Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Kama kijana nimekuwa nikipata maswali mengi sana toka kwa vijana wenzangu pale ninapojaribu kuonesha husia zangu au pale ninapotoa hoja zangu zinazoonesha kuiunga mkono iwe hapa ama mahali kwingine kokote.
Maswali hayo yamekuwa wakati mwingine yakiuliza chanzo changu cha hamasa ya Chama.
Unaweza kutana na maswali kama " wewe Mzazi wako nani CCM"
Swali hili limekua likinipa mawazo mengi , maswali ambayo moja wapo ni kama uanachama wa mtu katika chama cha siasa unazingatia kigezo cha mzazi kuwa sehemu ya chama husika.
Naishia kujuiliza nia hasa halisi ya swali hilo.
Historia ya vyama vingi hapa nchini inaonesha kwamba vyama vilivyopo sasa vimeanza 1992, na kabla ya hapo hakuwahi kuwepo vyama vya upinzani tunavyoviona sasa ukiachana na vile vilivyokiwepo nyakati za ukoloni.
sasa tukianza kusema kwamba ili uwe mwanachama wa chama flani cha siasa basi mizizi iaznie kwa mzazi, wanachama wengi wa vyama vya upinzani na hata waanzilishi watakosa sifa hiyo.
Tukija katika CCM pia iliyoanza 1977 baada ya muunganikonwa ASP na TANU tunaweza kuona kwamba wanachama wa CCM waanzilishi wangekosa sifa ya kuwa wanachama.
Hivyo basi hoja ya kwamba uanachama wa mtu na umuhimu wake unatokana na mizizi yake katika chama inakua ni hoja mfu isiyo na mantiki yeyote na ninaweza iona kama hali flani tu ya kujikweza na kushindilia ubinafsi uliopitiliza pale haswa lilapokuja swala la mgawanyo wa madaraka.
Binafsi ningependa kuona kauli hii ya kibinafsi inayotaka kujijenga katika vyama vyetu vya siasa ikipingwa na kila mzalendo anayelitakia mema Taifa lake kwa nguvu zote.
Niwatakia sikukuu njema ya Mapinduzi.
Wasalaam
Stroke.
Dar es Salaam.