Single mothers nawaibia siri nyingine

Nani aliekwambia single mothers walipata mimba kwa kuamua?? Na una ushahidi kwamba wanawake wenye watoto hawakuwahi kutoa mimba
 
Nimeona nyuzi kadhaa na maoni kuhusu hawa tunaowaita single mothers, mitazamo iko tofauti sana kulingana na kila mmoja anavyoamini.

Hawa ni wanawake Kama wanawake wengine tu na wanastahili kuheshimiwa kwani wengi wao wamebeba majukumu ambayo wanaume wenzetu wameyakimbia

Sitetei feminism ila Ifike wakati tuache kuwaona kama walikosea pahala mpaka kupelekea kuwa Single mother kwani sisi wanaume siyo malaika pia

Kuoa single mother siyo kujitwika mzigo kama baadhi ya vijana wavivu wanavyofikiria kwani kufanya hivyo ni moja ya kujipima uwezo wa kuhudumia familia yaani mkeo na watoto wako/wake uliowakuta kwake

Single mothers wengi wanajitambua na hawanaga utoto tena kwakuwa wameshajua maisha yapoje, wanajua kulea watoto wanajua kuhandle mwanaume na kila material wanayo

Sina uzoefu nao ila nawaona vijana wengi wakijenga shavu baada ya kuoa single mother na mara nyingi mahusiano yao yanadumu sana

Nawasihi wanaume wenzangu tuache shutuma na tuhuma zisizo na msingi kwa hawa wanawake kama hatuwezi kuoa tutulie kimya kuliko kuwaangushia jumba bovu wanawake waliozalishwa na kuachwa/kuacha.Tuwape heshima na treatment ile ile wanayopata wengine

Wanawake wote ni sawa



Student
 
Upo sahihi kijana. Hii ni kutokana na uzoefu wako, pia maelezo yako yanatudhihirishia kuwa umeoa single mother.

Ila wengi ni pasua kichwa kutokana na retrospective history!!!

Komaa naye tu, utatoboa jombaaa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu sijaoa single mother ila sijaona bado matatizo yao yako wapi mpaka kupelekea kukosa mvuto kwenye ndoa
 
Sitetei feminism ila Ifike wakati tuache kuwaona kama walikosea pahala mpaka kupelekea kuwa Single mother kwani sisi wanaume siyo malaika pia
Si kweli wamekosea pakubwa.

Hata kama wanaume tunakosea pia, makosa yetu hayawafutii makosa yao.

Two wrongs don't make a right.
 

Nenda kaoe single mother, kama huna ozoefu bora ungekaa kimya. Watu wamepigwa wewe unakuja kutubania pua hapa eti wanawake wote Sawa?
 
Moderator muwe mnaangalia nyuzi za kuacha....humu ndani kuna tabia ya kubully sana single mother wakati hamna anayependa kuwa hvyo ni nyie nyie wanaume ndo mnaowazalizalisha na ķuwaacha halafu mko mstari wa mbele kuwatolea lugha chafu
Kiuhalisia huku mtaani wengi tu wanaolewa maana wengine sio kwamba wana tabia mbovu ni mambo madogo madogo yalitokea wakaachana
 
Alafu huyu jamaa sindo kaja na uzi kuwa single maza hataki mtoto wake aitwe ubiniwake akasema kapiga chini kipi kimetokea?
Au nimefananisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…