Sio Uchawi, hii ndio mbinu wanayotumia wakinga kuteka biashara kwa spidi kali na mfanikio makubwa, mbinu rahisi ambayo kabila lolote linaweza kutumia

Sio Uchawi, hii ndio mbinu wanayotumia wakinga kuteka biashara kwa spidi kali na mfanikio makubwa, mbinu rahisi ambayo kabila lolote linaweza kutumia

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ni jamii ambayo ilikuwa haijulikani lakini hivi karibuni kutoitambua ni sawa na kusema hakuna kitu kwenye chumba mlichomo na tembo, hata kwa wanaofunga mizigo yao soko kubwa kuliko yote nchini pale kariakoo ni mashuhuda, hawa watu ni kama wameimeza kariakoo, kuimeza kariakoo ni sawa na kuwa mfanyabiashara mkuu wa bidhaa zinazouzwa madukani nchi nzima.

mbinu kuu ni kuinuana, nyingine zinazofata ni ngumu kutekelezwa bia kuinuana

KUINUNUANA

1655655367667.png


Wakikopeshana wana nidhamu ya kurudisha, Wakiinuka kwa kuinuliwa wanayo nidhamu ya wao kuwainua wengine

Mbinu ni nyepesi mno na ninahofia endapo kabila kubwa likiiga basi litakuwa mbali sana kimafanikio, mbali sanaaaa!!

Kinachofanyika ni swala la kuwa na umoja unaowaunganisha wakinga waliofanikiwa Dar kuinua wenzao wenye biashara ndogo mikoani waende kufanya biashara kubwa dar.

Kunakuwa na umoja kwa mfano wanakuwa wakinga 500, kinachofanyika ni kwamba kila mwezi kila mtu awe mfanyabashara au kaajiriwa inabidi atoe elf 50, laki, laki 2, n.k kutokana na status yake, hata ukitoa M ni wewe tu.

Hapo kila mwezi huwa inapatikana takribani milioni 50

sasa kitachofanyika hapo, wanamchagua mkinga ambae ana fanya vizuri kwenye biashara yake ndogo huko mikoani walikojazana kama Mbeya, Songwe, Iringa, n.k..wanamchangia mtaji ahamie Dar, ile biashara ndogo huwa tayari wana watu wanaosaidiana ndio ambao wataendeleza yeye akienda kariakoo.


wale waliomchangia tayari huwa wana frem zao kibao pale kariakoo, watampa frem mwanachama mpya na kumshughulikia mambo ya vibali..

Mwanachama mpya ataamua afanye biashara ipi, akishaamua ataletewa mzigo na wakinga wenzake ambao wamejazana kama utitiri kwenye jiji la Guangzhou huko nchini China, hili jiji lina viwanda vya kutengeneza bidhaa, machimbo ya kununua bidhaa, bandari ya kusafirishia, n.k. wakinga ni wamejazana sana huko (kwa waliofika ni mashuhuda), hao ndio huwa wanasaidia kutafuta na kusafirisha bidhaa kwa wenzao, wana kampuni yao kubwa tu ya kusafirisha mizigo inaitwa mapembelo cargo, hilo neno mapembelo ni salamu ya kikinga, ukisalimiwa mapembelo unajibu vavene,😂


Mzigo ukifika bandarini tayari tayari wana umoja kusaidiaa connections za kuutoa chap chap mzigo unaingia fasta dukani unaanza kuuzwa kwa wafanyabiashara wanaojumua,

Kuuza kwa faida ndogo ili kuwa na wateja wengi.

Wakinga hutumia kanuni ya kuwa na nidhamu ya kuikandamiza tamaa ya faida kubwa kubwa, kanuni yao ni kuuza kwa bei ndogo kwa lengo la kuuza bidhaa nyingi kwa mpigo na kupata wateja wengi, Heri faida ya elf 5 kwa kuuza pakiti 5 kila siku kuliko faida ya elf 20 wiki nzima kwa kuuza pakiti moja. Bei ndogo ina faida pia ya kutangaza biashara zao bure kabisa, hata humu jamii forums kuna uzi wa kufahamishana machimbo ya kufunga mzigo kariakoo na kigezo kikuu ni wapi wanapouza bidhaa ile ile kwa bei rahisi.

Wakiipata pesa wanayo nidhamu ya matumizi yake

Wakinga wengi ni kawaida kuwakuta asubuhi wanaenda na mahotpot kwenye biashara zao, wengi ni bora anywee hata bia zake mbili nyumbani kwake kuliko kwenda bar, n.k. kwa wale tuliowahi kuishi hata Mbeya unamkuta mtu ana duka la Hardware kubwa si mchezo anauza sana lakini gari yake ya kawaida tu premio lakini ana scania zake kwajili ya kumletea mzigo kila muda...

Bidii ile ile bila kutobweteka

Bidii huwa ni ile ile, Wengi kupumzika huwa ni kumapili tu haijalishi wamefanikiwa kiasi gani, ni kazi mtindo moja jumatatu hadi jumamosi asubuhi hadi jioni.
.........................................................................

Hadi wamefika hapa si rahisi maana Zamani wakinga waliokuwa wnafika Dar walikuwa wamekulia kijijini kwa muda mrefu sana na umri umeenda kidogo na mbaya zaidi huko walikotoka elimu ilikuwa duni,,, hali hii iliwafanya wapitie mitihani mingi sana kama kutapeliwa, ilikuwa ni kawaida sana kukuta mkinga kashazoea kuvaa ndala zake na koti lake, yani kama yupo kijijini huko Makete na ndio kashazoea hivyo, kwa siku hizi zama zimebadilika wanafaidi mema, hata ukienda kariakoo utawakuta vijana wao ndio wanauza suti za kujumua na mabelo ya nguo kwa hio wanavaa vizuri tofauti na babu zao wa miaka ya zamani.

Kuhusu uchawi kiukweli hili jambo nimelisikia mda mrefu, nakwambia biashara ni kuwa na bidhaa au huduma sahihi, jua soko linataka nini na ulete kile soko linataka, watu tutakutafuta tu popote ulipo. mambo ya kafara ni kweli yapo ila ni wachache huyafanya kama ilivyo wafanyabiashara wa makabila mengine, haya mambo ni imani ya mtu binafsi na huwezi kumzuia kwenda kwa mganga kuiza nafsi yake, haya mambo yapo hata makazini kwenye kupanda vyeo, hata wanasiasa baadhi hungarisha nyota zao kwa uchawi hasa kipindi cha uchaguzi kikifika ni foleni kwa waganga. ni hata kwa wachaga wafanyabiashara wakubwa jamii huwachukulia wanafanya wizi na utapeli kupata mitaji na ni kweli wapo wa aina hii lakini ni wachache sana, sio wote. ni vile tu watu hutilia umakini mabaya machache na kupuuza mengi mazuri. Ingekuwa ni rahisi kupata pesa utajiri kichawi basi kuna baadhi ya makabila siwezi kuyaweka hapa wangekuwa mbali sana.

sasa sipati picha kabila kama wasukuma, wachaga, wanyakyusa, wahaya, hawa wenye idadi ya watu milioni 2 na zaidi, kabila moja wapo wajikusanye wawe na umoja wa watu hata elf 10 tu wawe wanachangiana hata elf 50 kila mwezi,

watu elf 10 x shilingi 50,000 = milioni 500 pesa taslimu

ni kiasi kikubwa sana hicho kinaweza kisiishie kuinuana kwa mitaji bali hata kielimu na kuendeleza makwao.

Tatizo kuu wengi hawataki waendelee ili wao wawe juu kuliko wenzao, hiki ndicho kinawapa raha.
 
Wakinga wanajulikana kwa kafara zao kwenye biashara.
Hio ni negative mindset tuliyonayo wafrika, tukiona ngozi nyeusi ambayo sio kabila letu linafanikiwa huwa tunalenga zaidi kuwasagia kunguni badala ya kujifunza kutoka kwao.

sipati picha kabila kama wasukuma wanaoongza kwa idadi kubwa ambao wapo takribani milioni 5 wangeyumia hii system.

Yani wangejikusanya wawe hata elf 10 tu basi wasingegusika

wasukuma elf 10 x 50,000 = milioni 500 pesa cash taslim kila mwezi

hio ni pesa nyingi mno, ni bilioni 6 kwa mwaka hio, hapo inatengwa bilioni 3 kwajili ya mitaji,nyingine inayobaki wanapeleka wale vipanga haswaa waende kusomea vyuo 10 bora duniani warudi na elimu za kisasa za kusaidia nchi ma jamii yao sio hizi elimu zetu za kikoloni, pesa nyingine ijenge madarasa huko vijijini, pesa nyinginr kusaidia wanafunzi wenye uwezo mkubwa kuendelea na vyuo vya hapa bongo waje kuwa wanasheria, madaktari, n.k.


ila ndio hivyo tena, mchawi anatafutwa ila huwa ni sisi wenyewe watu weusi, utakuta hata huo muungano ukiwa na watu 10 tu kila mtu anataka pesa iliyochangushwa imsaidie mdogo wake au kaka yake hata kama hawezi biashara.
 
Wakinga wanajulikana kwa kafara zao kwenye biashara.
Biashara ni kuwa na mali mkuu siyo uchawi,jua soko linataka nini lete kile soko linataka uza tutakutafuta tu popote ulipo!(sikatai/na siwezi kuthibitisha uwepo wa kafara) ila ukweli wa kwanza ni huo.

Ukitaka kuniamini kauwe nduguyo kisha kafungue biashara usiweke bidhaa zenye tija uone ukweli ulivyo.
 
Hizo story za kwamba wakinga ni washirikina huwa siziamini kabisa ila nachojua wakinga ni watu wakubebana sana sasa makabila mengine mtu mmoja akifanikiwa anataka awe anaonekana pekee yake kwenye ukoo kitu ambacho sio sahihi
 
Kariakoo yupo jirani yangu mkinga asubuhi wakija wanakuja na hotpots kubwa chakula kutoka home marufuku kununua chakula.

By the way,ubahili siku zote ndo huifadhi shilingi so wanachokifanya ni sawa.
Unaona sasa, lakini pia chakula kinakuwa salama maana wamekipika wao wenyewe tofauti na cha kununua mtaani kila siku.

ila wapunguze ubahili huu muda mwengine wawe wanaenda hotelini
 
Biashara ni kuwa na vitu mkuu siyo uchawi,jua soko linataka nini lete kile soko linataka uza tutakutafuta tu popote ulipo!(sikatai/na siwezi kuthibitisha uwepo wa kafara) ila ukweli wa kwanza ni huo.

Ukitaka kuniamini kauwe nduguyo kisha kafungue biashara usiweke bidhaa zenye tija uone ukweli ulivyo.
Umejibu vizuri sana
 
Hizo story za kwamba wakinga ni washirikina huwa siziamini kabisa ila nachojua wakinga ni watu wakubebana sana sasa makabila mengine mtu mmoja akifanikiwa anataka awe anaonekana pekee yake kwenye ukoo kitu ambacho sio sahihi
Kama sisi wahaya unakuta mnapgana vita kabisa mtu wako wa karibu anakusagia kunguni uzidi kuwa nyuma, matokeo yake hadi mkoa wetu umerudi nyuma sana kimaendeleo wakinga wanabebana nazani ndio winning yao hiyo kwenye biashara
 
Kama sisi wahaya unakuta mnapgana vita kabisa mtu wako wa karibu anakusagia kunguni uzidi kuwa nyuma, matokeo yake hadi mkoa wetu umerudi nyuma sana kimaendeleo wakinga wanabebana nazani ndio winning yao hiyo kwenye biashara
kwa jinsi wahaya walivyokuwa na uwezo mkubwa darasani nadhani hio pesa ingekuwa inatumika kugharamina ada za wanafunzi wenye uwezo wakasomee vyuo 10 bora duniani, mngekuwa hamkamatiki kwenye elimu na mngekuwa na maprofesa kama utitiri.
 
Kwahiyo sasa hivi sio wachagga na wahaya tena ni wakinga? Loh..... Haya basi sawa.
 
Back
Top Bottom