Ahaaaa embu kwana nicheke maana nina ka shoga kangu ka marekani kalikuja juma mosi kwangu kameondoka jana ila nimekoma yaani hawa watu vyakula vyao nadhani viko hotel kubwa.
Juma mosi usiku saa 5 kananipigia kanataka kuja kulala kwangu kako bored kwakwe hakajui kiswahili hakana wa kuongea nae kana jua "mambo" tu so kakaj kwangu.
Usiku huo mimi nilipika ndizi ahaaaaa kwani kalikula? Kakanywa chai tukalala.
Asubuhi nawaza nikapikie nini? Nikawaza mayai, kweli kalikula mayai na chai chai yenyewe hata kikombe hakawezi maliza.
Mchana nikakapikia chips, kakadono🤣
Mimi nikajipikia ugali tukala na shoga yangu mwingine, ahaaaa ndo kanauliza " Luckyline what kind of food is this? 😅 kanashangaa kweli kananisimulia marekani wengi hawaopiki wanachukua vyakula ambavyo viko tiyari na wanakula junk foods mara nyingi.
Hapo nilimuita shoga yangu aje nina mgeni basi kila kitu janashangaa na kuuliza kakasema kenyewe kanakula hotelin almost every day.
All in all nimefurahi kuwa nae tumeenjoy ila kumbe ni kazi kiasi hiki kuongea kiingereza siku mbili mfululizo? Yesuuuuuu nyie.🤣
Shoga yangu alivyokuja kukasalimia nikaona ananiangalia mashavu nikamuuliza vip? Ati hujavimba? Unawezaje kuongea na huyu kiunbe ambae hajui kiswahili.
Kuna wakati niliwaacha nikaenda dukani kufata soda mara shoga akanitumia sms " shoga wahi ubaki na mzungu wako mimi hii lugha nakaaga nayo mbali" nyie🤣
Kwa bongo hii tumejizoea kuongea kiswahili na viluga vyetu huko kijiji tukipiga simu lisaa tunaongea kiluga leo mtu anakuongelesha kimarikia siku mbili sio mchezo.
Mkiona mtu siku nzima huko ofisin anaongea kiingereza msimchukulie poa mpeni heshima zake. sio rahis kama mnavyo dhani.
Kuna rafiki yangu ni mbongo yeye halagi ugali anasema ugali ni chakula cha nguruwe. Anakula wali jan-dec