Sipo tayari kufanya ajira take home chini ya milioni moja

Katika vitu vinawatesa sana undergraduates wengi ni over expectations kwenye salaries.

Nikueleze hv mshahara haujawahi kumtosha yeyote, kinachofanya watumishi wa taasisi mbalimbali kuenjoy maisha ni vile wanavyotengeneza mazingira ya kuwa na pesa nje ya mshahara ambayo nyingi inategemea umejiwekezaje huko nje ya kazi yako.

Kwa sasa utakataa kila aina ya kazi unayopewa offer kwa ku-expect ipo siku utaitiwa offer itakayokutosha, ambayo kimsingi haipo isipokuwa kwa kuotengeneza mwenyewe ukiwa umeanza kazi.

Zinduka mdogo wangu, nguvu ya boom haitokuwepo tena, uncles, ba mdogo, brother na wategemezi wengine inafika point nao wananchoka na kuamini huenda ni mikosi ya wewe kutokupata kazi kumbe mkosi ni wewe mwenyewe!!!
 
How good are you with international financial markets? Specifically the NYSE. Are you very good in computers? I might give you a part time position to help making trades and dealings. Also, how is your English language proficiency? What GPA did you get exactly?
 
Una uzoefu wa muda gani?
 
Wewe mjinga sana.
Nani akutafutie milioni nawe ukale tu.
Zitafute mwenyewe ujilipe, na ukiwa na akili nzuri wweza kujilipa zaidi ya milioni moja , hapo ukiingia biashara halali.
 
Bila shaka upo kwenye migodi ya wa canada
 
Attitude is like a price tag. It shows how valuable you are (Anonymous).
**Kwa attitude hii, hutoboi. Endelea kuangalia tamthilia Hapo kwa shemeji.
Duh ni kweli hawa mashemeji wanawadanganya wadogo zetu, mm nina ndugu wawili wana CPA wamesomea Banking na bado wamekosa kazi toka awamu hiyo iliyopita sasa wanabiashara mitaani ya kuuza vyombo na madawa ya wadudu sijui km wanapata hiyo milioni kwa mwezi.
Mm nashukuru nina vibanda nakodisha wafanyabiashara wananipa mara3 ya huo mshahara anaoutaka NILIKATAA KABISA KUAJIRIWA NA BINADAMU MWENZANGU saa moja afajiri mpaka saa 10 uwe kwake
vijana wamalizao masomo waache ndoto za ajira km hawana g/father haya mabenki kila siku yanakufa
 
Umesoma nje ya nchi Je? Na je? Kama umesoma nje ya nchi Nitafute
 
Kadegree kenyewe ni ka pale jalalani..unathani atakua anajua maana NYSE?
 
Ha ha ha nilipigaga sehemu nikaanza na laki mbili akasema ataongeza kaja kuongeza baada ya miezi mitatu ikawa laki mbili na 50 nikakomaa hapo 2 years waapi nkasepa
angekuua huyo mbwa sio boss kabisa
 
Hawa wanachuo shemeji zao waliopita bila kupingwa Wana matarajio makubwa kuliko Hali halisi.
Maliza chuo uje field nikusaidie kubadili soli
 
Leo ni 2020 miaka sita mbele; mshahara ungekuwa umepanda, una uzoefu, ungekuwa umetengeneza connection za kutosha.
 
Umenigusa Sanaa mkuu huyu ana wazazi ,ndugu wanajiweza na wanaweza kumsupport ,ilaaa akumbuke hawataishi milele na pia kuna magonjwa n.k wanaweza filisika .

Nakumbuka nilipokwenda kuanza form one shule moja ya bweni mm ndo nilikuwa na ahueni ya maisha kwahyo nilijiona kama nimebalikiwi hivi sababu pesa home ilikuwa sio shidaaa ,ilaa mzee alipokufa ghafla bila kuumwa ndo nikaona nyota nyota mpaka Leo akil yangu huwa haiamini kama ilifika kipind nikawa napata ada kwa mbinde

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
daah maboss wa kibongo jau sana, inaonekana boss wako anatabia za kizungu.
Ukweli ni kwamba hakuna boss ata risk kuchukua fresh graduate Bongo amlipe kiasi hiki. Waajiri ndio wanajua gharama na hasara za hii kitu. Kama hujawahi kuwa mwajiri hutaelewa.

Huyu jamaa lazima aliongeza thamani sana kwenye biashara. Vinginevyo asingeongezwa zaidi ya kupumzishwa baada ya probation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…