Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Mimi ni mwanachama wa CCM. Kwa sasa CCM ipo chini ya Samia ambaye pia ndio Rais wa JMT.
Kwa utaratibu waliojiwekea CCM ingawa haupo kwenye katiba ya chama au kanuni nyingine, mtu akiwa kwenye nafasi ya Urais kipindi cha kwanza, ni vizuri anaachiwa pia kipindi chake cha pili ili aweze kukamilisha sera zake na maono yake katika ujenzi wa Taifa. Ikitokea hataki yeye mwenyewe ndo chama kinakubali na kuweka mchakato wa kupata mwingine kama ilivyotokea kwa Idris Abdul Wakil kule Zanzibar miaka ile.
Hivyo kwa sasa ni wazi atakayependekezwa na chama CCM kugombea na kushika usukani 2025-2030 ni Rais wa awamu wa 6 Samia Suluhu Hassan. Endapo kuna mtu anataka kupambana nae kwa sasa ili ashike usukani 2025-2030 huyo bila shaka anaweza akawa anakiuka taratibu za chama ambazo ingawa hazijaandikwa popote ila chama kinaziamini haswa.
Kuhusu Mawaziri kujiandaa kuwa Marais 2030. Kwa hili sioni kosa lolote. Kwanza hili jambo ni zuri kwa sababu linawapa muda mzuri wananchi kumpima huyo mtu kwenye kila eneo kabla ya kumwamini na kumpa nafasi ya kuwa kiongozi Mkuu wa nchi.
Ningependa kuwashauri CCM kuunga mkono jambo hili na kutolichukulia kama uhaini kwa sababu hata kwao litakuja kuwapa faida hasa kwa kupata mtu sahihi kwa mazingira sahihi.
Kwa nchi nyingi Duniani viongozi hawaibuki kama uyoga tu ila wanapimwa kwa kipindi cha kutosha na pale wanapokuwa viongozi wanafahamika vizuri na wananchi wao.
Kwa Dunia ya sasa kiongozi mzuri lazima apimwe na wananchi wake hasa kwenye uwezo wake wa kifedha, Je, anaweza kutafuta fedha? Kuhusu maendeleo yake binafsi? Je, ana maendeleo ya kuridhisha binafsi? sio mtu anatuomba uongozi mkuu wakati hata yeye hakuwa na uwezo wa kujiletea maendeleo binafsi sasa atawezaje kuleta maendeleo kwa wengine?
Lazima tumjue kwa muda mrefu ili tumpime pia kifamilia kama Familia yake ikoje? anawaongozaje mke wake na watoto? Au mume na watoto maana kipimo kikuu cha uongozi kipo ktk ngazi ya familia. Lazima tujue pia uwezo.wake kiushawishi ktk kuifanya dunia ije Tanzania, ifanye biashara na Tanzania, iwekeze na kuleta mitaji Tanzania na kwa hilo hatuwezi kukiachia chama cha mapinduzi tu ndo kifanyw hilo.
Watanzania tunahitaji kuwajua wataka Urais kwa muda mrefu ili tupate muda mzuri kuwa assess hawa watu katika maeneo haya.
Hili pia litasaidia kupata kiongozi ambaye ni Mtanzania kweli na sio pandikizi. litasaidia pia kupata mtu mwenye afya njema ya akili maana kwa muda mrefu watu wattapata kujua historia yake vizuri.
Naomba kuwasilisha