Sintosahau nilivyosota miaka miwili bila kukutana kimapenzi na mama mtoto wangu

Sintosahau nilivyosota miaka miwili bila kukutana kimapenzi na mama mtoto wangu

Kabla sijaendelea,inaonekana alifuga kumguru.
Af pia,vitu vyote hivyo ulikuwa unafukia wewe tu? Na maskani ukifika tena ugali dagaa unafyeka! Af uzito wako ni kama wa Demi !!!!
Umemaliza F6 unajua kugegeda! Kumbe maskini tudada twa watu huko F4. Njaa mbaya.
Pole sana kwa mizinga FaizaFoxy
Kaka mi nilianza kugegeda tangu nipo darasa la saba
 
NAENDELEA NILIPOISHIA...

Alilia sana huo usiku na nilijaribu kumbembeleza sana hadi mi mwenyewe machozi yalinitoka lakini bado hakuzungumza chochote,(niliumia sana).
Kesho yake aliwaambia mashoga zake hapo kazini. Ila mmoja nilikua niko karibu nae sana alijaribu kunitafuta na kunieleza kua kile kitendo kimemvunja sana moyo mwenzangu yaani alikua analia kila mara. Nilijaribu kuomba msamaha lakini sikufanikiwa hata kidogo ila nikajipa moyo tu kua yataisha na mamb yatakua safi tu kama zaman kwani niliamini kabisa kua kwangu hawezi pindua.
Ilikua siku mara wiki baadae miezi yaani hataki kupokea simu zangu wala kujibu meseji zangu. (Kiuhalisia sijawahi kumbembeleza mwanamke niliyemkosea kwa muda wa zaidi ya mwezi maana huaga nafanya kujiongeza mwenyewe halafu namtupilia mbali ila kwake mtoto wa kiume nilikwama).

NGUVU ZA GIZA ZIKAINGIA KATI KUTETEA HISIA ZANGU

"Mapenzi yanauma mnoo mapenzi yanauma sana, MAPENZI SHIKAMOO!!"


Baada ya kama miezi mitatu hivi nikaona mwenzangu kaweka picha ya mwanaume mwingine kwenye whatsup acc yake. Niliumia sana !!
Nikazidi kuongeza kasi nimuweke karibu tuyazungmze lakini wapi.
Kiukweli hakuna kipindi nilichopitia kwenywe wakati mgumu kama hiko kipindi nimeachwa aisee niliteseka sana. Katika kipindi hicho ndo niligundua kua kumbe yule mwanamke nilikua nampenda zaidi ya nilivyokua ninamchukulia kwani ilifikia hatua nilikua nakula chakula kinakua kama kinanikaba kooni na mbaya zaid ilikua inafikia hatua nakosa usingizi kabisa. Kila ikifika usiku wa manane nilikua ninashituka na kuangalia simu labda kanitafuta nakuta ndo katoka online kama lisaa hivi nyuma na meseji zangu za wasap alikua anani blue tiki tu.
Baadae kuna shoga yake akanifuata na kunambia ,"shemeji kama bado uko na mpango wa kurudiana na X hapo utafeli kwani hivi sasa anatoka na P na yuko na ujauzito tayari.
Mwenzenu nilikonda nikawa kama mbwa koko.
Katika kutafuta ushauri kwa marafiki zangu kuna jamaa mmoja akanishauri niende kwa mganga nikamrudishe mpenzi wangu kwani nilionekana naenda kuwa chizi wa mapenzi.

"
Naomba nieleweke vizuri kabisa kua ninachokizungumza hapa ni ukweli mtupu"

Nilipelekwa kwa ustadhi mmoja hivi akanambia ninunue nazi tatu na nitafute picha ya huyo binti pia nimlipe kama 45k. Nilifanikiwa kuipata picha yake kwani tulikua marafiki facebook so nilienda kuprint moja ya picha zake.
Zile nazi ziliandikwa maneno ya kiarabu kwa marker pen nyekundu wakati tunafanya kisomo huo usiku wa manane. Baadae nikapewa jukumu la kwenda njia panda kuzipasua hizo nazi usiku. ( Mwenyezi Mungu naomba anisamehe sana mja wake). Nilifanikiwa kufanya hilo zoezi pia ile picha yake nilienda kuzika kwenye moja ya makaburi huku nikinuia kwa kusema," wewe X naomba uachane na huyo mtu uliyenaye na unipende mimi tu yaan ufe katika mapenzi yangu kama alivyolala mfu aliyemo ndani ya hili kaburi😭. (Allah Aniepushe na Haya madhambi🤲🏻).
Baada kumaliza hilo zoezi bado msoto ulikua pale pale wala hakua na muda na mimi kabisa😢
Ikanibidi niende kwa mganga wa kienyeji sana huyu alikua ni mwanamke na yeye akafanya yake (ila nilipoenda kwa mganga sikutaka tena yule mwanamke anirudie bali nilitaka tu anitoke moyoni mwangu manaa kila nilipokua nikimuona MOYO wangu ulikua unamua sana) . Huko nako niligonga mwamba!! Tabu ikawa pale pale!!!

NILIKUBALI KUACHIKA NA NIKAANZA MAISHA MAPYA CHUO KIKUU....

Nitaendelea...
"
samahani sana kwa usumbufu"
 
Back
Top Bottom