- Thread starter
- #61
Tofautisha umuhimu wa daraja la Kigamboni na hili, population ya Kigamboni ni kubwa activities zake ni nyingi na huko Kigamboni inakwenda kuwa manispaa.Wewe hujui barabara za huku Mikocheni,Mbezi beach,Msasani,Masaki. Kwa taarifa yako jinsi foleni inavyokuwa kali watu wa mikocheni au mbezi walikuwa wanaingilia maandazi road(siku hizi kuna barabara ingine ya DMDP unaingilia Tanesco Mikocheni unatokea Msasani) wanapita CCBRT wanatokea O'bay kuja kukatisha Kenyatta Drive ili kukwepa foleni ya Ali Hassan Mwinyi road. Kwa maana hii watatumia njia hio hio ila hawatarudi Kenyatta tena wataunganisha darajani. Hili daraja sio kwa watu wa Masaki tu acheni negativity.
Maneno haya haya yalisemwa wakati daraja la Kigamboni linajengwa na hadi leo watu wasiolitumia bado wanaongea ujinga kuwa daraja halina msaada wowote. Waulize wakazi wa Kigamboni wanaotumia hilo daraja wawaambie umuhimu wake.
Unataka kusema mtu wa mbezi beach akishashuka cocobeach foleni ndiyo inakwisha sidhani, ndiyo maana nimesema ni daraja la wakazi wa Masaki tena lingeitwa Masaki bridge.