Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Get off your high horse of GPA ma'aam. Your employee gets nothing off your GPA. The value you add to the business is what matters.

Unaweza kulipwa hata mil 20 kama unastahili.
Anyway nitapenda kusikia maoni yako 2030. Hope utakuwa sober by then!
 
Mkuu kuliko zile pisi ambazo wako vitengo vya sales kwenye makampuni makubwa mfano tigo, airtel, cocacola wanaotembeza vipeperushi africana, tangibovu, mwenge, makumbusho

Kuliko zile pisi ambazo zinapiga graduate trainee program crdb, nmb, tib tena hawa ndio wako smart nama gpa makubwa kutoka udbs ifm +cpa na wanapata tu posho, tena crdb unapiga kwa miezi 36 ukimaliza ndio wakufikirie ajira

Kuliko wale shombe shombe ambao wako kkoo wanaokaribisha wateja kwenye maduka naelimu zao wameweka pembeni

Bora hata ingekuwa kozi ya maana, hiyo ambayo anaweza kuwa replaced na malaki ya wahitimu huku mtaani asilimia 90 ya vyuo vyote wanatoa Bcom

Yaani sijui wale jamaa wa ifm, cbe,tia ,udbs ,institute of accountancy government huwa inawapeleka wapi[emoji22][emoji22] bora hata wanaosoma ba education
36 months?

Kweli watu Wanakaza[emoji848]
 
Hahaha kwani kuna aliyekulazimisha uchukue pesa yoyote?!

Subiria ukue utoke kwa baba na mama utachukua hata mia mbili.

Haya maisha na degree hata hawana uhusiano wowote.

Bank zenyewe zinafungwa, technologia inashika kasi wewe unaongelea GPA zetu hizi?!
 
Kulingana na kazi yangu kama mlinzi wa taasisi moja ya serikali sometimes nakuwa dereva, sometimes nakuwa receptionist and so.
Wahitimu wa shahada ya kwanza wanaokuja kuomba kazi ya usafi kazini ni wengi sana. Sasa sijui ni ugumu wa maisha au wanatafuta connection tu!
Sipingani na mawazo yako ila ngoja nikuambie kitu.
Mimi niliwahi kukataa kazi ya police, jeshi na nilikataa kusomea ualimu.
Maisha yalinitandika mpaka nikanyoosha mikono.
Imagine sasa Mimi ni mlinzi , ningekuwa mjeshi sasa tayari ningekuwa na nyota 3.
Huku niliko nalipwa vizuri tu. Nimejenga, nina gari ya kutembelea lakini naichukia title hii ya "Mlinzi". Hata ujasiri wa kutaja kazi yangu mbele za umma sina
Mkuu jiite tu "Security Officer"
 
Muda utafika na utaitamani ya laki 3, so karibu duniani ambako kuna degree za kutosha tena zenye uzoefu na kazi hazina.
But unahitaji kupitia Mateso kwa miaka isiyopungua 3 tu! Baada ya hapo utaitamani ajira ya hiyo laki 3.
 
Nafikiri tumuacheni kwanza. Kuna muda haya mambo ni kama hayana formula.
 
Tukwambie ukweli au tukuache [emoji1787][emoji1787]
Ngoja tumuache tu [emoji16][emoji16][emoji16] kuna mwenzie juzi kaenda kilingeni kwa Mshana Jr kuroga analalamika kwamba ana mwaka wa 4 tangu amalize chuo hajapata Ajira
 
Attitude is like a price tag. It shows how valuable you are (Anonymous).
**Kwa attitude hii, hutoboi. Endelea kuangalia tamthilia Hapo kwa shemeji.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Over my Dead body Kama huyo wa kwenye Avatar ndio wewe walah hicho kiuno na kalio utapata hata 2M take home, we tembea tembea tu utapata!!!
Daahh ile avatar simchezo [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]

Out of topic kuna bimkubwa katokq kunionyesha picha ya binti yake masaa 2 yaliyopita aisee nusura mate yanitoke mbele yake ... aisee duniani kuna warembo nyie acheni tu
 
36 months?

Kweli watu Wanakaza[emoji848]
Ndio mkuu crdb miaka 3 ..tena haya mabank yana graduates wakutosha mpaka basi wanakuja na gia ya training programme malipo ni posho na ahadi ya ajira ukifaulu vizuri

Ukisikia wametangaza ajira, ukisoma tangazo unakuta wanataka relationship manager [emoji23][emoji23] experience miaka 10 ndio atajua hajui

Tena crdb wamekuja na program ya kuwafungulia acc wafanya biashara wadogo mama ntilie, machinga, bodaboda unakuta hao graduates ndio wanazunguka mtaa kwa mtaa wanafanya hizo kazi.

Halafu dada yetu hapo hana hata experience, cpa, hatambuliki na bodi ya wahasibu analete maringo
 
Ndugu, Bora ningepata hio laki nane, fursa nyingi napata microfinance, na wanataka niwe tayari kuanza na shilingi laki tatu na nusu. Sasa nawaza, maisha ndio yatakuaje? Hio Nile, nipange, niende saloon, nitoe sadaka kha
Nyinyi watoto wa shule
Kitu hamjui kampuni nyingi hazitaki kuajiri mtu ambae hajui kazi. Hivyo vi GPA vyako hawaviangalii. Uzoefu kazini.

Nausitegemee kuwa utapata nafasi yajuubila experience
 
Mie ni muhitimu wa degree ya kwanza ya Banking na Finance mwaka huu wa 2020 na nimepata GPA kubwa. Kinachonishtua ni ofa zinazo patikana ni mishahara kiduchu mno!

Kiukweli, over my dead body, sipo tayari kwa ajira ambayo take home yake ni chini ya milioni moja.

Hope zinapatikana bila shaka.
Duh !GPA ya ngapi ? Na je? Unadhani waajiri wanaagalia sana GPA kuliko ujuzi wako? n.k
 
Back
Top Bottom