Just for curiosity: Wamiliki watahamishwa kwenda " Msovera" au watalipwa kupisha wajomba toka Arabuni?
Wakati Serikali ikibainisha mpango mpya wa 2026/2046 wa kuliendeleza eneo lote la Sinza jijini Dar es Salaam, wamiliki wa nyumba katika eneo hilo wamehoji ni wapi watakwenda kuishi mpango huo ukianza.
Pia, wamehoji ni namna gani wamiliki wanane wataunganisha viwanja vinane ili kupata ukubwa wa kiwanja kimoja na katika eneo litakalounganishwa ni nani atakuwa mmiliki?
Baadhi yao wametaka wapewe Sh1 bilioni ili kuyaachia maeneo yao kwa mwekezaji, wengine wakitaka Sh3 bilioni.
Mpango huo wa kuiendeleza Sinza mpya ni wa miaka 20 utaanza 2026, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiwa ndiye msimamizi, ikilenga kuwa na eneo jumuishi Sinza.
Mpango huo utahusu kujenga maghorofa ya makazi na biashara huku maeneo ya huduma za jamii kama shule na hospitalini yatabaki palepale lakini yataboreshwa kuwa ya ghorofa.
Hayo yameelezwa leo Jumapili, Aprili 19, 2026 na Ofisa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Emily Mwasogye katika kikao na wamiliki wa maeneo hayo.
Mwasogye amesema ardhi ya Sinza imejaa, hivyo Serikali inakwenda kulipanga eneo hilo kwa kwenda juu kujengwa maghorofa.
Pia soma ~ Mpango wa Serikali kuendeleza upya maeneo ya Sinza unahitaji uwazi na uwajibikaji