Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA


Huna hoja sanasana naona umeandika pumba hata sijakuelewa unamaanisha nini. LETA HOJA
 
Ningependa kujua nani wakunithibishia kama biblia siyo story ya kufunga au composed novel mixed with true events plus fictions wakuweza kunielekeza kindaki mdak wa haya mambo
 
Hakuna apologetics wazuri humu ndani.
 
Dini ni IMANI

IMANI ni fumbo, vitabu vinavyo ondolewa vinaenda kinyume na fumbo la imani ya dini husika.

Kitabu chochote kiwe cha ukweli au Uongo kama kitaelekea kufumbua fumbo hilo lazima kitapigwa marufuku katika mafundisho ya dini husika.

Kwa muktadha huo, ni halali kwa dini yeyote ile kukataza au kupiga marufuku mafundisho yeyote ya kitabu kinachoweza kuyumbisha imani ya dini husika.
 
Okay tufanye Book of Enoch na Jasher hakifai na kinapingana na Mainstream Bible je kwanini Kitabu Cha Yuda kina cite Book of Enoch? Na Kwanini Kitabu Cha Yoshua kina cite Book of Jasher?

Kama havifai basi visifae kwa wote sio sisi tunakatazwa kusoma au lucite ilijali mitume wame cite na kuweka maneno ya hivo vitabu kwa Bible?

Hiyo ndio double standard inayoleta huu mjadala
 
Katika pitapita yangu huku JF nimekutana na andiko lako nimelisoma na nimelielewa,umeeleza vizuri lakini kuna vitu mhimu hujavielezea inawezekana umesahau au umefanya makusudi ili kutimiza malengo yako ya kutuaminisha kuwa biblia ni kitabu chenye makosa mengi kama ulivyoeleza.

Kwanza unaposema kuwa wanatheologia wote duniani kuwa wanakubaliana juu ya swala fulani, je unajua kuwa kuna makundi matano tofauti ya wathiologia duniani? Hao waliokubaliana ni wanathiologia wa kundi lipi? Kama kweli mada hii umeiandika kutokana na ufahamu wako ulionao kuhusu biblia na hujaikopi sehemu je ni kweli hujui vigezo vilivyotumika na macanon ili kukubali vitabu vilivyoingizwa katika Biblia huku vingine vikikosa vigezo.

Je ni kweli hujui kuwa kulikuwa na miaka zaidi ya 500 ya ukimya kati ya agano la kale na jipya miaka ambayo wanadamu waliamua kuandika hadithi wakisema ni Mungu kasema nao,kwa mtililiko wa andiko lako ulipaswa kuyajua hayo pia.
 
Okay tufanye Book of Enoch na Jasher hakifai na kinapingana na Mainstream Bible je kwanini Kitabu Cha Yuda kina cite Book of Enoch? Na Kwanini Kitabu Cha Yoshua kina cite Book of Jasher?
Inawezekana hivi vitabu viliandikwa na waandishi wengi kwa nyakati tofauti (tena baada ya miaka sana mingi kupita kati ya mwandishi mmoja na mwingine).

Hili limeleta ukinzani wa mawazo au maandiko kati yao, hivyo ni rahisi ndani ya kitabu kimoja kuwe na maandiko yanayopingana sababu ya utofauti wa mawazo au kutofautiana kwa historia baina ya waandishi.

Kunukuliwa sidhani kama ni hoja kubwa Sana, inawezekana waliko nukuu ni kwenye maandiko ya waandishi wanaofahamika.

Mfano: nje ya mada

Ukisoma habari za Ibrahimu alipotokewa na malaika watatu waliokuwa wanaenda kuichoma moto Sodoma na Gomora.....(Mwanzo 18:2)

Ila mbeleni wanaonekana malaika wawili walifika nyumbani kwa Lutu, hatujaambiwa yule mwingine alielekea wapi. (Mwanzo 19:1).....hapa Kuna mkanganyiko kuhusu huyu malaika wa 3,je alienda wapi ?

Ila kuna malaika alimwambia Ibrahimu kuhusu Sara kupata mtoto mwakani kwa majira yale (Mwanzo 18:10)...je huenda alikuwa mkuu wa wale malaika wawili na hakuja kwa kazi ya kuichoma Sodoma, ila alikuja kuzungumza tu na Ibrahimu ?

Pia Mungu alizungumza na Ibrahimu kuhusu kusudio lake la kuichoma Sodoma na Gomora kabla ya kuondoka(Mwanzo 18:33 )........hapa pia pana mkanganyo,je huenda aliyekuwa akizungumza na Ibrahimu ni yule malaika ambaye hakushuka kwenda kwa Lutu pamoja na wale wawili ?..

Je huyu malaika ambaye hakwenda kwa Lutu, alikuwa ni malaika kweli ?, maana ametajwa kama 'Bwana' /( Lord ),r ejea mazungumzo yake na Ibrahimu )...

Na kama hakuwa malaika, je alikuwa ni nani ?, Kwanini hakwenda huko Sodoma kwa Lutu ?, Je alielekea wapi ?

Kumbuka ni yeye pekee tu aliyezungumza na Ibrahimu, wale wengine waliongea na Lutu walipofika kwake.
 
Na ndio hapa napaojua watu hamsomagi threads. Nimeshakwambia Pseudepigrapha na apocrypha ziliachwa kwenye canon.

Sasa swali langu kwanini Biblia hiyo hiyo inatutuma tukasome hizo vitabu vilivyokataliwa kama reference??

Joshua ananakili Book of Jasher whilst Yuda ananakili Book of Enoch why watumie vitabu ambavyo Biblia yenyewe inavipinga? Or rather kwanini mitume waruhusiwe kucite apocrypha ilihali sisi haturuhusiwi?

Kingine unasema vigezo vinajulikana!!? Vigeoz vipi? orthodox, catholic, Protestants wote tuna canon tofauti ilihali tunaamini vitabu vilichaguliwa na Mungu mwenyewe now why wengine wabaki na 66 wengine 72 wengine 84 etc hamuoni tuna contradict wenyewe..
 
Kumbeee biblia sio kitabu Cha Dini
Asante Sana mkuu 😁
 
Utupe pia siri zilizofichwa kwenye Qur'an Mkuu!!!
 
Ila kusema Quran ni kitabu kitakatifu ni sahii mkuu???
 
Haya mambo ya imani magumu, mleta mada tukutane mbinguni, tu maana wakati vinaandikwa hatukwepo haya ni mambo ya kiroho zaidi
Anatulazimisha tuamini maoni yake!!!!Sisi ni wakristo na biblia ni kitabu kitakatifu!!!Mimi namshauri akadili na imani yake tu
 
Wewe dili na Quran mdogo wangu Zitto au una chili binafsi kwa Mungu WETU YESU?????MBONA SISI HATUMSEMI MUDI NA KITABU CHAKE CHA KUKOPI!!!Sisi hatuwezi kufuata tamaduni zenu wala kuzijadili!!!!Sisi wenyewe tunaona Quran miyeyusho tu ila tumewaachia wenyewe sababu haituhusu!!!SISI NI WAKRISTO MPAKA KUFA NA HUWEZI KUTUBADILI
 
Ushasema kwa mtazamo wako Quran ndio kitabu sahii sasa unataka tujadili nini mdogo wangu????UNGELETA MADHAIFU YA QURAN NA BIBLIA HAPO SAWA ILA KWA MAONI YAKO TUSHAJUA MALENGO YAKO!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…