Sioni kama kuna haja ya kuendelea kutumia wachezaji wazee kwenye Timu ya Taifa

Andaeni mashindan kwa vijana tena kule mtaani ila mpira wa bongo ni figisu
Hiyo vyote vishafanyika ila kuwapata wachezaje aina ya Samata na msuva ni bahati unaweza kupata mchezaji mwenyekipaji ila hajitumi wala Hana nidhamu
 
Hao vijana unaowataka wako wapi? Hao wazee hawana viwango. Sisi kelele nyingi.
 
Wewe unafikiri kuna kocha mle?
 
Tanzania haijawa tayari kumwacha Samata au msuva kwakua Haina wachezaji wenye draja ilo.

Samata ana uwezo wa kukaa na mpira kusubiri wenzake, ana uwezo wa kushambulia peke yake japo umri ume mtupa ila hakuna mwenye uwezo kama wake kwa Sasa.

Ao wakina Kibu na Mzize Bado Wana safari ndefu kufikia ata uwo uwezo wa Chini walionao Samata na mMsuva.
 
Swali fikirishi je hao wachezaji vijana wana uwezo na uzoefu, nadhani walisha wajaribu
 
Mleta mada umekurupuka kuleta mada hii. Ulitakiwa ujue kwanza taifa lina hiyo mipango ya kuandaa timu kuelekea AFCON 2027? Kiufupi haina. Na kama mipango hiyo ipo unategemea hao under 23 wataitwa wenyewe tu pasipo kuwachanganya mdogo mdogo mpaka nao wanakuwa wazoefu? Kama mipango hakuna je alitakiwa aitwe nani wa kumzidi uwezo samatta,msuva,mo hussein,kapombe,manura,mudathir ktk nchi hii? Wameitwa kulingana na kuonyesha uwezo mkubwa kuwazidi wengne hao unaowasema under 23! Hao under 23 waliopo,licha ya taifa ya kutokuwa na mipango ya kuwaandaa,wanatakiwa waoneshe uwezo wao wenyewe wataonekana hivyo wataitwa na hao akina samatta tutawasahau!
 
Umeelewa nilichosema?
Kwahy mtawatumia hao mpka lini?
Tulia maana kwa hatua tuliyopo wanahitajika watu wenye uzoefu kutuvusha,Huyo Edwin Balua unayetaka acheze inafaa aongeze juhudi na maarifa,umeambiwa hatutaki ushauri wa kipumbavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…