Sipati ajira, sioni faida ya elimu yangu, naona bora kuuza vyeti

Sipati ajira, sioni faida ya elimu yangu, naona bora kuuza vyeti

Hayo mawazo potofu,Kama hivyo vyeti havijakusaidia wewe unafikiri huyo atakayevinunua vitamsaidia nini? Halafu hiyo milioni kumi na nane inatoka tu kirahisu rahisi? Sema uko wapi tuone unafanyaje ili utoke.Usidharau elimu,elimu siyo vyeti Ni maarifa uliyoyapata.
Wapo wana faidika, kina bashite umesahau?
 
Kichwa cha uzi chahusika, Kwa wale wenye uhitaji wa vyeti mimi ninavyo.

Nitakuuzia vyeti vyote kuanzia sekondar mpaka chuo ili visikusumbue kwenye matumizi yako.

Sifa ya vyeti

O-level kina masomo 10 hakina F
A-level matatu (comb CBA) hakina F zaidi ya Bam
Degree ya Sua na Post graduate diploma in Education Teaching, chuo St. John.

Bei ya vyeti vyote ni tsh 18,000,000
Tutawasiliana Pm mpaka tuonane nikukabidh mzigo nawe unipe hiyo pesa.
Hii ni baada ya kuona naenda off target na mahitaji ya serikali yangu kwa soko la ajira.
Kwa sasa napatikana Rufiji njoo tufanye biashara.
Kama ulisoma uajiriwe hukutakiwa kabisa kwenda shule.
 
Sasa kitu hakina faida, halafu unauza bei juu. Hiyo m18 hata ujiuze mwenyewe watu hawawezi kukununua acha hayo makaratasi
 
Kichwa cha uzi chahusika, Kwa wale wenye uhitaji wa vyeti mimi ninavyo.

Nitakuuzia vyeti vyote kuanzia sekondar mpaka chuo ili visikusumbue kwenye matumizi yako.

Sifa ya vyeti
O-level kina masomo 10 hakina F
A-level matatu (comb CBA) hakina F zaidi ya Bam
Degree ya Sua na Post graduate diploma in Education Teaching, chuo St. John.

Bei ya vyeti vyote ni tsh 18,000,000
Tutawasiliana Pm mpaka tuonane nikukabidh mzigo nawe unipe hiyo pesa.
Hii ni baada ya kuona naenda off target na mahitaji ya serikali yangu kwa soko la ajira.
Kwa sasa napatikana Rufiji njoo tufanye biashara.
Wacha kuwa mjinga bro kwani lazima uajiriwe fanya kazi zako binafsi utaona raha tu hiyo elimu yako weka pembeni .
 
Vyeti vina picha yako huwezi kumuuzia mtu, labda viwe vya zamani kabla ya mfumo wa kuweka picha kuanza
 
Back
Top Bottom