Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

K
Kwa mantiki hiyo mkuu, naamini kwa namna moja au nyingine wahutu watakua wanajipanga kulipiza ili washike hatamu wawachomoe Watusi.

Swali in je wanatumia mbinu gani kujipanga? Tuliona Kagame alitumia RPF akitokea msituni.
 
Mkuu je hizo silaha walikuwa wanapewa na Nani?serikali iliyopo madarakani au Kuna ufadhili walikua wanaupata?

Sent using Jamii Forums mobile app
Silaha za interahamwe zilikuwa..jembe.marungu .haya marungu yaligongwa misumari ya nchi sita kila sehemu mfano wa tunda la stafeli.nyengo.mapanga.mashoka.n.k.

Hizi silaha zilinunuliwa nchini china zililetwa rwanda makontena na makontena kwa ufadhili wa mfanya biashara ambaye alikuwa kiongozi wa interahamwe wakati huo george rutaganda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@LadyRed bwana, hili Jambo naona huwa unalizungumzia sana. Linakuumiza kwani? Ni kweli kuwa zipo jamii zilikuwa na privilege nyakati za mkoloni, ilà trust me nao walijiongeza sana tu, na wanazidi kujiongeza to-date. Zipo jamii hapa bongo hadi leo hii pamoja na fursa kuwa kwa kila mtu lakini bado they lag behind, hatuwezi kufanana na kuna watu naturally wapo gifted katika utafutaji na kusaidiana. Kuna sehemu leo hii ukienda vijijini japo ni afrika lakini hutaamini kuona palivyo, na kuna mahali ukienda unaweza kuishia kutoa machozi, ndani ya hii bongo.

So pamoja na privilege kuwepo kwa wote, kuna gifted hands, kuna watu wanabebana sanaaa, na wapo ambao hata dada mtu anaona wivu kwa mdogo mtu kuwin maisha.

Ya huko Rwanda siyajui sana, unaweza kuwa sahihi kwa analysis uliyofanya, ila kwa bongo mmmh.
 
Mkuu hapa ame eleza vizuri
Unanichanganya mkuu.inamana gani kusema hakuna kabila ya tusi na hutu? Sasa waliokuwa wanaopigana ni kabila gani vs kabila gani.maana tumesikia ni Vita ya wahutu na watusi.
Mkuu yale hayakuwa mauaji dhidi ya watutsi tu bali ilikuwa ni VITA yaani wakati wahutu wanachinja watutsi na hao Watutsi wanachinja wahutu kutumia vikundi vyao vya waasi mfano INTEREHAMWE/FDLR,APERHUTU kwa Wahutu na be it UPRONA/RPF kwa watutsi na ndio maana kule Uganda kwenye mitaala ya shule haiitwi Rwanda genocide kule tulisoma inaitwa Rwanda civil war yaani VITA sio Mauaji!!

Ila yaonekana kagame alikua kajipanga zaidi hivyo baada ya kushinda vita naye akalipiza kisasi akawachinja hao wahutu wakakimbilia DRC ambapo aliwafuata na kuwateketeza na tokea hapo nguvu ikahama kutoka kwa Wahutu ikaja kwa watutsi na imekua hivyo mpaka leo.

Wahutu sio kwamba wali-fight for nothing" ila walishashinda vita tokea 1959 na wakajikomboa kutoka mikono ya watutsi so walienjoy uhuru wao mpaka 1990 ambapo uvamizi wa Watutsi ulianza. Hivyo ile vita ilikua ni ya kujilinda zaidi dhidi ya uvamizi wa watutsi na sio kuvamia watutsi kama unavyodhani. Yaani kama watutsi wasingetishia kuvamia Rwanda kulikua hakuna haja ya wao kuwaua maana madaraka yalikua kwa wahutu.

Hope umepata picha mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitabu cha bodigad wa slim shade kinasema RPF walikua wanavaa kama interamwe na kwenda kuua watus wenzao ili wapate huruma ya dunia
 
Matukio kama hayo mi naona sawa mkiweka kwasabu mtoa mada hajaona yote kwahiyo fresh tu.
 
Nasikia majamaa yalikuwa kama mazombi ,,,,utapiga risasi hola linakufuata kibabe Mpaka likucharange ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kuna kitu kinaendelea kwa sasa, tunagawanywa kutokana na maeneo tunayotoka, japo sioni yakifika huko kwenye chuki ila sioni kama ina afya nzuri kwa taifa. Ukanda unaweza kutugawa kwa kiasi kikubwa tu, Kanda ya ziwa, Kanda ya kaskazini, Kanda ya kati na Kanda ya kusini. Na inasemekana Meku ndio aemeleta haya.
 
K

Kwa mantiki hiyo mkuu, naamini kwa namna moja au nyingine wahutu watakua wanajipanga kulipiza ili washike hatamu wawachomoe Watusi.

Swali in je wanatumia mbinu gani kujipanga? Tuliona Kagame alitumia RPF akitokea msituni.
Ukifika Rwanda utaona kama nchi yenye utulivu wa kutosha. Hata uhalifu mkubwa kama ujambazi na uporaji wa kutumia silaha umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa,iliyobakia ni udokozi mdogomdogo tu.

Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kua Rwanda kuna tension ya hali ya juu sana miongoni mwa raia wake. Ule utulivu na amani ni kama vimeshikiliwa na kamba nyembamba. Unahisi kwenye nyoyo za watu kuna kutokuridhika flani hivi na kilichokuwepo ni kuogopa mkono fulani wa chuma

Kwa maoni yangu Rwanda ya baada ya Kagame lazima iwe handled very careful vinginevyo kitanuka tena! Nilisafiri kutoka Kigali kwenda Goma DRC kupitia Gisenyi na pote upitapo na kuonana na watu na kuongea nao unahisi ni watu wenye wasiwasi sana na hasira! Tuiombee Rwanda yasijirudie yaliyopita
 
Hutu walikuwa wanapigana vita mbili.jeshi lilijikita kupigana na waasi kina kagame..walibaki wanajeshi wachache wakiungana na interahamwe kupigana vita ya ndani ya kuua raia wote wa kitutsi na kihutu ambao hawaungi mkono juhudi .
Sasa ikatokea vita ya kijeshi .waasi walikuwa vizuri wakawashinda jeshi la rwanda wakafanikiwa kuingia ndani.ikapigwa ya ndani wakashinda tena.interahamwe wakakosa sapoti ya jeshi na hawakuwa na silaha za kisasa.pia waliopunguzwa sana .wakasilimu amri wakakimbilia congo.tanzania.na wengine walijichanganya na raia wema kwenye makambi ya wakimbizi.maofisa wa jeshi la rwanda nao walikimbia nchi.ndio chanzo cha kagame kuwa na nguvu.kwasababu alishinda vita.kwahiyo kuna wahutu wengi interahamwe nje ya rwanda ambao wanatamani sana kurudi rwanda lakini wanamuogopa kagame.ndio maana tunahisi siku kagame akipoteza power.hawa wahutu wakirudi wanakiwasha tena.safari hii watawachoma mishikaki kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Barikiwa sana Mkuu,shukran kwa Wife kukuachia simu yake japo kwa muda ili utupe hii simulizi ya kusisimua! Jumapili njema na kwako pia!
 
Kwamba itakua wahutu ndio wanaleta hali ya wasiwasi ? I'm so curious to know the cause of that tension to citizens whilst there is Peace.
 
Haaaa nchi ilikuwa inaongozwa na serikali goigoi by nyerere @@@ raisi alikuwa mzenji legelege siyo kama huyo balozi mama wa kipemba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi vikundi vilipaswa kupigwa marufuku, green guard na red brigade vyote havifai kwa faida ya Taifa letu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…