Timu yetu ya taifa bado haina mbadala wa Msuva na Samatta, vijana wenye vipaji wapo ila wakipewa nafasi wanaleta ubishoo tu, hawana tija.
Mechi ya mwisho itaamua japo nafasi yetu ni finyu sababu Guinea wametuzidi uwezo kiasi, wana kasi mno na mechi na DRC wanaelekea kushinda au kupata droo.
Taifa stars inacheza vizuri kipindi cha kwanza, wakiingia second half hawana morali na hawana pumzi tena kama mwanzo, wanakata moto na kukaba bila utaratibu na bila umoja , wanazurura tu uwanjani, mazoezi ya kukimbia na pumzi ni muhimu sana kwasasa ili tushinde mechi ya mwisho. Nashauri wakimbizwe tu mazoezini kwa dakika 200 , maana mpira wanajua.
Nampongeza sana kocha Morocco kuna namna kaamua kufungua akili anapanga kikosi imara siku hizi. Sijui alikuwa wapi siku zote. Mechi ya awali na Ethiopia tulipaswa kushinda, hii iwe fundisho kampeni zetu za Afcon zianze mwanzo kwa timu kupambana na kushinda mwanzo sio kusubiri hadi mechi ya mwisho. Timu yetu ni kubwa kwasasa wachezaji wajiamini hakuna kuogopa timu yoyote tena.
My take
Ushauri kwa wachezaji wa taifa stars waache rafu za kipumbavu hasa za kuumiza wapinzani kutokea nyuma, binafsi wananiboa sana, kucheza rafu za makusudi ni kuonesha uwezo wa mchezaji ni mdogo, nawashauri wanapopitwa wasiwakwatue wapinzani kwa nyuma waache waende kwani mbele si kuna mabeki rafu za nini, wamejaa ujinga mtupu, mechi ya leo refa katubeba sana katunyima kadi zetu nyingi , mechi ya mwisho na Guinea taifa stars waache huo ujinga wa rafu za kijinga watakula red, ukipitwa kimbiza ila usicheze rafu. Hiyo anayo zaidi Mzize, Msuva, Mudathir na Miroshi acheni hizo mtaikost taifa stars.