuwahisha kunizoea😖🤨

NB:sijawahi mjaza sumu mwanangu...hicho ndicho nilichoshinda....namwacha akue yeye ndo atachambua magugu na ngano.Hongereni Kwa kupambana wanawake wenzangu kulea ni Kaz kweli.Nawapenda sana😍😘
Ila naomba tu hii thread ikifika mwisho unishtue niseme jambo kwaajili ya singo mama wote.
Maelezo yako ndio hali halisi waliyokutana nayo single mother wote hivyo haipaswi wanawake waliozalishwa kabla ya ndoa wanyanyapaliwe au kubaguliwa.

Comment yangu ya page ya kwanza ilikuwa utani tu kabla sijasoma habari yako. Naomba unisamehe tafadhali.
 
Ila naomba tu hii thread ikifika mwisho unishtue niseme jambo kwaajili ya singo mama wote.
Maelezo yako ndio hali halisi waliyokutana nayo single mother wote hivyo haipaswi wanawake waliozalishwa kabla ya ndoa wanyanyapaliwe au kubaguliwa.

Comment yangu ya page ya kwanza ilikuwa utani tu kabla sijasoma habari yako. Naomba unisamehe tafadhali.
No,easy mkuu!
 
.....hivi wenzangu mnawezaje kuendelea kuwasiliana na mwanaume aliyeshindwa kukupa thamani ya kuweka ndani na akakuacha na mtoto....
Mnawezaje kuvua nguo tena Kwa mwanaume ambaye si mumeo Yaan Ex tena aliyekudharaulisha?....


Hivi haya maswali wahusika wamejibu Kweli?
 
Back
Top Bottom