ndugu katika kristo zitto junior ninaomba kutumia nafasi hii tushirikishane kimawazo juu ya moja ya maswali uliouliza katika uzi wako.
kumbe hiki hapa chini ndicho ambacho kwa kuanzia tu ningependa kukichangia then mengine nitaleta mawazo yangu kadiri ya nafasi na muda
Mathayo 28:9 inasema Yesu baada ya kufufuka aliruhusu Mary amshike ila Yohana 20:17 Inaonyesha baada ya kufufuka na kuonana na mary, Yesu akamzuia kumgusa sababu alikua bado hajarudi kwa Baba!!
kwa faida ya wengi ongeza na hii pia.
ni kwanini Yesu amemzuia Maria Magdalena asimguse katika sura ya 20:17 lakini baada ya aya chache za sura hiyo hiyo yaani 20:27 anamwambia Thomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu, ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu?
mpendwa zitto junior hayo ni moja ya maswali kati ya mengi ambayo watu wengi hutumia kudai kuwa biblia inajipinga yenyewe ila ukweli halisi haupo ivo yaani biblia haijipingi ila wengi wetu ndio hatujui na wala hatuthamini na kuzingatia kabisa mambo muhimu katika kutafuta ukweli wa kimaandiko. (kiufupi sisi ndio tunajipinga na wala sio biblia)
hayo mambo ambayo yapo matano nimekwisha yafafanua katika post yangu post namba #145. na hilo namba tano yaani lihusulo mambo ya lugha ndilo linakwenda kujibu swali lako.
4: lugha asili ya kitabu husika cha Biblia (hiyo mpendwa wengi huwa tunachukulia poapoa lakini kwa upande wa kanisa katoliki limewekeza katika hilo kwani ni muhimu sana kufahamu na kuielewa lugha asili iliotumika kuandika kitabu husika ili kupata ujumbe halisi uliokusudiwa na mwandishi. ndipo utakuta kanisa katoliki linawataalamu lukuki wa lugha za biblia yaani kiebrania cha kale kilichotumika kuandika agano la kale, kigiriki kilichotumika kuandika agano jipya na LXX, kilatini nk
jitahidi ulisome kwa umakini na kulielewa kwani ndilo linalokwenda kujibu swali lako hapo juu
mpendwa zitto junior
tunasoma katika Biblia Takatifu kuwa siku ile ya kwanza ya juma yaani aliyofufuka Yesu, Maria Magdalena na wenzake wengine walipokwenda kaburini waliukosa mwili wake, walipokuwa wakiondoka kurudi kuwapasha habari mitume walikutana na Yesu naye akawaambia “Salaam wao wakamkaribia wakamshika miguu wakamsujudia” (Mt 28:9).
sasa Je, kama Mwinjili Yohane anasema Maria Magdalena alizuiwa kumgusa lakini Mathayo Mwinjili anasema alimgusa, tusadiki lipi? tuamini lipi na tuache lipi ?, je bible inajipinga ? au sisi ndio tunajipinga ?
Kama suala lingekuwa ni kutomgusa yesu baada ya ufufuko wake. je, ilikuwa ni kutoguswa na Maria Magdalena tu ? au wote na mbona Tomaso alimgusa kabla hajapaa ?
Pengine ni vyema turudi kwenye lugha asili ya mwinjili yohane yaani kigiriki sasa tusome Biblia Takatifu kwa lugha ya Kigiriki lugha aliyotumia Yohane kuandika Injili yake, ili tuweze kupata tafsiri sahihi ya kile alichokisema Yesu.
Nasoma Injili Yn.20:17
“Legei auth o ihsous, “mh mou autou, aupw gar avnabebhka pros ton patera mou... poreuou de pros tous adelfous mou, kai eipe autois; a vabai vw pros tov patera mou kai patera umwn, kai eov mou kai eon umwn”
Kwa maandiko hayo ya kigiriki cha yohane mwinjili tunaona kuwa, Maneno,
me mou apotou, yaani usinishike katika sentensi za lugha ya Kigiriki, huundwa kwa muunganiko wa “
me na katazo lililo katika wakati uliopo”.
Hii ni kusema, neno “
usinishike” linamaanisha amri ya kukataza kuendelea kutenda kile ambacho tayari kinafanywa au kinatendeka au kinaendelea kutendwa.
Amri hii inalenga kukatisha tendo lisiendelee. Ni sawa na kusema,
acha kufanya ufanyalo au koma kulifanya unalolifanya.
Kwa maana hiyo, Amri ya Yesu (Yn 20:17) kwa Maria Magdalena ni ya mfumo huu. Anamwambia kwa kigiriki,
me mou apotou, kuonesha kuwa Maria Magdaleja alikuwa tayari amemshika Yesu na alikuwa an`endelea kumshikilia. Yesu anachokataza ni tendo la Maria kubaki amemshikiria Yesu yaani anamwambia aache kuendelea kujing`ang`aniza kwake amwachie ili mambo mengine yafanyike.
Kwa mant)ki hiyo, Mwinjili Yohane hatofautiani na Mathayo kuhusu Maria Magdalena kumshika Yesu.
Yesu hamzuii Maria Magdalena kumgusa bali anamwambia imetosha asiendelee kumshika.
Ni kweli kwamba amefurahi kumwona lakini furaha hiyo ya maria magdalena ni lazima izingatie ukweli kuwa kitendo cha Yesu kuonekana tena baada ya kifo chake si cha kudumu ni kitu cha Muda mfupi, yaani kitu cha kupita tu.
Ndiyo maana anaendelea kumwambia sababu ya kumkataza, Yesu anasema, “
aupv gar anabebhka pros ton patera mou. Yaani, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Ni kweli Yusu alitakiwa aondoke ulimwenguni kwenda kwa Baba yake ili apokee tuzo lake kwa kazi aliyokwishaifanya.
Ndiyo maana tukirejea nyuma kidogo aliwaambia mitume wake akisema, "Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona." na hIlo ni kwa Sababu anaenda kwa baba (Y. 16:16).
Sasa kitambo kidogo, ndicho hicho kwani kikiisha anapaswa kuondoka kwenda kwa baba.
Yesu anaendelea kumwambia, “
poreuo de pros tous Adelphous mou,kai eipe autois,anabaivw pros tov patera mou kai patera umwn,kai theon mou kai theon umwn”.yaani enenda kwa ndugu zangu ukawaambie ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu .naye ni Mungu wenu.
Maneno hayo ya Yesu yanauonesha uhusiano wa karibu kati yake na Mungu na kati ya Mungu na mitume kumbe hata kama ataondoka, hakuna kit!kacho haribika.
Kutokana na maelezo hayo ni hakika kwamba Yohane alitaka kutufikishia ujumbe fulani ambao ama alishindwa kufikisha au alifikisha lakini haukuweza kueleweka kwetu sisi ambao Biblia tumeipokea katika tafsiri toka lugha ya Kigiriki.
Laiti tungekuwa tunajua jinsi sentensi za kigiriki zinavyoundwa na masharti yake, tusingepata shida kumelewa yohane.
kumbe kwa kifupi Yesu anapomwambia Maria Magdalena asimguse anamaanisha kwamba, Kumgusa Yesu kunakotakiwa tangu alipofufuka ni kwa njia ya imani. Maana yake ni kuwa,
baada ya kupaa mtu anamgusa Yesu si kwa mkono bali kwa kuamini kuwa amefufuka na hafi tena.
Ndiyo maana baada ya siku 8 anapowatokea tena mitume wake, Yesu alimwambia Thomaso kuwa, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona wakasadiki.
Hao ndio mimi na wewe ambao tunamsadiki kwa imani yetu ingawa hatukumwona kwa macho.
Pia habari hii ya ufufuko ni habari ya kimisionari zaidi.
Hatutakiwi kupoteza muda tukishangilia ufufuko wa Yesu peke yetu bali tutoke twende tukawashirikishe wenzetu ambao bado hawaijui ndiyo maana anamwambia Maria magdalena usiniguse maana yake, usipoteze muda mwingi katika kuniabudu kwa furaha bali nenda kawaeleze mitume kile ulhchokiona karibu naenda kwa Baba na ningependa kuwaona wao badala ya kubakia na wewe tu.
(Yn. 20:17).
hivyo kwa maelezo hayo mathayo na yohane hawajipingi hata kidogo. na kama tulivoona tatizo sio waandishi ila tatizo ni watafsiriji wa biblia toka katika lugha mama za waandishi kuja lugha zetu hizi sijui kiiengereza, kiswahili nk
mpendwa zitto junior
ninaomba niishie hapo kwa leo pia kama kutakuwa na makosa ya lugha kama kukosea herufi hasa hicho kigiriki nk
NINAOMBA UTANIWIA RADHI sababu mimi sio mtaalumu sana wa hiyo lugha ila ninaibiaibia tu. lakini naamini lengo langu na ujumbe wangu vitakuwa vimefika.
NIKUTAKIE JUMAPILI NJEMA NA SIKU NJEMA PIA.
mtu chake
SANCTUS ANACLETUS
KIBUYU 180
Otorong'ong'o