Sipati ajira, sioni faida ya elimu yangu, naona bora kuuza vyeti

Hili la kuuza vyeti lipo, hata mimi jamaa mmoja alitaka nimuuzie cheti cha sekondari kwa laki mbili tu, nikaona bora viozee sandukuni kuliko kuuza kumbukumbu yangu kwa gharama yeyote
 
Nasubiri vya ubatizo.
Kuna wakati nilipata ajira serikalini ila sikuwa na cheti cha kuzaliwa walichokuwa wanataka pia. Ili nipate cheti cha kuzaliwa ilitakiwa niwe na kadi ya kliniki au cheti cha ubatizo, nikaambiwa niende kanisa mmoja wanatoa vyeti vya ubatizo. Kufika kule niliulizwa nitaje mchungaji aliyenibatiza nikapatwa na kigugumizi, kwanza sikuwa mshirika wa kanisa hilo na wachungaji wao siwajui. Ilibidi niondoke tu niende hospitalini kujaziwa kadi ya kliniki ili nikapate cheti cha kuzaliwa nikamilishe vielelezo vya kuajiriwa. Kwa hiyo hata vyeti vya ubatizo ni vigumu kuvipata
 
Cha kifo unacho.....???
Hivi wale tbc1 tangazo la shukrani huwa wanadai cheti cha kifo ndio warushe hewani picha ya marehemu au wanawaamini sana wateja wao? Ukute mtu kapeleka tangazo la kifo kumbe anayetangazwa ni mzima
 
Kwa vyovyote vile umesomea SUA kuwa mvumilivu . Zikitoka Ajira za ualimu omba walimu wa agriculture na biology. Ukipata Ajira njoo nikuunganishe unafanyiwa recategorization unakuwa afisa kilimo au mifugo or etc
 

Cku hizi elimu co dili.
 
Sijui una mda gani baada yakumaliza chuo! Kuna mshikaji wangu ana CPA plus MBA Mzumbe! 2019 Lakini hana kazi! Anapiga story kwenye vijiwe nakuomba omba hela za kula! MBA plus CPA alisomeshwa na kaka yake,enzi za miaka ya 2018 akavuta!!
mi 2012. Nishaa give up kuwa mtumishi wa serikal, kibaya nimesoma kwa tabu ningejua niachie kidato cha nne niwahi mambo mengine mtaani huenda ningekua mbali kuliko nilipo sahizi.
 
Wacha kuwa mjinga bro kwani lazima uajiriwe fanya kazi zako binafsi utaona raha tu hiyo elimu yako weka pembeni .
Nishaa uacha ujinga tayar, sahizi nalima pia nakomaa na boda boda mjini.
 
Ukikosa mteja kabisa njoo in-box
 
Ukikosa mteja kabisa njoo in-box
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…