Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Inategemea unatafuta ajira huku umesimama wapi,Kama Bado unakula na kulala nyumbani,na wazee wapo vzr, hapo hakuna shaka, lakini Kama wazee ni choka mbaya, na ulikuwa umepanga chumba,hata 400K,utachukua,la msingi hapa, utaendeshaje maisha bila kipato, ni ama, unasadiwa na wazazi/upo nyumbani, au mpenzi anakupiga tafu, lakini Kama huna vyote hivyo, mazeee,unaweza kwenda kuwa mlinzi wa SGA,
 

Usidharau kazi kazi ni kazi tu
 
Una degree unaleta mashauzi wakati wife ana CPA na anaosha vyombo home 😁😁😁! Kenge wewe
 
wenzako wana masters na wanatafuta kazi za kulipwa laki 2 na nusu. Kupanga ni kuchagua.
 
We bado ni kijana hujui kuhusu maisha na bado unaakili za chuo
Yani hivi nisome nimalze niende chuo nikimalza chuo nipate kazi nijenge Nyumba nzuri nioe MKE mzuri niwe na magari zaidi ya matatu niwe nawatoto.

NB:
Ndugu maisha hayapo kwenye system Kama unayofkria wewe na hakuna formula ya maisha inayoeleweka ama kuzoeleka Haya nakuacha utakuja huamini nachokwambia
 
Sikuona DP πŸ˜πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜˜ kwa hilo body ukiwa mjanja humalizi miezi 6 utakuwa kitengo mahala salama. Hakikisha unajisogeza kwa mameneja wa bank mjini na pia jiingize katika shughuli za kichama pia huenda ukapewa ukuu wa wilaya flani.
 
Wajuba,,

Tunazika Au Tunasafirisha,!?[emoji1745]
 
Kuna watu elimu zenu za ajabu kabisa!!

Hivi unashindwa hata kutumia akili yako kujifunza na kuelewa uhalisia wa mambo kupitia ajira za walimu? Unafikiri hao walimu ni wajinga kulilia ajira za serikali? Then unapata nafasi ya kulipwa such amount of money unaanzisha uzi ? You're not serious, kama unaona kwako ni ndogo ni heri ukae kimya na kuishia kujadili vijiweni na wenzio wenye akili sawa na zako,

Maneno ya kuandika yanauma mno kuliko ya kusemwa, uzi wako humu ni mwendelezo wa maumivu kwa wanaohangaika kupata hata ajira zenye mishahara ya laki mbili then you are talking about one milion? Uko serious kweli?


USIONYESHE FURAHA KWA WENYE MAJONZI, USIONYESHE PESA ZAKO KWA WASIO NA PESA, USIJITAMBE KUWA NA WAZAZI MBELE YA YATIMA



Maisha yangekuwa kama tunavyofikiri, basi tusingeona utamu wa maisha, ujumbe wako hapa unaumiza sana na kuonyesha kejeli kubwa kwa wasio na ajira.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hahahahahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…