Hivi wewe kwa akili zako watu wa usalama wapo baa wamuone mlevi ana silaha anaitotoa/anaichezea chezea halafu wameshamuonya wao waendelee kukaa hapo wakati wanajua kinachofuata na madhara yake. Sana sana watakuwa waliondoka fasta kwenda kutoa taarifa kunakohusika na kama ilifanyiwa kazi kwa wakati au laa mimi na wewe hatuwezi kujua. Shida ya watanzania wengi bado hawana macho ya kuona hatari mbele yao na hawachukui tahadhari mpaka yawakute. Siku zote ukishaona mtu mahali hasomeki halafu anachezea chezea silaha hata kama ni panga/kisu wewe sepa zako ikiwezekana katoe taarifa kunakohusika huko mbele ya safari lakini sio kuendelea kukaa karibu nae.Nilisikiliza mashuhuda wa tukio la huyo jamaa kuua. Marehemu aliyepigwa risasi kosa lake kubwa ni kumfuata mlevi mwenye silaha, tena ameshamrisha DJ azime muziki na kupiga risasi mbili juu eti kumpa tahadhari aache bugdha. Alichotakiwa kufanya ni kumlia timing na kumpokonya ile silaha bila kutoa onyo lolote. Alitakiwa kijipima kama anaweza kumdhibiti na afanye hivyo kwa haraka bila kumsemesha. Vinginevyo alitakiwa kuondoa haraka sana eneo la tukio. Hivi huyo afisa usalama anayesemekana alikuwepo hakuna na silaha am-shoot? Au pengine alikuwa hajabeba silaha.