Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Nusu jiniazi anaweza kutueleza kwa kutumia sayansi kipi kilianza kabla ya kingine kati ya usiku na mchana ama jua?

Maana Biblia imeweka wazi, ikawa usiku ikawa mchana vilianza kabla ya jua kuumbwa.
 
Mmh mkuu roho mtakatifu amekujaa kweli kweli
 
Mkuu mimi huwa napuuzia kujibu maswali ya watu wengine sababu wanauliza maswali ya KIJINGA sana. Watu wasioutambua UWEZO wa MUNGU, hao ni wa kuwaacha tu maswali yao ya kijinga jinga.

Mtu anayeuliza swali kama hilo hatambui uwezo wa MUNGU. Hiyo Sayansi anayoizungumzia imewekwa na MUNGU mwenyewe, sisi tumejifunza kile alichokifanya MUNGU kisha tunajiita "Wanasayansi", na kujiona bora kuliko yeye ALIYEUMBA!

Kazi ya uumbaji aliyoifanya BWANA MUNGU ndiyo hiyo wanayojifunza hao wanaojiita "wanasayansi" na mpaka sasa wamejua asilimia 0.99% na kujiona wamepiga maendeleo makubwa wakati bado kuna mengi sana hawayajui na kamwe hawatajua mpaka siku YESU atakaporudi.

  • Mfano, bahari; mpaka leo hii kuna vitu vingi sana vimo baharini na havijulikani.
  • Angani kuna sayari na nyota ambazo hazijulikani.
  • Mwili wa mwanadamu una mengi sana ambayo bado ni fumbo kwa hao wanasayansi.
  • Bara la Antakitika bado ni fumbo kwa wanasayansi.
  • kuna mengi sana ambayo mpaka kesho wanasayansi wanahangaika kuyajua na bado hawajui kitu.
Ifike mahali tukubali kuwa MUNGU yupo na hawezi kulinganishwa na kitu chochote kile, ifike mahali tumpe heshima yake anayostahili BWANA MUNGU.
 
ukitakata uielewe biblia nilazima uwe na nguvu za roho mtakatifu lkn ukisoma kama gazet la mwananchi Au nipashe n.k, hutaelewa na ukitaka ujibiwe hiyo miswali yako kawaulize wapo watu wana Phd za theology watakujb vzr...Kwanza una hoji nini imani za watu? Pambana na hali yko ndugu.......
 
Rafiki, mada yako imejikita kwenye maswali mengi ya kisomi (scholarly), ambayo ndio chakula cha wanazuoni. nadhani kwenye forum hii huwezi kuwaita walete majibu yao yatakuwa magumu kuyaelewa watu wa kawaida (ambao si wanazuoni). mimi nitakupa ushauri mdogo, wewe pamoja na watu ambao mnadhani kunakitu kimefichwa kwenye Biblia: ushauri wangu ni ule Yesu aliwapa wasomi wa wakati wake hapa namnukuu:
Mnayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa ndani yake ninyi mna uzima wa milele; na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima. Yohana 5:39-40

You search the Scriptures because you think that in them you have eternal life; and it is they that bear witness about me, yet you refuse to come to me that you may have life. John 5:39-40

Kwa hiyo kama Yesu alivyosema kilicho cha muhimu kwako ni kupata uzima kwanza, na uzima wa milele ndio huu: "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma". Yohana 17:3.

Ukiisha kumpokea Yesu, ukapata uzima wa milele; mimi nakuhakikishia na ukawa na nia ya kufanya utafiti utapata majibu mazuri ya maswali yako (kama mimi nilivyofanya). kwa hiyo utakuwa na uzima na maarifa pia, ila ukitaka maarifa pasipo uzima haitakuwa na faida kwako utakuwa kama wale waandishi na mafarisayo wa kale ambao walikuwa na elimu kubwa ya Biblia ila hawana uzima na ndio maana walipiga kelele "msulibishe, msulibishe" bila kujua wanamkana bwana wa uzima!

.
 
Wakristo wana vitu vingi hawavijui...mfano suala la roho mtakatifu nashangaa hapo watu wakihojiwa wanasema isome bible kwa uwez wa roho mtakatifu inamaana bible inatakiwa isomwe na walio amin tu sasa nini maana ya neno la Mungu na huyo roho mtakatifu ni nani anafanyaje kazi?....Yesu alisema kwemye yohana 12-14 nina mengi ya kuwa eleza ila hamuwezi kunielewa sasa ila yeye roho mtakatifu atakapo kuja atawaelekeza kwenye kweki yote na atanitukuza mimi..!

Ila ukiwauliza wakristo yesu alisema ana mengi ya kusema ila hamuwez kumuelewa ila huyo atakae kuja ambae wakristo wote wamekubaliana ni roho mtakatifu kuwa atakuja kuwalekeza mengi ambayo hakuyasema yesu...muulize mkristo yoyote jambo gani jipya kawafundisha roho mtakatifu tangu aondoke yesu miaka 2000 iliyopita... Au huyo roho mtakarifu ndio mnaishi nae kwa hisia bila ushahid kuwa anawaongoza na kuanza kuongea lugha za ajabu na kujiongopea eti una nena kwa lugha..na ukisoma maandiko roho mtakatifu alikuwepo hata kabla ya yesu na alikuwepo na yesu kumsadia kazi zake kama ambavyo alifanya na manabii wengine..ukisoma maandiko roho mtakatifu alikuwepo kwenye tumbo la elizabet mariamu alipomuambia ana ujauzito,na pia yesu alifukuza mapepo kwa uwez wa roho mtakatifu....

Lakin pia kwenye maandiko yesu amasema ni bora kwenu mimi nikiondoka kwa nisipoondoka msaidiz hatokuja ( ambaye wakristo mnasema ni roho mtakatifu) yaana sharti la huyo roho mtakatifu kuja ni yesu kuondoka...lakin ukisoma maandiko kama nilivyo onesha hapo juu roho mtakatifu alikuwepo.!


Hebu niambie kwenu nyie wakristo roho mtakatifu ni nani na anafanyaje kazi...maama mmatuchanganya mkiombwa ufafanuzi mnakimbilia kusema umuombe roho mtakatifu akushukie usome biblia na wakati houo biblia hata Yesu mwenyewe haijui hajawai kuiona wala kuitamka ilikuja miaka 300 baada ya yeye kuondoka dunian ina uhusiano gani roho mrakatifu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe mwenyewe ukiandika maneno ya hekima yasio mpinga Kristo wala yasiopingana na maagizo ya Mungu alafu ukayaleta kwetu yakakubalika na imani yetu hapo utakuwa umeongozwa na Roho Mt: Ndio Mambo yalikuw hivo toka mwanzo watu waliokuwa wanayachambua maandiko waliongozwa na Roho Mt; kwahyo Roho Mwenyewe aliwaongoza kuyachambua yale yaliyoyake na yasio yake aliwakataza wasiyachukue......Kwanza kuhusu Biblia Kujipinga hilo sio kweli bali italetwa tafsri ya kupotoka na watu wasio na Roho Mt:

UKWELI KUHUSU BIBLIA:
Biblia Muundo wake Umekaa katika mafundsho ya watu ambao tayari waamini wala haifundishi makafiri wala wasio amini bali imefundsha watu ambao tayari waamini inawakanya watu ambao tayari wamekuwa waamini ...wala hakuna mafundsho ya makafiri humo....hivo ndugu kama unaenda kusoma Biblia ambacho bado wew sio muumini jua umedandia gari kwa mbele ...Biblia yenyewe tu haiwezi kumfanya mtu akaacha ukafiri ila Mhubiri na Roho Mt: Ndio watakaomfanya mtu huyu kuacha ukafiri na kumpokea Yesu Kristo na hivo Sasa Biblia itamhusu Na itaanza kumfundsha jinsi ya kudumu katika Imani. Soma vitabu vingine kama Quran hivo havihitaji hata uwe na Roho wa Mungu ndo uvielewe bali vinahitaji tu utayari wako wa kusoma..

UNAJUA KWANN QURN NA BIBLIA HAZILANDANI?
(Biblia haifundshi makafir wala haiwatishii bali inawafundsha waumini kudumu katika imani ila Qurn inawatshia makafiri na kuwapa uoga ndio wengi wetu leo kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaosali ili wasiende kuchomwa moto wala hawasali katka kweli ya Mungu katik Kumpenda)

Nyaraka za Paulo zimetumwa kwa waumini sio (kwa watu kama nyie)
Injili zimeandika yale mafundsho ya Yesu Alipokuwa Anajenga msingi mpya wa imani na enzi mpya ya utumishi hasa kutoka katika misingi ya Kidini na kuhamia katika misingi ya imani tu!(ambayo enzi hii imeruhusu sisi kupata teknolojia nk🙂 Kitabu cha matendo kimerecord matukio ya mitume wa Yesu walivyomshuhudia Bwana wao alipifufuka na pia hata kuhubir watu kulijaza kanisa(vitabu kama zabur na mithal ni vitabu vilivyo na maneno ya farajakwa waumini (sio kwa watu kama nyie) vitabu vya manabii ni ujumbe wa Mungu kwa Waumini (sio kwa watu kama nyie)

Tuyatambue haya ili ujinga ututoke.
 
SALA NA KAZI SANCTUS ANACLETUS
 
Fuatilia yanayokuhusu ya dini yako. Yetu tuachie wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well and good basi tukiamini biblia ni kwa ajili ya waumini na sio akina sisi "makafiri" je Roho mtakatifu aliwaongoza hao watafsiri/waandishi wa biblia kwanini zikinzane??

Mfano niliuliza Yakobo alizikwa wapi?? Stephano na Musa wanaeleza tofauti kabisa

Mwanzo 50
13 kwa kuwa wanawe wakamchukuwa mpaka nchi ya Kanaani, nao wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia

Matendo 7
15 Basi Yakobo akashuka mpaka Misri; akafa yeye na baba zetu;
16 wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.

Je ikiwa ni Roho mtakatifu kweli aliwaongoza kwanini wakinzane alipozikwa yakobo??

2. Niliuliza tena na bado sijapata jibu mpaka sasa.... Ni biblia gani halali kutumika kwa nyie wafuasi...je ni NIV au KJV yaani KJV imekuwepo kwa miaka kama 400 sasa ila mwaka 1970 NIV ikasema KJV ilichakachuliwa hivyo wakaja na biblia mpya ambayo imefuta maneno 64,000 kutoka KJV pia imefuta mistari mingi zaidi ya 30 na sura kibao zimepunguzwa je ipi ndio biblia sahihi ?? Na kama ni NIV ndio sahihi ina maana kwa miaka 400 tulikuwa tunafundishwa kwa biblia feki?? Na kama KJV ndio sahihi kwanini mmeruhusu NIV kuchapishwa



Ntashukuru ukinisaidia hapa
 
Fuatilia yanayokuhusu ya dini yako. Yetu tuachie wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nyuzi ni kwa ajili ya kujifunza sasa unaposema nisifuatilie je kama nataka niokoke ila niko njiapanda huoni ukinitimua ndio nitabaki gizani ila ukinipa majibu ndio nitaingia kwenye nuru kama ww ulipo au since when hamtaki ''wapagani'' waokoke??

Je bible halali ni KJV au NIV?? Na kama moja wapo ndio halali na nyingine imechakachuliwa je Roho mtakatifu aliruhusu vipi biblia kuchezewa kwa miaka 400???
 
Mkuu nimekuelewa sana na nimependa ulivyowasilisha mada bila matusi,kejeli na jazba kama wafia dini wengine wa humu JF for that nakuheshimu sana

Sasa ningeomba unieleweshe now that umeniaminisha kuwa biblia haikinzani na ni halali kabisa (okay at least kwa sisi tusio scholars) je kati ya toleo la NIV na KJV lipi ni halali na lipi ni batili???

yaani KJV imekuwepo kwa miaka kama 400 sasa ila mwaka 1970 NIV ikasema KJV ilichakachuliwa hivyo wakaja na biblia ya tafsiri mpya ambayo imefuta maneno 64,000 kutoka KJV pia imefuta mistari mingi zaidi ya 30 na sura kibao zimepunguzwa je ipi ndio biblia sahihi ?? Na kama ni NIV ndio sahihi ina maana kwa miaka 400 tulikuwa tunafundishwa kwa biblia feki?? Na kama KJV ndio sahihi kwanini mmeruhusu NIV kuchapishwa.

 

Siyo kweli kuwa biblia ni ngumu kuielewa. Biblia inaeleweka hata kwa akili ya kawaida maana Mungu tayari alishatupa akili tangu uumbaji. Ukitegemea sana nguvu ya ziada ndo uielewe Biblia hata Shetani anaweza kukupa nguvu hiyo then ukaja kupotosha. tatizo hatuisomi.

Lakini pia ni ukweli usiopingika kuwa Biblia ina mkanganyiko mkubwa sana katika uandishi wake. Sijui ni kwa vile vitabu vya Biblia viliunganishwa katika zama ambayo elimu haikukua sana kama leo hii.
 

Hilo la kutajwa maeneo tofauti walikozikwa mababa wa imani nayo inahitaji uvuvio wa roho mtakatifu. si suala la kuelewa tu kuwa moja kakosea jina la eneo lilipo shamba la Ibrahimu la kuzikia.
 
zote ni halali kabisa, zamani kabla ya KJV Biblia ilikuwa kwa kiltini maana ndio ilikuwa lugha ya dola ya Rumi na lugha ya wasomi, kwa hiyo commoners walipaswa kusikiliza tafsiri kutoka kwa makasisi tu. Kumbuka literary level miaka hiyo ilikuwa ndogo hata huko ulaya, ikawepo hamu kwa baadhi ya watu kulileta Neno la Mungu kwa watu wa kawaida.

Hivyo mfalme James wa uingereza alitumia rungu la dola kuwakinga watafsiri wale ndio tukapata KJV. Lakini hii ilikuwa tafsiri ya wakati ule, miaka kadhaa baada ya vita kuu ya 1 shughuli za uchimbaji (archeology) pamoja na kupatikana kwa maktaba ya kale kabisa (inakadiriwa miaka michache kabla ya Kristo) iliyokuwa na nakala za kale zaidi ya zile watafsiri wa KJV walizozitumia.

kwa hiyo sasa hivi tuna utajiri wa nakala hizo za kale. Lakini kwa taarifa tu; ukisema nakala za kale maana yake nakala za kale. kazi kubwa inayofanyika kuazia wakati huo hata sasa ni kulinganisha nakala hizo, cha ajabu ni kwamba hakuna tofauti yoyote inayoweza kubadili maana au imani, tofauti zilizopo ni makosa ya kawaida kabisa kama watu kwa karne zaidi ya 21 wamekuwa wana nakili kwa mkono bila kuwa na chapa (print).

Ndio sababu nikasema sio rahisi ku dadavua (analyse) manuscript zote hizo halafu nikakupa jibu rahisi. Kwa hiyo NIV wao walikaa na kuamua kuacha mistari ambayo hawakuiona kwenye nakili za kale zaidi. Lakini kumbuka hii ni kazi ya kisomi (interlectual research) ambayo kama reseach yoyoe inategemea na ushahidi uliopo (research conclusions depends upon current knowledge and the tools avaible to obtain the data). kwa hiyo kwangu mimi nahitimisha kwa kusema siwezi kujua kwa nini wale marabi wa kiyahudi miaka ile (walioandika hizi mss tunazolinganisha leo) kwa nini walitofautiana, naamini walikuwa na sababu, na sababu zenyewe zinaweza kuwa ni makosa ya kawaida ya kibinadamu, halafu waliofuata wakaamua kurekebisha hatuwezi kujua.

Kingine kwa faida ya wasomaji au wafuatiliaji wa uzi huu ni kwamba Biblia ina historia ya ajabu kidogo, na kwa majaribu iliyopitia tusingekuwa nyo kama si Mungu kuilinda. Sehemu ya kwanza ya Biblia inaitwa Agano la Kale; hii ilikuwa inatunzwa vizuri chini ya uangalizi makini wa makuhani na walawi lakini mfalme Nebukadreza aliitea Yuda na kuuchoma moto mji wa Yersalemu halafu akalivunza hekali na kulichoma moto, kwa maneno mwngine ile maktaba iliteketea, nyaraka zilizopona ni zile baadhi ya watu walizoziokoa na kukimbia nazo.

Agano Jipya limepitia mateso makali chini ya utawala wa Rumi ambapo ilikuwa kosa dhidi ya Dola kuwa Mkristo au kubeba Biblia. Kwa hiyo naomba tu mniamini hakuna mtu au kundi la watu waliokaa na kuchakachua Biblia, ukifanya utafiti bila jazba au upendeleo (bias) utagundua kwamba copy ya kitabu cha Isaya, kwa mfano, iliyosomwa kabla ya uhamisho wa Babeli na hii ninayoisoma leo haina tofauti ya kimaudhui, inaweza kuwa na tofauti kidogo za kiuandishi (typo).

Nimekufurahia Mr. Zito Jr kwa maswali yako ya kufikirisha, na mimi nimejitahidi kuelezea kwa njia rahisi sana bila kujaribu kuleta uthibitisho wa kisomi (scholarly quatations and references) otherwise ningekuwa naandika Dissertation. Nakutakia siku njema ya baraka kwako na kwa watu wengine wanafuatilia au kuchangia uzi huu
 
Mkuu hata hivo bado haujanielewa nilichokizungumza nashangaa bado umeendelea kuhoji kitu kilicho nje yako. (SASA SIJUI UMEDHARAU MAJIBU YANGU?)
 
kitabu cha wayahudi waliotengenezwa wakati wayahudi original wanafichwa na ndio sababu ya kuingizwa hayo yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…