Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Hili ni angalizo kuelekea wikendi.
Mabinti, msiwaamini sana wanaume! Kama mna hela, hakikisheni mnakabeba. Sio kila mwanaume anayeenda chooni anaenda kujisaidia, wengine huenda kuangalia salio lililobaki. Wengine wakiona bili ni kubwa, wanatafuta njia ya kutokea karibu na choo.
Nawaambia, mtaaibika! Hali si nzuri, wanaume siku hizi hawana mshipa wa aibu. Jana nimeona dada mmoja yamemkuta, walimng’ang’ania hadi tukachangishana kumsadia. Kibaya zaidi, tulilipa hadi vinywaji alivyokunywa maana alitelekezwa!
Hili lilinikumbusha kilichonipata mwaka 2018 kwenye baa moja Mikocheni. Nilipotoka kazini, shemeji yangu wa zamani aliniita nikaungane naye. Nilipofika, nilimkuta anakunywa na jamaa mmoja, akasema ni mfanyakazi mwenzake. Wakaniletea bia tatu na chakula, nikakula.
Ghafla jamaa akaondoka, nikamuita mhudumu niletewe bili yangu, shemeji akasema jamaa anarudi na atalipa zote. Ilipotimu saa tatu usiku, jamaa bado hapatikani. Nikamwambia shemeji yangu nalipa vya kwangu, akaniomba nisaidie zake, nikamwambia siwezi!
Mhudumu alileta bili yangu, nikailipa. Lakini yao ilikuwa shilingi 49,000! Akaja meneja, akasema tusiondoke mpaka polisi waje. Nikamwambia naondoka, na kama kuna tatizo, asome namba ya gari langu.
Nililipa nilichokula na kunywa, kisha nikazima simu. Baadae nikamhadithia kaka yangu, akacheka sana na kuniambia "ukome mteremko!"
Huyu sasa ni shemeji X kabisa! Sijui hata waliishiaje au kama aliniset na jamaa yake aliyekuwa naye.
Muwe makini na hizi ofa! Kama huna kitu mfukoni, jihadhari. Kukimbiana kwenye baa na klabu imekuwa michezo ya mjini kwa sasa. Mungu awalinde, wikendi njema!