Sioni tatizo lolote mtu kujiandaa kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2030

Mimi ni mwanachama wa CCM. Kwa sasa CCM ipo chini ya Samia ambaye pia ndo Rais wa JMT.

Kwa utaratibu waliojiwekea CCM ingawa haupo kwenye katiba ya chama au kanuni nyingine, mtu akiwa kwenye nafasi ya Urais kipindi cha kwanza...

Tujiandae kisaikolojia kuwapisha Watanzania wenye uzalendo kushika hatamu za nchi ili kuwavusha watanzania kwenye mtanziko wa sonona za kisiasa tangu tumeingia vyama vingi
 
Wakati wa chuma waligombea.? Why now? Ngoja mama awale vichwa
 
Tupe uthibitisho yanaharibuje utendaji serikalini?

Mtu kujiandaa kuwa Rais kunaongezaje vitendo vya Rushwa? Rushwa zinazotokea siku zote zinatokana na Watu kujiandaa kuwa Marais?
Ukiulizwa jibu, sio unajibu kwa kuuliza, we vipi!.

Makundi ya Urais CCM ndio chanzo cha rushwa na ufisadi, mfano 2015, kuna jamaa alikamatwa na pesa Dodoma akiwa anajiandaa kuhonga wajumbe.

Siku hizi umekuwa chawa haya mambo huwezi kuyakumbuka.
 
Urais wa 2030 unatafutwa Kwa kuhujumu jitihada za Rais aliyepo madarakani kutimiza ahadi alotoa Kwa wananchi?

Urais unatafutwa Kwa waziri kuacha majukumu aliyopewa na aliyemteua na kufanya UDALALI wa gesi ya wafanyabiashara?

Urais unatafutwa Kwa kutengeneza mgao wa umeme?

Urais unatafutwa Kwa waziri kuacha ofisi na kwenda kusikiliza kero za wananchi zisohusiana na wizara husika ya fedha aloteuliwa kwayo??

Uwaziri unatafutwa Kwa kupandishwa Bei za vifurushi vya data Ili zipatikane pesa za 2030?
 
Kwani 2025 hakuna uchaguzi wa RAIS!?
 
Hata Mimi sidhani kama ni dhambi ila DHAMBI inakua kwenye CHADEMA wakitaka kufanya siasa wanaletewa mambo ya kishenzi, kihuni na kipuuzi na SERIKALI ya CCM kwa kushirikiana na Polisi na usalama. wajinga Wakubwa hawa
Siasa ziliishia kipindi cha kampeni sahz ni mikutano ya kazi na kutatua matatizo ya wananchi.
 
Na Mimi nautafuta KWA kufundisha KWA bidii wanafunzi!!!

Sijui nani ataniona nafaa!?
 
Na Mimi nautafuta KWA kufundisha KWA bidii wanafunzi!!!

Sijui nani ataniona nafaa!?
Ndugu Hawa wasaka urais wangeshirikiana kuhakikisha inapatikana KATIBA mpya, ingesaidia kuepusha kufukua makaburi.

Maana hawajui kama Katiba mpya ikikwama AJAYE akiingia hatotoka Hadi MAONO yatimie.

Yaani vyama vingi ndo itakuwa basi tena.

Hakuna RANGI ambayo hawatoona wanaotuibia nw!!!!
 
Mkuu

Hivi BADO tunae tena mwingine kama yule wa kulala nao mbele kwa mbele!?

Si hakuna mwingine tena!!?

Ina MAANA FDR NDIO huyo atakaewaminya ipasavyo tena!!?

Duh!
 
Kazi unaitafsiri vipi? Vitu vingi sana ambavyo sio kazi ni vitu gani?

Katiba yetu inataka candidates wasiwe vichaa hivyo hakuna umuhimu wa kuwazungumzia vichaa.
Kwani vichaa hawapigi kazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…