Nimeona nyuzi kadhaa na maoni kuhusu hawa tunaowaita single mothers, mitazamo iko tofauti sana kulingana na kila mmoja anavyoamini.
Hawa ni wanawake Kama wanawake wengine tu na wanastahili kuheshimiwa kwani wengi wao wamebeba majukumu ambayo wanaume wenzetu wameyakimbia
Sitetei feminism ila Ifike wakati tuache kuwaona kama walikosea pahala mpaka kupelekea kuwa Single mother kwani sisi wanaume siyo malaika pia
Kuoa single mother siyo kujitwika mzigo kama baadhi ya vijana wavivu wanavyofikiria kwani kufanya hivyo ni moja ya kujipima uwezo wa kuhudumia familia yaani mkeo na watoto wako/wake uliowakuta kwake
Single mothers wengi wanajitambua na hawanaga utoto tena kwakuwa wameshajua maisha yapoje, wanajua kulea watoto wanajua kuhandle mwanaume na kila material wanayo
Sina uzoefu nao ila nawaona vijana wengi wakijenga shavu baada ya kuoa single mother na mara nyingi mahusiano yao yanadumu sana
Nawasihi wanaume wenzangu tuache shutuma na tuhuma zisizo na msingi kwa hawa wanawake kama hatuwezi kuoa tutulie kimya kuliko kuwaangushia jumba bovu wanawake waliozalishwa na kuachwa/kuacha.Tuwape heshima na treatment ile ile wanayopata wengine
Wanawake wote ni sawa
Student