Single mother tumeanza kushindwana na kutishiana maisha kisa mwanaye

Inahitaji uwe na akili kama ya jamaa. Kulea ubovu ni kulea magonjwa
Hiyo akili inahitajika pale usipohitaji kumlea huyo mtoto, ila kama una nia ya kumlea huwezi tumia njia ya kufukuza. Unadhani angekuwa wake wa kumzaa angefukuza? Angepambana ahakikishe dogo ananyooka.

Wanawake wanahitahi miongozo ya mwanaume katika malezi, ni suala la kumfanya aelewe na kukusikiliza kuwa nia ni kumlea mtoto wenu katika njia sahihi. Ukimfukuza maana yake humtaki tena.
 
busara gan itafanya kaz kama mama yakr anakingia kifua mapunguf ya mwanamke?

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Wanawake siku zote wana mapungufu ndo maana mwanaume anahitajika. Busara ambayo angeitumia iwapo huyo mtoto angekuwa wa kwake wa kumzaa ndo ilipaswa kutumika, sasa huwezi kuwa nayo mpaka uwe na nia ya dhati ya kubeba jukumu la malezi.

Jamaa yupo sahihi iwapo hakuwa tayari, kujilazimisha angeteseka sana.
 
Angekuwa wake wangemlea tangia mwanzo, sio huyo kaja na makuzi yake na mama anasimamia hivyo, kama nikweli anaongea hapa sio kwenu au Baba yako angekuwa hai angekununulia hayo ni maneno gani sasa, huyo akakae kwao amlee mtoto wake mpaka awe mtu mzima, hao ndiyo wale mwanaye akioa anataka kumsimamia kijana hata kama anamke akwende tu kwao na mwanaye.
 
Umesema vyema mkuu

Maisha ya ndoa ni zaidi ya sura nzuri, rangi nzuri na minyanduano

Alijichanganya sana mwanetu
 
Yaan awe na nia ya kulea mtoto asie wake? Yaani alianzisha mahusiano lengo likiwa kumlelea mtoto?
 
Wewe jamaa upo sahihi kabisa kabisa,
 
Sasa baba Ikram unaenda kumchukua lini mtoto wako , Yaan unalikuta litoto halina adabu halafu sio la kwako patamu hapo!!!!!
Ukilitia mikwenzi Mama mtoto anakuja juu kumtaja Mwanaume mwingine, shamba lenye mgogoro pasua kichwa
 
Sikiliza mkuu kulea mtoto asiye wako ni ngimu hata kama una hio nia itaisha hasa kwa mzazi mpuuzi kama huyo maza. Mtoto wako ikimzaba kofi mama yake hawezi kukujia juu, hata akiwaka ni kawaida tu, ila wa kufikia ukimzaba kofi utaona rangi ya mama yake na huwa wanakimbilia kusema humpendi mtoto wake, kama mtoa mada alivyosema, hapo utaendelea kumnyoosha au utakua unachekacjeka tu kama fala hata kama dogo kakosea na wewe unaungana na mama yake kujichekesha chekesha?

Kulea mtoto asiye wako ilikua zamani sio sasa. Zamani ukizingua unagongwa na mzee wa kitaa tu na anakushika mkono kukupeleka home huku unambembeleza asikupeleke home manaa ukifikishwa ni kipondo tena. Sasa ivi mfinye mtoto wa mtu uone. Mtoto ukimkalipia tu mzazi anakujia juu. Yaani siku hizi watu wanahisi kuzaa wameanza wao. Ni mfumo wa maisha umebadirika sana, huwezi lea mtoto wa mtu kwa malezi ya kumnyoosha utaqmbiwa humpendi
 
Sasa ivi mfinye mtoto wa mtu uone. Mtoto ukimkalipia tu mzazi anakujia juu. Yaani siku hizi watu wanahisi kuzaa wameanza wao. Ni mfumo wa maisha umebadirika sana, huwezi lea mtoto wa mtu kwa malezi ya kumnyoosha utaqmbiwa humpendi
Utaambiwa umemwingizia Chupa hawachelewi, kua makini single Mama asije akakubambika kesi ya kupaka na kutawiti mtoto wake chondechonde utaozea selo
 
Kuna jamaa yangu kampangia chumba&sebule singo mother wa watoto wawili (miaka 2&4), anasema kupata sex Ni mpaka ajipange Ela ya gesti wakati alikompagia pango kalipia miezi 6. Nae soon anakaribia kutema BUNGO[emoji23]
Na hapo kila mtoto ana Baba yake

Single Mama mtoto wake kwanza alafu wewe ndio unafuata yaan wewe umevamia mke wa mtu na baba wa mtoto bado anamuita mume wake hio ipo hivyo yule ni mume wake wa kwanza kabla yako hilo atakua anakwambia hata kimoyomoyo kwamba ulichelewa wapi Mwanaume mwenzio akakuwahi kumjaza kitumbo ulikua wapi ona sasa unalea kisichokuhusu mtoto sio wa kwako hata yeye sio wako maana bado yupo kwenye umiliki wa Mwanaume wake wa zamani indirectly maana ili uende nae Sawa cha kwanza umpende mtoto wake yaan umpende mumewe wa zamani maana huyo mtoto ni copy & paste ya Mwanaume wake aliemzalisha

Maana yeye anamuona mumewe aliemzalisha kupitia huyo mtoto hata km huyo Mwanaume hatoi matunzo yoyote kwa mtoto au amekataa mimba au amekueleza vyovyote iwavyo Ila kitendo cha kujazwa mimba na huyo Mwanaume kwake anachukulia ni Jambo lenye uzito mkubwa mno maana bila huyo Mwanaume kumtia mimba yeye asingeitwa Mama hata km alipitia magumu gani kwenye kushusha injini

Kwa hio single Mama akikwambia Baba wa mtoto sijui fyokofyokonyoko kanifanyia fyokonyoko we mwangalie tu Ila deep inside akijikusanya kwenye pembe 4 chumba hua anapiga goti chini na kumshukuru huyo Mwanaume kwa kumtia mimba na kumuombea Mazuri popote alipo na akisikia kapatwa na baya lolote anaumia ndani kwa ndani hata km amekufa anapiga goti kwa huzuni kuomba Baba mtoto alale salamu huko mavumbini

Maelezo haya nimeyafanyia research ya kina kwa kufanya sampling za kutosha na kutengeneza questionnaire za kutosha kwa single Mama watatu ambao wote wamezaa na wanaume tofauti yaan kila mmoja ana watoto ambao kila mtoto ana Baba yake mmoja

Jacklyn
Jesca
Joy

Kila mmoja ana watoto wawili na kila mmoja ana Baba yake na kila mtoto ana story yake tofauti jinsi alivyopatikana

X
 
Kwahiyo singo Maza wawili mmeshindwana

Rainbow nation Naona mmeamua kutoka makabatini
 
Wanawake wanaongeaga tu kwa mihemko. Huyo anarekebishika.

Unless angekuwa na tabia za kimalaya ila kama ni gubu, anarekebishika na hata huyo mtoto ananyooka na fimbo anakula za kutosha na mama yake ataelewa tu kuwa nia ni kulea vizuri.

We sema kwa mazingira ya jamaa ni ngumu sababu yeye mtoto hana, angekuwa nae na yupo hapo kungekuwa na urahisi.
 
Yaan awe na nia ya kulea mtoto asie wake? Yaani alianzisha mahusiano lengo likiwa kumlelea mtoto?
Kuwa na nia ya kulea mtoto asiye wako inawezekana mkuu na kuna watu wanalea watoto pasua kichwa na wanapambana nao na sio wa kwao. Ila si jambo la kuiga au kujilazimisha.
 
Sikiliza mkuu kulea mtoto asiye wako ni ngimu
Ni kweli, sijasema ni rahisi.
hata kama una hio nia itaisha hasa kwa mzazi mpuuzi kama huyo maza.
Wanawake wengi kwenye malezi hufanya upuuzi au makosa ndo maana ni vizuri watoto kupata malezi ya baba na mama.
Ndo maana nikasema busara inahitajika, fimbo anachapwa na mama yake ataelewa. Huyo mwanamke bado akili ndogo ana mihemko ni vile na jamaa bado kijana na huenda hana mtoto ambaye angekuwepo hapo huyo mwanamke angeona kuwa jamaa si mwonevu bali ni mlezi maana hata mwanae anamtandika akifanya ujinga.
Kulea mtoto asiye wako ilikua zamani sio sasa.
Kama zamani iliwezekana hata sasa inawezekana na kuna watu wanalea mkuu.
Zamani ukizingua unagongwa na mzee wa kitaa tu na anakushika mkono kukupeleka home huku unambembeleza asikupeleke home manaa ukifikishwa ni kipondo tena.
Ni kweli, jamii ilitulea.
Sasa ivi mfinye mtoto wa mtu uone. Mtoto ukimkalipia tu mzazi anakujia juu. Yaani siku hizi watu wanahisi kuzaa wameanza wao. Ni mfumo wa maisha umebadirika sana, huwezi lea mtoto wa mtu kwa malezi ya kumnyoosha utaqmbiwa humpendi
Inawezekana ila ni ngumu sana haswa kama wewe huna watoto wa kuonyesha kuwa ni tabia yako kulea watoto kwa mtindo huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…