Sipati Picha Kama Hili La Wachezaji Wa Singida BS Kupewa Uraia, Kama Rais Angekuwa Magufuli?

Huyu Kibu Denis siku za mwanzo anavaa uzi wa Taifa Stars si baadhi yenu mlikuwa mnamuita Mcongoman?

Kwanini mnapenda kuwakatia watu tamaa mapema? Kwanini mnapenda kuangalia hatua moja mbele na sio mia moja?
 
Umezingumzia kuwa US unaweza pata uraia ndani ya siku 1, mimi nimekwambia hilo jambo si kweli. Hakuna nilipomtaja Rais wala Tanzania.
 
Na yule raia wa Mali aliyemuokoa mtoto kwenye lile ghorofa na kupewa uraia pamoja na kazi katika jeshi la Zimamoto alitumia muda gani?

Huamini kama kwenye baadhi ya scenerio kuna exceptions?
Well,ihawa wachezaji hakuna exception yoyote! Ni magarasa tupu.

Lengo la kuwapa uraia ni timu kukwepa kanuni ya idadi ya wachezaji wa kigeni.

UHAKIKA:Wakitemwa leo,wanarudi kwenye nchi zao na kuendelea na uraia wa awali.

Mamoudou Gassam aliombwa mpaka na rais wa nchi yake Mali arudi nyumbani aandikishwe jeshini.

Hayo magarasa hata timu yetu ya taifa hawatoitwa labda vimemo vitembee na huko.
 
Hii nchi imejaa watunga sera wasioeleweka. Miaka ishirini na tatu iliyopita nilitoa ushauri Uhamiaji kuhusu kuwatumia wageni wenye elimu ya juu walioko kihalali nchini waajiriwe au wapewe mikataba ya kufanya kazi kwenye Idara na Wizara ambazo tuna uhitaji wa watumishi wazawa. Miaka hiyo nchi ilikuwa na upungufu wa waalimu hadi kufikia kuanzisha shule za kata.
Leo nimesikia buruji likinadi uhalali wa wachezaji wa kigeni kupewa uraia kwa sababu tu ni wazuri katika kucheza mpira. Najiuliza na kutafakari bila majibu, huu mpira wetu ambao umehodhiwa na Yanga na Simba usioleta matokeo chanya kwenye timu ya Taifa, ni muhimu kiasi cha kutoa uraia kwa wachezaji hao wakati kuna waalimu, waganga kadhaa ambao wangetusaidia kazi kwenye hizo fani pale ambapo sisi hatuwezi kufikia? 🤔
 
Wachezaji wenyewe hata hawawezi kupata namba kwenye timu ya Taifa ni wa kawaida saana!
 
Hii ni ajabu mkuu, tupo kwenye nchi ya maajabu
 
Kukosekana kwa elimu ya uraia ni moja ya vikwazo vikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu. Hiki kilichoandikwa hapa ni kiashiria cha wananchi kutokujua wajibu na haki zao kama raia
Kweli bdo tuna safari ndefu mkuu, kuwaelimisha watu kama hawa mwenye hii karne!
 
Yaani uraia wa nchi yetu unagawiwa kama njugu za kuonja, kweli Samia amejua kuichezea nchi yetu.
Ila nyumbu!! Natamani jf ingekuwa inaweka sura halisi za watu Ili tuone nyusi za hawa nyumbu wasio na akili zinavyochujuka na kuhangaika kwa wivu wenye mateso makali kwao. Mama Samia anawatesa aisee hawa viumbe si mchezo.
 
Naiona Kama ni skendo inayo hitaji kutazamwa vizuri, watu tayari wangekuwa wamesha tumbuliwa, kuanzia Mawaziri hadi Makatibu, sasa hivi kungekuwa kumesha changamka muuuuda! Mtu ana wiki 2 Bongo kupewa uraia, hiiiii!
Alisema atakumbukwa hata akiwa hayupo.
 
Kwanini wapewe uraia, tumekosa vijana wanaweza kucheza mpaka tutafute mamluki nje ya nchi?

Je unadhani Mtanzania kwenye hizo nchi wanaweza kupewa uraia kwa kucheza mpira?
 
Botswana tu hapo kuna madaktari wetu bingwa kibao wamepewa uraia.

Sheria zipo ila exceptions pia zipo.

Hao madaktari waliohamia Botswana wamepewa ndani ya wiki 2 ????

Hakuna nchi inagawa uraia kama njugu.

Citizenship is bedrock of our identity.
 
Waarabu wanawapa uraia wanariadha pamoja na zaidi ya dola milioni 1 cash (USD 1M). Na hupata ajira za kudumu hasa kwenye majeshi ya hizo nchi. Wakenya wengi wamechangamkia fursa. Kuna watanzania wachache pia ni wanariadha kupitia jeshl la Qatar. Majina pia wameshabadilisha.
 
Ila nyumbu!! Natamani jf ingekuwa inaweka sura halisi za watu Ili tuone nyusi za hawa nyumbu wasio na akili zinavyochujuka na kuhangaika kwa wivu wenye mateso makali kwao. Mama Samia anawatesa aisee hawa viumbe si mchezo.
Anza kuweka sura yako tukuone chawa wa Samia
 
Mtu wa intelijensia aje atupe muongozo wa madhara ya kuwapa hao wachezaji uraia! Madhara kwanzia ma'5

Kwa faida ya wengi
Mpumbavu kama wewe huna hata haja ya kujibiwa... Yabayotokea Marekani Sasa hivi ilikuwa ni sera za democrats kuweka mianya ya illegal immigrants kuingia Kwa wingi na kuhatarisha maisha ya wamarekani. Kama hujui madhara ya watu kuwa raia wa nchi yako bila kuwafanyia enough vetting wewe ni mpumbavu hupaswi hata kuelimishwa


Ukienda Burundi wamejaa na kadi za kupigia kura za Tanzania na wana kadi za Ccm wanasema Tanzania ukiwa na hizo kadi husumbuliwi. Watu wanamiliki ardhi chanika na maeneo mengi ya nchi kinyume na Sheria.


Kuna wageni wengi wanamiliki ardhi bila vibali.
 
Tutoleeni upumbavu wenu sijui mnatumia viungo Gani kufikiri.


Issue ni Wachezaji wanne Tena hawajafanya lolote kwenye mpira kusema wanastahili kupewa uraia.


Kama huo uraia angepewa chama, Mayele, Aziz Ki tungekuwa na sababu za kuwatetea kwasababu wameshafanya makubwa kwenye mpira.


Ila mtu mzima kama wewe kutetea upumbavu kama huu ni kuonesha hii nchi hata wazee kama nyie ni mizigo.


Ndio maana hii nchi kuendelea ni Hadi wapumbavu pumbavu kama wewe waende mbinguni kije kizazi kingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…