Single Mother ananiwekea Vikwazo kuonana na mtoto wangu

Single Mother ananiwekea Vikwazo kuonana na mtoto wangu

Kama ataendelea na huo ujinga nitamnyanganya huyo mtoto kwa nguvu na hamna kitu atafanya
Huwezi! System inawalinda Singo maza ujue. Hata ukienda Kisutu, mahakama ya watoto, hutapata haki yoyote. Yalitupata nasi ila kwa sasa tunawatambia maana watoto hao wapo vyuo vikuu ambapo Ada na gharama zote si chini ya 10M. Hapo heshima imerudi, lakini tumeonja joto la jiwe wakiwa msingi na sekondari ujue
 
Mwanamke hawezi kukufanyia hivi kama kweli wewe ni baba wa mtoto, pengine ulizingua kwenye mimba au ulimkana, leo mtoto kafikisha miaka minne unajifanya kumjua jua mtoto, upendo unajengwa toka mwanzo inawezekana kuna baba wa mtoto halali au wewe ni halali lakini ulikuwa falla kwenye matunzo ya mtoto,mama mtoto hataki mazoea na wewe inawezekana hata mtoto kahamishwa shule na ukizingua zaidi hutomwona huyo mtoto, kumbuka mama ndiye ajuaye baba halisi wa mtoto, kaa pembeni fanya maisha yako mengine kama unampenda baby mama mwelekeze muishi pamoja.
Acha akili ya Kitombile, hakuna sheria inayolazimisha upendo. Sasa hivi ni mtoto tu ndo bottom line
 
Peleka kesi ustawi wajamii haruhusiwi kufanya chochote bila kukushirikisha , ukiona wanazingua peleka kesi mahakama ya watoto wilaya
 
Back
Top Bottom