Sipendi na sitaki ukaribu wala shobo na wanawake wenye vijitabia vya feminism

Sipendi na sitaki ukaribu wala shobo na wanawake wenye vijitabia vya feminism

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,113
Reaction score
6,251
Peace be upon you all.

Nimekuja kugundua wanawake wenye vijitabia vya ufeminism sina muda wala sitaki shobo nao hata punje.

Binafsi ni mwanaume ninaeamini katika jinsia tofauti zenye majukumu tofauti, yani mwanaume ni mwanaume na nafasi yake haiwezi kuchanganywa na mwanamke hali kadhalika mwanamke ni mwanamke na nafasi yake kamwe haiwezi kulinganishwa au kusindanishwa na mwanaume.

Nikisikia tu mwanamke analeta mind set za haki sawa bla bla bla hata kama ni ndugu taratiibu namuondoa katika kundi la watu ninaowasiliana nao. Nawaona kama madume jike na nakosa positive vibes kabisa kwa hawa viumbe, watanisamehe tu.

Kinyume chake nimekuwa navutiwa sana na wanamake wanaoikubali nafasi yao kama wanawake, hawajishindanishi wala kujilinganisha na wanaume. Nakiri wazi nawapenda sana wanawake hawa Mungu awape mairha marefu.

Hali hi ya kutotaka ukaribu na "masupawuman" imenisababisha kuwaweka kando wanawake wengi na kuonekana naringa na sina time ya kuwaeleza kwanini nimewaweka kando kwasababu siwezi hata kuongea na wanawake mafeminists naona napoteza muda wangu kwa viumbe wanaofake mambo, limbukeni na wajinga wa utandawazi.
 
Napenda mwanamke anayetambua nafasi yake, napenda zaidi yule mwenye elimu japo kidogo asiwe mbumbumbu halafu awe na tako, kiukweli napenda sana mwanamke anayejua kudeka na anayenipa muda wowote ntakapotaka, kiufupi tu kwangu mimi mwanamke ni starehe yangu.

Mungu awape maisha marefu popote mlipo
 
Nilichogundua.. Jamii forums ina misogynists wengi sana. (You’ll need to google the term).

Mwanaume ambae anajiamini hatetereshwi na confidence ya mwanamke. Only inferiors feel intimidated by a woman’s confidence.

Yani unataka ukifika mahali kila msichana ainame kama kaingia mfalme? Ama?

Punguzeni inferiority complex automatically mtaacha kuchukia wanawake wanaojitambua. Hivi haki sawa kwani ni kwenye kuosha vyombo? Si ni fursa za kimaendeleo ama?

Wewe kamata kishoia wako wa ku bow down and stop downgrading women. Jiamini bro.!

Yani mada za humu utakuta ni wanaandamwa wanawake as if ni viumbe ambao hawaja wazaa? Like seriously mna shida kubwa kichwani. Mwanaume mwenye pesa na confidence zake haogopi mwanamke challenging. Ila inaeleweka mkikua mtaacha uoga😅
 
Back
Top Bottom