Sioni sababu ya kuilaumu CCM na Mahakama Wakati aliyefungua Kesi ni Mwanachadema


Nipo kwenye vita na Rashidi, wote tumeoa na tunawatoto.

Rashid katumia mtoto wangu kunishambulia au kamrubuni Mke wangu akanisaliti.
Lipi kosa la Rashid kumtumia Mke au mtoto wangu kushinda vita yake na Mimi?

Kumbuka CCM na Chadema wapo kwenye vita vya Kisiasa.
Kuibiana wanachama ni Jambo la kawaida kwenye vita hiyo.

Ni kama M23 kuwalaghai wanajeshi wa Kongo.

Ambacho sitataka kuona na Sisi tusio na chama ni uonevu na mauaji lakini hiki kinachoendelea ni Makosa ya kawaida ya chadema ambayo CCM wanayatumia
 
Mtibeli, una hakika kuwa Salumu Mwalimu ni Chadema? Au yule amvaye yuko Chaumma wamefanana tu majina?

Vv

Hao wote walikuwa Chadema.
Ni kama wale Askari wa Kongo waliojiunga na M23.

Kwa hiyo Mkuu huoni makosa ambayo chadema wanatakiwa kuyafanyia kazi kabisa?
 
Huyu mwamba mtoa mada nilikuwa namheshimu sana ila leo amenishangaza saaana yaani hajuhi adui anatumia mbinu zote.ata chauma atawalaumu chadema??

Nachojaribu kuwaambia msilalamike, wenzenu wanatumia weakness zenu kwa nini ninyi hamtumii zakwao?

Mkiendelea hivi shughuli itawachachia nawahakikishia.

Ukitaka kumuua nyoka gizani anzia kumulika miguuni. Ninyi mnamulika mbali wakati nyoka wapo miguuni mwenu. Mkiambiwa hamtaki.

Sawa
 
Eleza how does that concern CCM wakati wanaoshitakiana ni Wana CHADEMA.

 how ???
kivipi. ???
Wewe nikikujibu utajinyea..............kwanza kamsikilize Jebra Kambole Wakili wa Chadema, Kama unaweza ku-connect dots utaelewa nani aliyoko nyuma ya haya yote. Fungua bongo utaelewa.
 
Eleza how does that concern CCM wakati wanaoshitakiana ni Wana CHADEMA.

 how ???
kivipi. ???
CHADEMA sasa hivi inajichuja, pumba zinaelea mchele unabaki chini. Hakuna mwanachadema mwenye akili timamu anayeweza kuishitaki Chadema chini ya uongozi wa mwamba Tundu Antipas Lissu.
#NO REFORMS NO ELECTION
 
Mkuu nilikuwa nakuona wewe ni mtu wa kusoma alama mapema sana, kumbe nilikuwa najidanganya
 
Kuna baadhi ya masuala hayahitaji uchambuzi wa kina ili kuonesha kwamba una akili, yanahitaji tu uchunguzi wa kawaida kubaini kuwa serikali inahusika moja kwa moja. Uchambuzi wako hauoneshi akili hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…