Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nakumbuka 2014 namaliza chuo nikawa na mawazo kama haya. Aunt yangu ni HR benki moja hivi pale HQ. Akanambia nianze na salary ya laki 4. Nikasema mnanionaje[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]
Nikakataa jaman. Just on my graduu day ukumbini. Basi bwana, nikakaa miaka miwili nyumbani. Loh, sindo nikaanza ona uhalisia? Ntie nyie nyiee[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Utakua unakaa kwenu au kwa shemeji yako, ukiwa mkubwa ukakaa kwako hiyo hela utaichukua tu,kuna watu wanachukua 300,000 wako hapa unakuja kuwatukana na kuwakejeli?
Mimi wakati naanza kazi mwezi wa pili mwaka huu boss alinitajia mshahara wa laki 3 kwa mwezi lakini mbali na hapo ilitakiwa nifanye probation kwa miezi mitatu huku nikilipwa nusu ya pesa yani laki moja na nusu, baada ya kumaliza interview na kunitajia hiyo offer yao boss akaniambia nenda kafikirie halafu unipe jibu.

Nikafikiria sana ila nikaona ngoja nikomae nikakomaa miezi mitatu ikaisha ile nianze kupokea laki 3 sasa kama mshahara baada ya probation boss akaniambia kuanzia mwezi huu nitakulipa laki 4 baada ya miezi miwili akaniongezea tena laki moja nyingne nikawa nalipwa laki 5 mwezi November kaniongezea tena sasa nalipwa laki 6.

Acha kudharau kazi mkuu mtaani maisha ni magumu sana labda kama wewe ni mtoto wa kigogo sawa.
 
Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
Kwa kozi uliyosomea ni halali kabisa huo mshahara
 
Hajui ugumu wa mtaani huyu, wahitimu wengi hua na matumaini makubwa sana kuliko uhalisia na ndio maana wanapata msongo wa mawazo,
Kipindi hicho namaliza chuo rafiki yangu mmoja alisema bila 2m take home hafanyi kazi, ajabu zaidi alianza na laki 8 kwa mchina.
Duuuhh
 
Kulingana na kazi yangu kama mlinzi wa taasisi moja ya serikali sometimes nakuwa dereva, sometimes nakuwa receptionist and so.

Wahitimu wa shahada ya kwanza wanaokuja kuomba kazi ya usafi kazini ni wengi sana. Sasa sijui ni ugumu wa maisha au wanatafuta connection tu!
Sipingani na mawazo yako ila ngoja nikuambie kitu.

Mimi niliwahi kukataa kazi ya police, jeshi na nilikataa kusomea ualimu.
Maisha yalinitandika mpaka nikanyoosha mikono.

Imagine sasa Mimi ni mlinzi , ningekuwa mjeshi sasa tayari ningekuwa na nyota 3.
Huku niliko nalipwa vizuri tu. Nimejenga, nina gari ya kutembelea lakini naichukia title hii ya "Mlinzi". Hata ujasiri wa kutaja kazi yangu mbele za umma sina
we mlinzi acha kuona jau kuitwa hivyo. mbona... 😆😆😆 dah! imenbidi nicheke tu hehehehehh! sema jau kisenge yaan 😂😂😂
 
Mie ni muhitimu wa degree ya kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
Wapo vijana wenye degree kama hiyo yako, wakaenda UK wakafanya ACCA walipo rejea wakaanza na gross salary ya sh. 325,000. Nenda kafanye kazi, taratibu utapanda na kufikia hiyo milioni
 
Kwa msoto huu wa ajira kwa degree holders; inafika time hata ukipata kazi ya ukondakta basi la mbagala- makumbusho unashukuru Mungu!!
 
Uzi huu unaonyesha jinsi Watanzania walivyokata tamaa. Yaani hakuna mtu mwenye ambition. Wote ni magoigoi tu. Chochote sawa tu. CCM itaendelea kuiba chaguzi inavyopenda, na sisi tutaendelea kulala tu kwa attitude za aina hii!

Majumba saba - kupanga ni kuchagua. Kila kitu kinawezekana. Nimefurahi kusikia kuwa una mpango wa kutoa kilicho cha Mungu katika mapato yako. Mungu atakubariki. Thamani yako unaijua wewe. Lakh 2.5 kwa mwezi ni nauli ya kwenda kazini na kurudi nyumbani tu hakuna kitu kitabaki.
mkuu sisi vijana wa kitanzania sijui tumepatwa na nini?
 
Mie ni muhitimu wa degree ya kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
fanya
 
Mimi wakati naanza kazi mwezi wa pili mwaka huu boss alinitajia mshahara wa laki 3 kwa mwezi lakini mbali na hapo ilitakiwa nifanye probation kwa miezi mitatu huku nikilipwa nusu ya pesa yani laki moja na nusu, baada ya kumaliza interview na kunitajia hiyo offer yao boss akaniambia nenda kafikirie halafu unipe jibu.

Nikafikiria sana ila nikaona ngoja nikomae nikakomaa miezi mitatu ikaisha ile nianze kupokea laki 3 sasa kama mshahara baada ya probation boss akaniambia kuanzia mwezi huu nitakulipa laki 4 baada ya miezi miwili akaniongezea tena laki moja nyingne nikawa nalipwa laki 5 mwezi November kaniongezea tena sasa nalipwa laki 6.

Acha kudharau kazi mkuu mtaani maisha ni magumu sana labda kama wewe ni mtoto wa kigogo sawa.
daah maboss wa kibongo jau sana, inaonekana boss wako anatabia za kizungu.
 
Back
Top Bottom