Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Bwana @zittojunior nafahamu namna unavyoheshimika hapa jf kwa mada tata na vikirishi ila nikusaidie kitu kimoja cheza na mipaka yako katika mambo yanayomuhusu Mungu yaani hapa sizungumzii dini wa dhehebu.

Sijaona utata katika vilivyoandikwa katila bibli kwakua ni vitu vya kiimani na si kisayansi kwamba vinahitaji scientific proof.... Huweizi pata.
Ninauhakika hujisoma biblia ukaielewa nnauhakika hii hoja umeiokota.... Ni kwamba mi si muandishi mzuri ila nishakutana na hoja hizi wakati nafuatilia imani zilizo kinyume na Mungu.....

Ukisoma biblia Agano la kale na jipya limetofautiana kimapokeo tuu lakini kusudio la Mungu lilikua moja tu na bado liko vile vilehata sasa.

Tambu baraza lilipata mamlaka ya kipi kiingie kipi kitoke kutoka kwa Mungu (uvuvio) na huo ndio mpaka wangu wa kuhojik
Sasa kwanini hizo injili zingine haziwekwi hadharani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefurahishwa saana kwa huu ufafanuzi.....
Tatizo watu wa GT wanazani wamesoma kila kitu wamemaliza kumbe si kweli, wengi ni vi 'hoja' wanaokoteza kwa wafuasi wa mashetani na kuja kupotosha watu.

Mleta mada ameleta mada vikorishi kwa watu wasiojua maandiko wala imani.

Biblia ni kitabu kilicho vuviwa kila moja kwa wakati wako ila kwa dhumuni moja tuu kama kuna vilivyo acjwa maana dhumuni ni tofauti na hivi vingine ambavyo Mungu alikusudia vitufikie.

Kama zama hizo manabii haikua rahisi kuwaamini mpaka kujaribiwa wengine unadhani ni waongo wangapi waliibuka wakijifanya wanatoka kwa Mungu?? Na ndio maana Mtume s.w.a anawaambia waislamu Quran imekamilishwa na taorati, zaburi, injili pamoja na Quran yenyewe kwakua msingi wa Imani kwa Mungu wa kweli ni kutoka kwa wayahudi kama taifa teule.

Biblia kwangu ni kitabu kisicho na shaka bali ni kimbilio na majibu ya maswali yangu yoote maana hata hichi kuulizwa juu ya kweli kutiliwa shaka ilashanijulisha.

Wakristo tusome biblia, waislamu tusome biblia na Quran.
Nakusahihisha kidogo, hapo siyo Quran na Biblia bali ni QURAN, INJILI TOURATI NA ZABURI. sijui maana ya biblia ila naamini ni mkusanyiko wa vitabu vya mitume na manabii ambao baadhi yao hawatambuliki katika UISLAM. All in all Tunatakiwa tusome vitabu vyote ili tuwe na ufahamu zaidi kuhusu imani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hiyo unayoisena ni kwa taarifa yako ni "hybrid" ya holly bible. Jamaa aliikariri kwa muda mfupi kama unavyotaka kufanya mtihani halafu unalazimisha material mengi kwa wakati mmoja, jamaa yakajichanganya kichwani , na akawa atatamka maandiko yaliyohalisi na madude mengine kama vile mtu anayeota ndio maana hata hayo maandiko hayajanyooka yaani habari hajulikani imezia wapi wala inaishia wapi ipo kama mashairi yanayoanzia mwisho
HOW GIVES? VIVID EXAMPLES.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HOW GIVES? VIVID EXAMPLES.

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Biblia ilikuwepo na yeye aliikuta hakuna ubishi kuhusu hilo

2. Biblia inaonyesha kuwa mtoto pekee wa Ibrahim ambaye aliambiwa amtoe sadaka ni ISAKA wao wanamwita ISIAKA mwana wa ahadi na wa uzeeni mwa SARAH wao wanamwita SARAT mke halali na wa ndoa wa Ibrahim

3.Kitabu chake kilichokuja baadaye hiyo story ipo lakini imepindishwa na kinaonyesha kuwa mtoto ambaye Ibrahim aliamriwa amtoe sadaka ni ISHMAEL ambaye hakuwa mtoto wa ahadi wa ibarahim bali alizaa na Housegirl wake aitwaye HAJIR baada ya kushauriwa na mkewe SARAH baada ya kuona kilometa za umri zimesonga na kuitupilia mbali ahadi aliyopewa na Mungu
 
Tuletee basi hivyo vitabu vilivyoondolewa kny biblia mfano vya Enoch?
Ningefurahi sana mkuu.
 
1. Biblia ilikuwepo na yeye aliikuta hakuna ubishi kuhusu hilo

2. Biblia inaonyesha kuwa mtoto pekee wa Ibrahim ambaye aliambiwa amtoe sadaka ni ISAKA wao wanamwita ISIAKA mwana wa ahadi na wa uzeeni mwa SARAH wao wanamwita SARAT mke halali na wa ndoa wa Ibrahim

3.Kitabu chake kilichokuja baadaye hiyo story ipo lakini imepindishwa na kinaonyesha kuwa mtoto ambaye Ibrahim aliamriwa amtoe sadaka ni ISHMAEL ambaye hakuwa mtoto wa ahadi wa ibarahim bali alizaa na Housegirl wake aitwaye HAJIR baada ya kushauriwa na mkewe SARAH baada ya kuona kilometa za umri zimesonga na kuitupilia mbali ahadi aliyopewa na Mungu
UNAELEWA MAANA YA VIVID EXAMPLES?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAANDIKO YENYE UTATA
Kuna mistari mingine ambayo ni halali kibiblia ila imebadilishwa maeneo husika ipo mistari zaidi ya 50 kwenye agano jipya mfano Yohanna 7:53-8:11 kuhusu Yesu kuwepo hekaluni ila ghafla kipande kati ya 7:52 na 8:11 vimechomeka story ya mwanamke kahaba alietaka kupigwa mawe na ghafla mstari wa 12 unaendelea Yesu akiwa hekaluni hii inakubaliwa na wanatheolojia wote kuwa kilichomekwa na hakikuwepo kwenye maandiko orijino kama una biblia hapo kasome hiki kipande alafu utaelewa nachosema. Kanisa likaamua kuita vitabu vyenye maandiko na uandishi wa utata kuwa ni disputed books ilihali zina sifa zile zile za kuitwa pseudepigraphi na kutakiwa kufutwa kwenye biblia. Mfano Marko 16 inaishia mstari wa 8 ila 9-20 haikuwepo bali iliongezwa miaka mingi mbele na mtu asiyetambulika ila bado kipo kwenye biblia lakini kitabu cha Enoch au Yuda iskariot vimetolewa kwa hoja hiyo hiyo?? Kuna ajenda gani hapa wakuu?? Kipi tunafichwa?? Anyway disputed books kulingana na mwanatheolojia E. P. Sanders ni waefeso,wakolosai,2 wathesalonike, 1 & 2, Tito na vingine vingi.... Je kama vina kasoro kwanini vimeachwa??

VILIANDIKWA NA MUNGU?
Kuna hoja inasema vitabu vya Biblia viliandikwa kwa uweza wa Roho mtakatifu hivyo vile vilivyoachwa havikuandikwa na Roho mtakatifu sasa tujiulize GT kama kuna mistari ya Biblia imeongezwa na wanadamu mfano isaya,wimbo ulio bora,Tito,Yeremia,marko je bado hoja hii ina mashiko ilihali wanatheolojia wanakiri biblia ilichezewa kwa mifano niliyotoa hapo juu na kama si kweli viliandikwa kwa uweza wa Roho bali fahamu za wanadamu je kwanini basi ilitumika kuzuia vitabu kama Injili ya Yuda ama Thomaso?? Je hakuna agenda ya siri kwanini vilizuiwa alafu sisi tukaaminishwa tu kuwa havikuwa na uvuvio wa Roho mtakatifu??
View attachment 830349
PSEUDEPIGRAPHI ZINAKINZANA NA BIBLE
kuna hoja ilitolewa kwamba vitabu vya biblia vinakinzana na Pseudipigrapha ndio maana vikatolewa kwenye bible ila cha kujiuliza GT mbona kuna taarifa zinakinzana ndani ya biblia lakini havijatolewa??

MIFANO
Mathayo 4:1-11 inasema mara tu baada ya ubatizo Yesu alienda kufunga siku 40 ila Yohana 2:1 anasema siku tatu baada ya kubatizwa Yesu alikua kwenye harusi ya Cana!!

Au mathayo 27:44 wale wezi wawili walimtukana Yesu ila luka 23:39 inasema mmoja alitukana mwingine alimtetea.

Mathayo 28:9 inasema Yesu baada ya kufufuka aliruhusu Mary amshike ila Yohana 20:17 Inaonyesha baada ya kufufuka na kuonana na mary, Yesu akamzuia kumgusa sababu alikua bado hajarudi kwa Baba!!

Hyo ni mifano tu ila kuna mistari zaidi ya mamia inayopishana taarifa ila vimeachwa kwenye bible lakini pseudipigraphi zikipishana hta neno moja ndio wanajengea hoja kwamba ndio sababu havipo kwenye bible je sababu hii ilisababisha vitolewe ama kuna mengi tunafichwa??

HITIMISHO
Kwa kuhitimisha labda niseme tu kumekuwa na maswali mengi juu ya chanzo hasa cha vitabu vingine kutolewa kwenye biblia na vingine kuachwa wakato vina kasoro zile zile..... Na hata mkuu Pendael24 alishawahi kuhoji kwamba kama tunafikiri biblia imechezewa je Mungu haoni hadi aruhusu hilo?? Na akahoji mbona Biblia inatenda ina maana kazi ya forgery inaweza kuwa na nguvu za Mungu na akanihoji je wachungaji wote hawa wakubwa hawalijui hili kiasi Mungu awaache watumie bibloa iliyochakachuliwa?? Kiukweli nilikosa majibu ila nategemea leo humu majibu yote yatapatikana

NB: Mimi nimechokoza mada tu ili kupata maarifa ya GT ila sio msimamo wangu kuwa bible ni batili au Qur'an ndio sahihi hivyo tunapojadili hoja humu tuhakikishe tunazingatia hilo pia udini na kejeli na matusi sio uwanja wake humu, nataka tujadili kwa kujifunza sio kupambana.

Karibuni kwa mjadala
Haya mambo ni mazito. Nafikiri hayo ni moja ya mambo yanayosababisha kuwepo na madhehebu mengi mno. Siezi kujudge yet....nafanya research kwanza...

Bwana yesu asifiwe!
 
Back
Top Bottom