Single mother bana, tabu tupu

Single mother bana, tabu tupu

Achana na akili za kivulana, single mother ni akili kubwa

Kama we huwezi muoa single mother wapo wanaweza kuwaoa tulia

""Kweli alisafiri. Picha likaanza kwenye status. Mara ampost mzazi mwenzie na caption like "asante baba kwa kunitunzia mwanangu" yaani ni post za mzaz mwenzie like bado wana uhusiano.""

#YNWA
 
Ila status bana Kuna watu ukiona tu unajua maisha yake yalivo ila Kuna wengine utasugua bench kumjua kwa kutumia status
Kuna jamaa mmoja nilipewa number yake akawa ananitumia mizigo mwaka 2016 mpaka leo hii sijawai kuona sura yake status na always huwa anaweka status mbili huwa anapost kiatu alichovaa na ya pili anaweka pic ya kiongozi yoyote

Pia mara moja moja huwa anapost pic ya mkono wa mwanamke (nadhani ndio demu wake)


Alafu Nina rafiki yangu mmoja muhaya sidhani kama Facebook kuna mtu hajui kuwa ni mechanical engineer Tanapa mwamba lzm always apost pic yake akiwa job na caption pendwa "MNIOMBEE"
 
Samaleko...

Hiki nacho ni moja ya visa vyangu kwenye harakati zangu za kumpata mtoto wa mama mkwe.

Kuna ka binti nilikutana nako miezi kama mitatu iliyopita. Siku ya kwanza tu nakaona nilipokasalimia tu, kalinichangamkia sana. Kakaniambia "ni kama nakuonaga maeneo flan" na ni kweli ndio maeneo niyoushi. Nikamjibu itakua kweli maana naishi maeneo hayo. Kwenye stori stori kumbe hakai mbali na ninapoishi. Basi tukabadilishana namba kila mtu kwao.

Nikatulia kama wiki kadhaa nikamche, just kumpa salam. Nikamuuliza upo wap? Akanijibu, kumbe anapofanya kazi nami huwa napita kila siku nikitoka kwenye mishe zangu jion. Basi nikamwambia naomba nisubiri nitakupitia hapo, akaubali.

Basi nimefunga zangu mida ya saa3 usiku nikamuuliza umemaliza kazi akajibu ndio, nikamwambia nakupitia, akajibu sawa. Kweli nikampita, nikampitisha mahala kupata dinner then kila mtu kwao. Siku ikaisha.

Sasa kipindi hichi sasa nikaanza kukathaminisha kama kanaweza nifaa kwenye nia yangu. Kimuonekano kakawa kanaingia, kanatoka. Nikajiambia anyway, ngoja nitupe ndoano huwezi jua pengine roho yake na treatment zake zinaweza nifanya nizame mazima. Wakati huu bado sijui kama ni ka single mother maana kalikua hakana muonekano wa kamba kalisha zaa na hakana smartphone, so sikua hata naona status zake whatsapp. Maana njia nyingine ya mkujua mtu ni kupia status anazopost.

Basi nikaanza kukasaundisha. Kakaanza kuingia lain. Jinsi nilivyokua romantic hadi kuna siku kakaniambia "yaani wanaume wengine jaman, unaweza hata wabebea mimba". Mimi bichwa hilo.

Basi life likaendelea, muda huu wote sijui kama ni ka single mother. Siku moja, nikasema leo nataka nijiridhishe na maisha yake. Nikamwambia atafute siku atakua na muda nimtoe dinner. Kweli akaniambia siku flan. Siku ikafika tukatoka. Basi ni msosi na soft drinks tu (situmii alcohol).

Kwenye mastori nikamtega akajaa. Akaanza kufunguka kuwa yy anamtoto wa kike alizaa na jamaa wa bukoba. Mtoto anaishi na baba yake bukoba. Nikamtega zaidi akaendelea kufunguka. Akasema, kuwa anampigia sim mzazi mwenzie anampa sim mtoto anaongea nae. Nikajiambia, hawa bado wana bondi inayoishi kabisa. Kwa kifupi nika conclude kwamba siku hio iwe mwisho wa kumfuatilia. Basi baada ya muda nikarudisha kwao maana anakaa na mama yake.

Sasa wiki mbili zilizopita nilimuona maeneo flan mida ya saa3 asubuhi ila yy hakuniona. Ilipofika saa5 nikamtext, nimekuona maeneo flan sijui ulikua wewe. Akasema ndio ni mm. Nikamuuliza hujaenda kazini? Akajibu sijaenda, ninasafari ya bukoba leo naondoka na magari ya saa7 yanayotoka dar. Nikamwambia safari njema. In short nilihisi kabisa anenda kwa mzaz mwenzie. Sasa kipindi hichi kesha nunua smartphone.

Kweli alisafiki. Picha likaanza kwenye status. Mara ampost mzazi mwenzie na caption like "asante baba kwa kunitunzia mwanangu" yaani ni post za mzaz mwenzie like bado wana uhusiano. Muda huu mm nilishasitisha zoezi, so nothing to complain.

Ninachota kuwaambia, kuoa single mother ni kujitafutia stress tu. Hawaachanagi hawa. Kama uko fresh tafuta fresh mwenzio muanze kwa score ya 0-0. Vinginevyo jiandae kuja kutuomba ushauri hapa.

Hapana wapo watu wengi sana ambao wanajielewa wakiachana na Baba za watoto wao inakua for good na yanabaki malezi tu.
Kuna kuachana alafu kuna kutokua maadui.
Maisha mengine yanaweza kuendelea ikiwemo hata kupostiana.
Sometimes be happy hakua muongo na hakukudanganya.
Hapo wewe unamuita single mother na hapo ulikua unataka mtumia tu aisee[emoji1418]
Na ingekua unatafuta ndoa ingekuaje?
 
Wapo tofauti sana na sisi ni ngumu sana kujua maisha ya mwanaume kupitia account yake ya mtandaoni ila wanawake asilimia kubwa utajua Leo Yuko depressed Leo anahiki
Akiumwa anatupia ki emoji cha dawa, akisafiri anaweka kigari
 
Wewe ndio una matendo maovu umeingia kusiko kuhusu,,sasa mtu asimposti mwanae??na ulitaka asimpongeze mzazi mwenzie kwa kumtunza mtoto vizuri,,,simu ni yake,,bando la kwake,,, mtoto ni wake,,,mwanaume ni wake!!huwezi ukachukia na kumpangia kama wewe unavyotaka tafuta wako na wewe umzalishe na sio kurukiarukia vya watu,,,alafu alishakueleza kila kitu kabla,,wewe ndio ulishindwa kujiongeza??acha kupenda vitonga ndio matatizo yake hayo
Jamaa anazingua ukioaa single maza au ukidate nae kubali ukweli jamaa aliemzalishaa ana nafasi kubwa kwenye maisha yake kuliko wewe labda awe KAPUKUUU MNOOO.. otherwise utamu atakula akitaka.
 
Huyo fresh nae ana ex/ma-ex wake pia sasa sijui unakwepa nn hapo.
 
Labda kuna kitu watu hawaelewi.
Sio kila mwanamke ambaye ana mtoto na haishi na baba wa mtoto au hajaolewa basi ni single mother.

Wengine hawaishi pamoja tu lakini ni wapenzi na wana mipango yao mingi ya kutimiza. Ni wakati tu haujafika.

Juzi jumamosi nilienda kwenye harusi ambayo maharusi walikuwa na watoto watatu na walikuwa hawaishi pamoja.

Kwahiyo huyo binti pengine yeye na baba mtoto wana mahusiano na hawajaachana.
 
Back
Top Bottom