Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa

Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa

Oysterbay ,Masaki wanakaa wazungu na viongozi wa serikalini ,ambao wengi wana magari binafsi,hawana tabu za madaladala,lakini huko uswekeni wakijenga daraja hil la mkwajuni-muhimbili hapa kati tunapiga lege tu TZ 11 ambapo ni shortcut kwahiyo nauli nauli za kwenda KKo/Posta zinapungua.
Aisee!
 
Tofautisha umuhimu wa daraja la Kigamboni na hili, population ya Kigamboni ni kubwa activities zake ni nyingi na huko Kigamboni inakwenda kuwa manispaa.

Unataka kusema mtu wa mbezi beach akishashuka cocobeach foleni ndiyo inakwisha sidhani, ndiyo maana nimesema ni daraja la wakazi wa Masaki tena lingeitwa Masaki bridge.
Daraja hili litatumiwa na wengi si wakazi wa Masaki tu. Kwanza sasa hivi nyumba za Masaki zaidi ya 50% ni ofisi ambazo wafanyakazi wengi si wakazi wa Masaki.

Sijalinganisha Kigamboni bridge na hili nimelitaja kukumbusha watu walivyokuwa wanasema halina maana.
 
Ivi mbona nyie kaz yenu kupinga tu kila jambo? mtu unakaa kwa mtogole utaujua saa ngapi umuhimu wa barabara hii...mimi naishi kunduch na ili kukwepa foleni huwa nikifika moroko naingia msasani then oysterbay then narudi salenda...sasa kwa daraja hili ina maana nitainyoosha moja kwa moja via daraja jipya...ebu tuacheni jamani...mbona kigamboni wana kivuko wana njia ya kongowe na still walipewa daraja??
Hawa watu wa ajabu sana. Hawajui watu wa mbezi,kunduchi,tegeta wanaingia msasani kutokea kenyata kukwepa foleni.

Ndio yale yale mtu anakaa Kivule huko anapinga daraja la kigamboni.
 
Tunataka pia ujenzi wa daraja la kuToka dar mpaka zenji

Ova
 
fly over ya TAZARA ni kwa ajili ya wanaokwenda AirPort. Gongolamboto wameponea hapo. WaMandela rd wataendelea kulia na pini ya Buguruni mataa. Uliangalia kwa jicho la 3 hii Miradi ina UKAKASI
Sasa Buguruni mataa si anakaa traffic police ambae anatoa priority kwa highway(mandela road). Mbona hili halihitaji hata jicho la pili?
 
Hawa watu wa ajabu sana. Hawajui watu wa mbezi,kunduchi,tegeta wanaingia msasani kutokea kenyata kukwepa foleni.

Ndio yale yale mtu anakaa Kivule huko anapinga daraja la kigamboni.
Kwahiyo kupinga au kukubali kitu lazima uwe unaishi maeneo hayo, mbona mimi naishi Mikocheni na bado napinga ujenzi wa hili daraja.
 
Kwa macho ya kawaida unaweza kufikiri lengo la daraja hili ni kupunguza foleni ya Salender Bridge na kuwaondolea wananchi wa Dar kero ya foleni. La hasha daraja hili linalojengwa kwa gharama kubwa halitapunguza foleni kwa sababu watakaotumia daraja hili ni watu wachache sana, (under utilised bridge).

Ukiangalia kwa jicho la tatu, lengo hasa ni kuwasaidia viongozi, mabalozi na wazungu wachache wanaoishi maeneo ya Osterbay na Masaki ambao hawazidi hata 200, labda wasikae kwenye foleni kwa muda mrefu wakichanganyika na walalahoi wa maeneo ya Mwenge, Kawe, Kunduchi, Tegeta, Boko na Bunju.

USHAURI: Kama lengo ni kupunguza foleni ya Salender Bridge ingefaa zaidi lijengwe daraja kubwa la nchi kavu kutokea maeneo ya Hananasifu au Magomeni hadi Muhimbili au Fire kuvuka bonde la Jangwani linalojaa maji kipindi cha mvua.

Daraja hili la Hananasifu - Muhimbili/Fire, lingehudumia watu wengi hasa wafanyabiashara wa Kariakoo na katikati ya jiji, ambulance, zimamoto na wafanyakazi wa kada za chini ambao ndio walio wengi, tofauti na daraja la Aga Khan - Coco beach ambalo litahudumia 'sana sana' wakazi wa Masaki na pengine kubaki 'idle' kwa kipindi kirefu.

Daraja kubwa la Jangwani si tu lingepunguza adha ya foleni ya Magomeni-Kariakoo/Posta lakini pia lingesaidia kupunguza magari yanayopita Salender Bridge.

Anyways kupanga ni kuchagua, tumechagua daraja la Coco beach kwa wadosi tukawaacha wa Mbagala wahangaike na foleni yao.

Ni ushauri na mawazo huru ya MwanaJF mzoefu Quinine.

Umeongea mengi weeee...ni kuwa sina muda wa kuandika deep analyisis ya hilo daraja, ni kuwa halitakiwi!, chochote mtu yeyote atakachoongea ni ku make justification tu. Halitakiwi kwa sasa na tena ukizingatia mji unahamia Dodoma!!
 
Kwahiyo kupinga au kukubali kitu lazima uwe unaishi maeneo hayo, mbona mimi naishi Mikocheni na bado napinga ujenzi wa hili daraja.
Unaweza tu kuamua kupinga hata ukiwa unajua reality. Ila ambaye hata hajui adha ya wakazi akipinga anashangaza na bongo hii aina hio ndio wengi.
 
Mpwa nakafahamu kale ka njia, ule ni uchochoro, hautapunguza foleni popote pale
Sasa wale wakazi wa maeneo yale wakae mkao wa kupokea tinga tinga litalobomoa makazi yao. Haitawezekana lijengwe daraja kubwa/refu vile halafu tributaries zibaki pale pale.
 
Sasa wale wakazi wa maeneo yale wakae mkao wa kupokea tinga tinga litalobomoa makazi yao. Haitawezekana lijengwe daraja kubwa/refu vile halafu tributaries zibaki pale pale.
Maumivu lazima mzee baba

Ova
 
Mkuu Quinine; kiongozi ambaye hajui aendako kwake kila njia ni njia..!!
Hii movie ndo kwanza imeanza..!!
 
Back
Top Bottom