Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Nimeelewa unaongelea wanawake wa aina gani kumbe cyo mke unaongea kuhusu slay queen πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Huyo mke firisika uone kama anakupenda wewe au huduma zitokanazo na hela yako
 
Huyo mke firisika uone kama anakupenda wewe au huduma zitokanazo na hela yako
πŸ€”πŸ€”πŸ€”Ila wewe unatongoza wanawake wa aina gani tajiri πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mara nyingine wanaume wanaokimbia watoto wanarudi kudai watoto kwa Sababu vifuatazo.

1. Huyo mtu kaingia kwenye Ndoa afu kashindwa kupata mtoto.

Sasa akikumbuka ameacha mtoto sehemu flani basi anarudi.

2. Huko kwenye ndoa yake kashidwa kupata mtoto wa kike pale akiona ana watoto wa kiume tupu au ana watoto wa kike tupu afu kaacha mtoto wa kiume sehemu huyo lazima atarudi tu.

3. Kaona Baby mama kaolewa sasa wivu umemkumba anarudi kwa sababu ya wivu tu.

4. Baby mama amefanikiwa na analea mtoto vizuri au kaolewa na mtoto analelewa vizuri na kusoma shule mzuri na kama akionekana anaakili sasa jamaa anaona mtoto anaweza kuwa na future mzuri baadae hicho kinamrudisha.

5. Mtoto kafanana na yeye kabisa kuliko mwanzo.

Huwa wanarudi kwa Sababu.
6. Baada ya kuhangaika mama mambo yamemunyokea na jamaa mambo yake hayayeleweki,anaamua kujilipua akahurumiwe. Hawa nao wapo
 
kwani kuwa single maza ni dhambi[emoji16][emoji16]yap Niko na vijana wangu wawili matata sana[emoji3059][emoji3059]ni washkaji zangu kinouma[emoji7]ukitukuta tumevaa sports wear unawezajua sio mama yao[emoji16][emoji16]ila wakizinguaga makonzi yanawahusugi [emoji1787][emoji1787]

Father of my boys tuko nae vizuri sana na huwa ninamuombea kila kukicha(sijui kama analijua hili)lakini nikiwa na ishu ya watoto basi mtu wa kwanza kuwasiliana nae ni mke wa baba watoto wangu then yeye ampatie taarifa mumewe ila ikitokea ishu ya kufanya maamuzi juu ya vijana wetu basi moja kwa moja nampigia baba mtu then nampigia mkewe kumpa taarifa kuwa niliongea na mumewe kuhusu watoto na tumefikia sehemu fulani inakuwa imeisha hiyo.[emoji7]

Ilinichukua miaka kama sio sita au saba kutengeneza huu upendo uliopo sasa lakini mwanzo tulikuwa maji na mafuta uadui ulitawala so ikabidi upande mmoja uteseke kwa faida ya watoto na huo upande ulikuwa ni mimi[emoji16][emoji16]

Kuwa single mama sio shida[emoji16]shida unakuja kuwa single mama halafu hujielewi[emoji4][emoji4]
Kuwa single maza ni dhambi na ni laana.
 
Yaani unawasiliana na baba mtoto bila kumshirikisha mumeo na unajua msimamo wake juu ya mawasiliano na baba mtoto apo ndio tatizo linapoanzia inaonekana dada bado alikua anampenda baba mtoto na sio mumewe iyo ni dharau mbaya na ndipo usingle mama unapoonekana jau
Labda tu alidhani ingekuwa rahisi kwa yeye binafsi kulitatua hilo suala kumbe ndio hivyo tena.
 
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa na mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa muda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lakini baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister.

Si unajua wanaume kwa kukimbia watoto wapo. Jamaa akawa hata huduma hatoi wala nini, ila mtoto anamtaka kumuona, kuna wakati alikuwa anajitokeza hata baada ya 3 month mara 1 tuu kumuona mtoto hatoi chochote. Baadae katokomea kabisa.

Sasa sister angu huyu akakutana na jamaa mwingine kipindi mtoto wake alikuwa na umri wa miaka 3 kwenda minne.

Jamaa hakuwa tayari kuwa nae si unajua single mother wanaume hatupendi sana, ila sister alijaribu kumshawishi mpaka kukubali. Na alimueleza kila kitu kuhusu Baba mtoto.

Jamaa akasema kwa vile Baba mtoto kasepa kapotea basi tutakuwa fresh, ila alitoa sharti hataki kuona Baba mtoto anajitokeza au mama anajipendekeza.

Wakafanikiwa kufunga ndoa.
Na kuchukua mtoto wakawa wanakaa nae dogo alipofikisha miaka 6 akampeleka shule nzuri ya 2 million per year akawa anasoma huko.

Sasa Baba mtoto aliposikia bibie kaolewa si akarudi bwana kuanza kutaka mtoto. Sister akagoma kabisa tena bila kumwambia mume wake. Na alirudi kipindi sister ana watoto wadogo mapacha aliyezaa na mume wake.

Waliangaishana kama mwaka 1 hivi. Sister alikataa kabisa kumpa dogo.

Sasa kipindi mtoto kafikisha miaka 8. Jamaa si akaenda ustawi wa jamii kwa lengo la kuchukua mtoto, sister kweli aliitwa ustawi wa jamaii na alienda tena bila kumwambia mume wake. Yeye alieleza kwao na kwao waligoma na kumwambia asiende. Ila ustawi wa jamii walilazimisha na kumwambia Mtoto ana haki ya kumjua Baba yake halisi. Hio ni haki ya mtoto.

Sasa mume wake baada ya kujua hilo akachachamaa kabisa ukawa ni ugomvi sana kati ya yeye na mke wake.

Mume wake akaamini kuwa Sister alimficha au niseme alimdanganya jamaa kakimbia kumbe laa. Waligombana sana.

Sasa jamaa akafanikiwa mpaka kubadilisha jina mtoto la mwisho maana sister aliandika jina la kwao la mwisho la mtoto.

Jamaa akaweka jina la kwao. Na jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa. Maana sehemu ya Baba ilikuwa empty nafikiri.

Mume wake baada ya kuona hivyo akamwambia kuwa kuhusu kitu chochote cha mtoto wake asimwambie mpk ada. Na mtoto aende kwa Baba yake pale home kwake amtaki tena.

Sister akaona kwa vile anataka kuokoa ndoa yake ampeleke mtoto kwa Baba yake. Sasa ishu kule kwa jamaa , dogo alikuwa anasoma shule ya over 2 million per year. Jamaa wa kawaida tuu.

Kwa kifupi dogo baada ya kwenda kwa Baba mawasiliano yakazidi kupelekea mpk mume wake kuanza kugombana. Sister akasema yule mwenzie anamsumbua sana na anamfanya mtoto kama kung'ang'ania kumuona mama yake, muda wote. So anajikuta muda mwingi anakuwa anawasiliana upande mwingine.

Baada ya kuona drama ni nyingi mume alimtimua sister home kwake. Na walisumbuana kama 2 years kutaka kuachana.

Mume wake ni mtu mwenye wivu. Walitaka kusuluhisha kwa kumuita jamaa yule msumbufu ila jamaa aligoma kuja na wala mume wake alikataa kusikiliza suluhisho. Wiki mbili zilizopita waliachana baada ya purukushani kwa miaka 2.

Alikuwa single mother na kuingia kwenye ndoa na mwishowe karudi tena single mother. Dogo anasoma shule za kawaida tuu hizi japo ni private pia kule kashatoka shule ya bei kubwa.

Hivi ishu kama hii mnaisolve kivipi jamani, IKIJA KWENYE FAMILIA, KARIBUNI.
Kuna viumbe very stabbon asikwambie mtu....

Kuoa single mother nikama kununua shamba lenye mgogoro....

Oa single mother ikiwa mumewe amefarik
 
Unaweza usitake mazoea ila huyo mtoto ndio anayeleta mazoea...
Ahhhhh wapi. Kama mtoto anakuwa busy na masomo yake,akirudi likizo jamaa anamjali kama mwanae,af ndo anamuita baba,unadhani ingekuwa rahisi kihivyo kwamba mtoto achangie mazoea? Mama mwenyewe keshaumizwa,mtoto akidai nimesikia hili na hili,si unamwambia baba yako ni huyu huyu!
Wengine tu hujisahau,na yeye ndo kilichomtokea,na hapo tayari uaminifu alishavunja.
Sema tu watu wazima kila wakivurugana, victims ni watoto. Baada ya wa kwanza, hato hao wengine wanaishi maisha ambayo hayakuwa stahili yao
 
mimi na waambiaga vijana kuoa single maza hakuna tofauti na kukopa mke wa mtu alafu ukaishi nae
 
Sema huyo jamaa aliyemuoa single mother naye ni kilaza wa kutupwa,unapo oa single mother kwanza,usijiingize kwenye mtego wa kusema huyo mtoto uliyemkuta naye ni wa kwako,ukataka mpaka majina atumie ya kwako,kama unalimpia ada au kumsomesha wewe lipa bila kuweka masharti yoyote yale,ukianza kuweka masharti mwishowe unakuja kujiumiza mwenyewe kama hivyo,
Mwache mtoto atumie majina ya baba yake huyo aliyemkata,kwa maana wewe huwezi jua mtoto amekataliwa kweli au la? Maana single mother asilimia 90 hudai kuwa wametelekezwa kumbe wakati mwengine ukweli wana ujua na wao ndo sababu ya kuachwa,husema wametelekezwa kutafuta huruma ili wapate ndoa,japo wapo baadhi walio telekezwa kweli
Nakuunga mkono mkuu

Sio kila single mother katelekezwa bali wengine wanavunja ndoa zao makusudi na mwisho wa siku ndio mambo kama hayo yanatokea.
 
Huyo jamaa aliyemuoa sister ako alifanikiwa kupata mtoto naye...ok, sometimes huwa tunafanya maamuzi flani tukidhani tuko sahihi au salama kwa namna flani,simlaumu sister ako ila aliteleza kumficha jamaa,alipaswa kumuambia mshikaji toka mwanzo yule fala alipoanza kumdai mwanae..alimkosea sana mwamba!
 
Back
Top Bottom