Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Mara nyingi watu waliokosa hoja hukimbilia kuwaita wenzao makafiri,wafuasi wa shetani nk..kama hujui kitu bora mtu ukae kimya utapata aibu bure hapa.na nakuhakikishia mkuu hautapata jibu lililonyooka maana vitabu tumepewa tu na kukaririshwa na hatujui vimetoka wapi hadithi nyingi bla bla bla...
 
Umetisha sana mkuu kwa haya maelezo yako, sasa hao NIV wanaodai biblia za kwanza hasa KJV zimechakachuliwa wapo sahihi au wanapotosha?? Na kama wanapotosha je kwanini Biblia yao imekubaliwa kutumika kama Biblia rasmi duniani kwa karne hii hasa pale unapoandaa tafiti au mafundisho ya kusambaza duniani kote NIV ndio inatakiwa kutumika

Na pia kama NIV wakiwa sahihi kuwa kuna mistari ya biblia ilichezewa je kuna uhalali gani wa kuvitoa hivyo vitabu vya apocrypha nilivotaja hapo juu

Hapo ndio nataka kuelewa zaidi mkuu maana hizi version mbili zina mgogoro mkubwa sana
 
Mimi binafsi Naamini kuwa Biblia ni kitabu kitakatifu kwa sababu yaliyoandikwa kwenye bible tunayishi na tunayaona na yanatongoza kwenye maisha yetuu.
Ni kweli biblia ni takatifu ila sasa zipo mbili kubwa yaani NIV na KJV ambapo NIV inasema KJV imechezewa na KJV anadai NIV ni maagenti wa shetani waliotumwa kuharibu neno ila ushahidi wote unaonyesha NIV wanazo vyanzo bora zaidi je nini maoni yako katika hili..... Biblia gani ndio takatifu kwa muktadha huu??

Ahsante
 
Hao wanao sema ni watu gani? Ungeweka nahiyo ambayo unasema ipo sahihi ili tufanye ulinganisho.
NIV ndio wanasema yaani harper-collins INC kikundi cha wanatheologia waliokutana kati ya 1965-1973 wakapitia takwimu na nyaraka za zamanu zaidi hasa dead sea scrolls wakagundua zinacredibility kuliko chanzo walichotumia wenzao wa KJV Yaani textus receptus huko mwaka 1600..... Hivyo kwa namna yeyote KJV au NIV moja ni mkweli na mwingine anapotosha sasa ukweli ni upi?? NIV au KJV.

Na ikumbukwe biblia ya kiswahili imetafsiriwa kutoka kwenye kiingereza cha version ya KJV ikimaanisha kama NIV ndio wapo sahihi basi biblia ya kiswahili ya chama cha biblia tuliingizwa mkenge na kama KJV ndio wapo sahihi basi tafsiri za biblia ya NIV zipigwe marufuku maana zimenyofoa maneno 64,000 na mistari 100 kidogo

Hapa ni zero-sum game so tusijibu kwa juu juu kumbuka hayo maneo 64,000 ni mengi sana kubadili maana ya mistari ya biblia so tujibu tukiwaza hilo pia
 
Mzee ni tafsiri gani ya biblia unayotumia? Maana mm nina UV hiyo mathayo 27:44 imesema tu wale wezi haijasema idadi yao ila Luka ndio inasema kuhusu huyo mwizi 1 aliemtukana Yesu contradiction iko wapi hapo sasa?
Mkuu 44 ya biblia ya chama cha biblia iko very clear kwamba wale wezi waliosulubiwa naye waliungana na wale makuhani kumtukana Yesu..... Lakini marko anapinga anasema ni MMOJA tu aliyetukana sasa kivipi kwenye Mathayo wawepo wengi wanaotukana ila marko awepo MMOJA

Na kwanini mathayo a-generalise kwamba wezi walimtukana ilihali hajui kuna exception ya mmoja?? Anyway tusilalie mstari mmoja nimeweka hapi mistari 6 sample ila biblia nzima ina mistari 105 inayokinzana kuanzia alipozikwa yakobo,wanawake walioenda kumuona kaburini,muuaji wa saul,vizazi vya Yesu na vinginevyo havina madhara sana ila vinatofautiana data. Ingekuwa vyema basi utolee maelezo pia ili tuwe kwenye boti moja.
 
mathayo 16:28
yesu alisema uongo
Kuhani nyabhingi.

Asalaam Aleikum, Waramatullah Wabarakatuhu
Ni salamu hiyo kwa Lugha ya Kiarabu.
Nasema hivi Kuhani,
Umeshatueleza mara nyingi tu kuwa kutokana na kitabu chako unachokiamini cha
" The Book Of The Dead "
Yesu Kristo hajawahi kuwepo hapa duniani, na habarizake zote ni za kutunga na kuzushiwa.
Sasa ni vipi unasema tena kuwa

" Mathayo 16:28 Yesu alisema uongo " ?

Huyo Yesu ambaye hakuwahi kuwepo, halafu tena huyohuyo aseme uwongo, umempata wapi Kiongozi.
Unajua Kuhani ni mtu wa kuaminika ha hapaswi kujikanganya kwenye maelezo yake mara kwa mara.
 
Mkuu siri moja wapo ni elimu ya jinsi mwanadamu anaweza kucontrol ulimwengu wa roho,kuona mapepo kwa macho majini kwa macho, na sayansi nyingine ambazo zimeongelewa kwenye kitabu cha Enoko na baadhi ya manabii na mitume wanazitumia kufanya miujiza makanisani?

Kingine kuna kitabu cha injili ya Yuda kinaelezea wanachokiita injili ya kweli na namna gani Yuda ndio alipewa "nondo" zote na Yesu na hata kufikia kusema Yesu hakusalitiwa na Yuda ila imebadilishwa kwenye vitabu vingine ili ionekane Yuda ni mbaya na wasije kusoma hicho kitabu chake. Pia kuna siri ya ugomvi wa Mungu na shetani bila kusahau siri ya uumbaji na issue nzima ya kilichotokea bustani ya Eden sasa hivi ndio naviita siri kwamba huenda biblia ya sasa ilivitoa hivi vitabu ili kuzuia watu wasijue kweli hizo kwa ajili ya maslahi yao hao viongozi wachache wa kanisa.

Ndio nikaenda mbali kuhoji kwamba hizo sababu zilizofanya hizo vitabu zitolewe mbona bado zipo kwenye vitabu vingine vya bible na jambo hilo limethibitishwa na biblia inayotumika sasa yaani NIV ilipofuta maneno 64,000 na mistari zaidi ya 100 ndio nahoji hatufichwi kitu kweli maana kma sababu ndio hizi basi kuna vitabu zaidi ya 20 vya biblia ya sasa vitatakiwa kuondolewa si ndio maana yake??

Sijui unanisoma hoja yangu mkuu??
 
HII YA AJABU KABISA...mnamo katikati mwa Karne ya 20 mgonjwa mmoja uko uturuki , alipewa Biblia ,na alipokua anarudi nyumban ,alikutana namarafik akawaonyesha, Mmoja akaichukua ile Biblia ,akaitoa karatasi zake aitupa ,, mgonjwa aliogopa kuiokota, akapita mzee mwenye ki Cafe chake, akaziokota zile karatasi,,Akaanza kufungia vitafunio kwa wateja wake.... Maajabu kila mteja alikua akirudi kuomba karatasi nyingine za aina iyoooo..... Mwishooo Siku muuza biblia alivyorudi eneo lile,MAELFU YA WATU WAKAGOMBANIA KUNUNUA BIBLIA.

kanisa lenyewe la kirumi lilijaribu kuitoa Biblia mikonon mwa watu, likisingizia kua "Masikin hatakiwi kua na biblia bali matajiri nawatu wajuuu tu"..... Hiii ikafanyaaa
Padre Jerome alotafasiri Biblia toka Kigreek na Kihebrania na kua Kilatin , ashutumiwr na maskofu wakimtuhumu Kuchezea Neni la Mungu.... Lkn maajabu tafasir yake ya Kilatin ndio ikaja kutumia ulaya nzima.

1320 Mtumishi John Wycliff huko Uingereza aliamua kuhakikisha anagawa biblia kwa Waingereza , biblia hii ilotafasiriwa kingereza Ilipingwa na Ma askofu na kumtuhum jamaaa Kuingilia mikakati ya kanisa.. Alikamatwa na Kuchomwa moto akiwa hai. Nawote walokua nabiblia hii ilotafasiriwa kingereza, walikamatwa na kuchomwa motoooo...LKN BIBLIA ILIISHI.

mwaka wa 1500 bwana William Tyndale Muingereza alitafasiri biblia kutoka ktk kingereza mpaka ktk lugha ya jamii yake , watu wengi wakaielewa sana.. Akakamatwa na ALICHOMWA MOTO AKIWA HAI ,na biblia zake nyingi zilichomwa moto.
Siku anachomwa moto alisema ""MUNGU MFUNGUR MACHO MFALME WA UINGEREZA" .....ndio Miaka mitatu Baadar Mfalme HENRY WA V11 Akaamuri Kuchapishwa kwa BIBLIA KWA LUGHA ZOTE ....

1700 Voltaire ,huyu mfaransa Tajiri alinunua mashine ya kuprintia akasema " Miaka mia moja tangu sasa HAPATAKUA NA BIBLIA TENA" maajabu mzungu mmoja alinunua Biblia agano lakale kwa dola 500000 ... Wakati huo Biblia ya uongo ya Voltaire wakainunua watu nane tu na kwa sent senti ... Miaka 50 baada ya kufa kwa huyu jamaa ,NYUMBA YAKE NA MASHINE YAKE VIKAGEUZWA KUA KIWANDA CHA KUZALISHIA BIBLIA

1229 baraza la Rumi liloongoza na Pontiff Gregory wa 1X , lilitangaza Rasimi kua Asipatikane mtu wa kumiliki Biblia kwa maagano yote yaaan Zaman na Jipya ...... LAKIN WAKASHINDWA

1910 baraza la Torragona likarudi tena na Madhimio kua anayemiliki biblia basi aisalimishe ili Ichomwe moto...LKN WAPIIII.

mmesahau nahuyu alosemaga " Socialism, communism, clandestine society, BIBLE SOCIETY, .......PESTS OF THIS SORTS MUST BE DESTROYED BY ALL MEANS?? 8/12/1886......

Hizo ni baadhi ya Majaribio ya kuifuta kabisa BIBLIA ...... LKN MUNGU ANASEMA,.. YADUNIA YOTE YATAPITA LKN HAMNA NENO LA BIBLIA LITAKALOPITA.

Ndio kwasasa Vita hii inaendelea ndio maana kila kukicha kunaibuka Biblia za kila aina .



The TransporterJF-Expert Member
Mods mtulie tuli !! Nyuzi nying zinaandikwa kuiponda/kuikosoa hata kusema Biblia ni Ya Uongo na visa vyake ni vya Uongo.

Huu uzi, nmeuandika Kama ukombozi kwa wale wavivu wa kusoma ,Nimeuandika kama MAJIBU ya watu wanaopotosha.


Mtu mmoja anasema ,Ukweli wa biblia ulofichwa!!!! Biblia ni ya Uongo , Biblia imeandikwa na Padre Jerome , Biblia imeandikwa na Freemason,Biblia imeondolewa vitabu, biblia matukio yote ni yauongo ....... Huwa nacheka sanaaaa ,Jamaaan wanaJF nadhan Kupitia izo HOJA ,mnaona namna UONGO UNAVYOJICHANGANYA NA KUJIDHIHIRISHA WENYEWE KUA NI UONGO.


Tuendelee zetu ,

Biblia ni Mkusanyiko wa Vitabu vya mafundisho vilivyoandikwa na Waandishi wapatao 40 . Waandishi hawa ndio Manabii tunaowajua pamoja na mitume ambao hawa mitume wengine walikua watoza ushuru, wanasiasa, wavuvi wa samaki n.k.
Biblia iliandikwa miaka zaidi ya 1500 ilopita.

MAAJABU NA UPEKEE WA BIBLIA

ndicho kitabu pekee kilichosomwa na watu wengi dunian na kununuliwa na watu wengi dunia.
ndicho kitabu pekee ambacho Gharama yake huwa Haichuji.
ndicho kitabu pekee Kilichopigwa vita kuliko kitabu kingine.
ndicho kitabu pekee kinachoeleza yalopita,yaliopo na yajayo
Ndicho KITABU CHA KWANZA KUCHAPISHWA NA MASHINE YA KUPRINT mwaka 1450
Ndicho kitabu pekee kilichotafasiriwa na Lugha zaidi ya 14000 hapa duniani.
ndicho kitabu kilichoandikwa na waandishi wengi 40 nabado kikaonekana kama kiliandikwa namtu mmoja tuu.
Ndicho Kitabu pekeee ambacho Hamna hata Nukuta moja ilowahi badilishwa (1947 uko Israel yaligunduliwa Mabaki ya Maandiko ya biblia , Nayalivyochunguzwa ikagungulika yaloandikwa humo, ndio yaloandikwa katika biblia tulizonazo) ...N.B Ingawa sasa kumekuwepo majaribio ya kubadilisha nakuondoa hata kuongeza maneno ya Biblia.


Maajabu ni Mengi sana


SASA HAYA NDIO MAJARIBIO YALOFANYWA ILI KUIVURUGA BIBLIA .
na sasa mtajiuliza km ni yauongo kwann wajaribu kuivuruga???? Km iliandikwa na masons kwann wajaribu kuivuruga??? Km inavisa vya kubuni ,kwann wajaribu kuivuruga??? ( Uongo unachekesha sanaa wakuuu ,yaan shetan nimuongo wa waziwazi .

Tuendeleee na Majaribio

Yeremia 36:21-32 jaribio lakwanza ,ambalo Mfalme Joakim wa Yuda, Alichukua maandiko ya nabii Yeremia nakuyatupa ktk Moto.... Lkn huwez amin.. nabii Yeremia alikuja kuyaandika upya na wala hakuacha hata neno moja yaan alicopy nakupaste tu ..Mungu ni Mungu

mwaka wa 200 AD ,dunia chin ya Antiochus mtawala wa kigreek, baada ya kulibomoa Hekalu ( hili ambalo mpaka leo ndio kuna msikiti na ndio mzozo wa Israel na warabu) , jamaa alijenga hekalu la Kuabudu Miungu watu, Na Akaamuru BIBLIA ZOTE ZICHOMWR MOTO ,napia akasema "YOYOTE ATAKAYEMILIKI BIBLIA ATAUWAWA "........ ( kasome kitabu cha kwanza Maccabees 1:56-57 ) ....... Aliua sana watu, alichoma biblia sanaa ,L

1320 Mtumishi John Wycliff huko Uingereza aliamua kuhakikisha anagawa biblia kwa Waingereza , biblia hii ilotafasiriwa kingereza Ilipingwa na Ma askofu na kumtuhum jamaaa Kuingilia mikakati ya kanisa.. Alikamatwa na Kuchomwa moto akiwa hai. Nawote walokua nabiblia hii ilotafasiriwa kingereza, walikamatwa na kuchomwa motoooo...LKN BIBLIA ILIISHI.

mwaka wa 1500 bwana William Tyndale Muingereza alitafasiri biblia kutoka ktk kingereza mpaka ktk lugha ya jamii yake , watu wengi wakaielewa sana..
 
Unaweza kuona kama kuna maneno wame nyofoa lakini siyo hivyo, lengo la mwandishi ni kuendana na lugha ya nyakati hizi. Unajua kuna kufaham kitu na kuelewa.
 
Mkuu MWANA ileje nimeelewa post yako na mimi hakuna mahala nimesema biblia ni kitabu kibaya concern yangu mimi ni kwanini Pseudipigrapha zilitolewa kwenye biblia ilihali sababu zilezile zilizopelekea kutolewa bado zipo kwenye baadhi ya vitabu vya kibiblia.

Na hii hoja sijaitoa mimi bali ni waandishi wa biblia ya NIV yaani harper-collins inc kundi la wanatheolojia miaka ya 60 walipoifanyia utafsiri upya biblia na kugundua makosa lukuki kwenye tafsiri ya KJV ndio kusema kwa mujibu wa NIV kama biblia ya KJV ilichakachuliwa na ndio imetumika kutafsiri biblia ya kiswahili kivipi sasa walitoa zile Pseudipigrapha na wakaacha vitabu vyenye utata vilivyoainishwa na NIV hadi kupelekea maneno 64,000 kufutwa kwenye biblia

Hapa tuna biblia mbili zote zinakinzana hivyo mnaposema tunapinga Biblia unakosea labda ungesema BIBLIA ZINAZOPINGANA ZINAKOSEA maana wao ndio walioleta huu mjadala sio akina sisi zitto junior so hamtutendei haki kutushambulia tunaoleta mijadala inapaswa muswashambulie KJV au NIV
 
Unaweza kuona kama kuna maneno wame nyofoa lakini siyo hivyo, lengo la mwandishi ni kuendana na lugha ya nyakati hizi. Unajua kuna kufaham kitu na kuelewa.
How can you explain this mkuu maana haijatolewa kweli???


Mkuu hili jambo ni serious tusilichukulie kiuwepesi.... Kuna mpaka bible inaitwa Today's New International Version ambayo imeweka gender balance kiasi kwamba maana nzima ya Biblia imetolewa mkishangaa mtakuta ishakuwa too late ntaiweka hapa hyo copy alafu utabaki mdomo wazi
 
Unasema kifungu hicho kinathibitisha kutokuwepo kwa Yesu Kristo...!Kwani ni Lazima Yesu aseme ukweli, ndipo aishi?

Mbona kuna watu wapo na wanasema uwongo na kufanya vichekesho pia.
Kama unasema Yesu hakuwahi kuwepo ni kwamba hakuwahi kuwepo fullstop.
Kumzungumzia tena Yesu ambaye hayupo ni kupoteza muda.
Kunukuu kifungu cha ovyo kwenye biblia sio kigezo cha kuto kuwepo kwa Yesu.
 
Hapa kuna kitu naona kama unataka kulazimisha mkuu.
Fact kuu. Wote NIV , KJv Douay (English version of Catholic Vulgate) hawajatoa kwenye origin manuscripts.
Ni translation of copies of origin. Naamini ni mpango wa Mungu origin zisiwepo maana mwanadamu hawachelewi kuziabudu. Ingawa Mungu ndiye anajua kwa nini zisiwepo.

Pamoja na tofauti zote hakuna tofauti au rekebisho kulingana na ukale wa origin copy zinazobadili fundisho au fact yoyote ya kwenye bibilia. Badala yake Wakati NIV inatoa vitu ambavyo kulingana ukale wa origin yake havirandani na zile za KJV lkn Bado kuna vitu ambayo kwenye manuscript za KJV vimo lkn manuscript za kale zaidi zalichazimo.

Ila ufanano ni kwamba manuscript zote maelfu za kale Bila kujali utofauti wa nyakati hazipingani kwa maana ya mafundisho.
Hivyo hakuna atakayeshindwa kumcha Mungu kisa version ya bibilia. Kwa scholars na wahubiri wanashauriwa kuwa na version mbalimbali kulisha waumini waumini mafundisho kwa kina chake Ikibidi kusoma na histori.

Apokrifa ktk Old KJV . Hazikuwa zinatambulika kama inspired books hata humo kwenye KJv. Hata kwa Vulgate Jerome hakuzitambua kama inspired books achilia mbalimbali wayahudi wenyewe.

Sababu ya kutenga hayo mavitabu yote na sababu hizo kutofanana na hoja za KJv na njv ni Doctrinal contradiction na pia vinakinzana na mengi ya bibilia kimafundisho sio kitextual differences. Na sababu nyingine nyingi za msingi .

Hiii ni tofauti na Quran ambayo source ni Moja tu yaani kiongozi wa caliphate Uthman aliyeteketeza manuscript zote hivyo kukifany vitabu hivyo kuwa cha kutiliwa Shaka maneno yake kuliko vitabu vingine vya imani.

Hivyo maarifa yote the ya 66 books yanaweza kuwa historically true but spiritually false because they contradicts with fundamental biblical facts
.lakini pia vingi vinatuhumiwa kuwa ni vya kubumbwa na viko backdated makusudi ili kujitaja usikivu wa watafiti wa maarifa yoyote yanayotoa mwanya wa kupotosha msingi mkuu wa kimafundisho ya bibilia.

Utofauti wa kimasimulizi na uwasilishaji wa synoptic gospel books za wskina mathayo au Marko haziondoi uhalali wa facts za bibilia na wokovu kupitia Yesu huku utii wa amri kumi (exodus 20) ukisisitizwa kwa wanaomuamini Yesu maana hakuwakomboa ili wake wakaidi wa kanuni za mbinguni.


Ubarikiwe[/QUOTE]
 
Mkuu hii mada ni moto sana na inahitaji watu watulivu kifkira kuelewa. MDO 2:17
"Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto."
 
Asante sana mkuu mm napenda san mtu anaefikiri kuliko mfia imani...wewe ni mtu anayefikiri,napenda sana biblia vile inaripoti mambo ambayo kwakweli inaonyesha wazi watu walioandika walikua watu wa kawaida kwa kisa hiki Marko anatuonyesha wazi aliemtukana Yesu alikua mmoja hasa ikiwa mtu anapendezwa zaidi na idadi kuliko tendo lenyewe,inaonekana Mathayo alionyesha tu kutukanwa kwa Yesu hakujikita kuhusu nani alimtukana,kwa ujumla wote wanaonyesha Yesu alitukanwa.
 
Tafsiri ya NIV inakanganya pia. Inatetea imani ya Utatu na inaikataa na hata kuyafuta maandiko mengi muhimu. Maelezo mara nyingi yamekuwa yakituama uwazi na kupuuzia ugumu zaidi. Baadhi ya bango kitita yanathamani hata hivyo na yanaweza kutumika vizuri sana.



Tafsiri bora kabisa ya KJV unayoweza kuitumia ni ile ya Companion Bible iliyoandikwa na Bullinger. Uandishi wake ni mzuri sana isipokuwa pale inapouelezea Uungu au Kronolojia. Hizo zote ameziosea. Hatimaye baada ya uandishi wa Biblia kukamilika na ikachapishwa, aliyagundua makosa yake aliposhawishiwa na A. E. Knock. Hata hivyo, alikuwa amezeeka sana na akamwachia imaliziwe na Knoch, ambayo ameifanya kwenye tafsiri ya Agano Jipya ya the Concordant Literal New Testament. Kwa hiyo, andiko hilo ni la muhimu sana.



Nyongeza hizi yana thamani bora sipokuwa, mara nyingine tena, kwa kronolojia na maelekezo yametuama kwenye hilo. Tafsiri ya Kiyunani ya The Marshall’s Greek English Interlinear ni nzuri na kama tafsiri ya toleo la RSV ni bora zaidi. Na sasa wanajaribu kuichapisha hii na tafsiri ya NIV zaidi kuliko ile ya RSV, ambayo ni aibu.



Tafsiri ya Green’s Interlinear Bible ni Interlinear nzuri pamoja na ile ya Strong’s ikihesabiwa inaweza kutumiwa kwa Agano la Kale. Agano Jipya limetuama kwenye tafsiri ya Receptus na kwa hiyo unaweza kuitumia tafsiri ya Marshall’s pia. Notisi za Bullinger inashughulikia matatizo yaliyo kwenye tafsiri ya Receptus kwenye bango kitita, kwenye Agano Jipya kwenye tafsiri ya the Companion Bible. Kitabu cha ufafanuzi cha Kiyahudi cha Agano la Kale ni ya Soncino. Inaendana na tafsiri ya Masoretic Text na haina mwingiliano lakini zaidi ni Kiingereza kizuri kilichomo. Ina nukuu za maandiko ya marabi, zinazoweza hata kukufanya hata ujihisi kuchoshwa sana kuliko kama ungekuwa na NIV kwa kupuuzia kwake kwa makusudi na marabi fulani na kushindwa kwa wengine kutenda kwenye kweli iliyo wazi ya kimasihi. Kwenye maeneo karibu mengi kuna majarida yaliyoandikwa yakitilia maanani maandiko hayo. Ni matarajio kuwa tutakuwa tunaweza kuzalisha andiko zuri lililoandikwa kwenye Mradi wa Kimataifa wa Biblia kwa kupitia Machapisho ya CCG, siku zijazo.



Hakuna kitabu cha Ufafanuzi zinazohusu Vitabu vya Apocrypha/Deuterocanonical vilivypoandikwa na Collins, ambavyo vitakusaidia pia wewe kwa kuvifanyia rejea. Tafsiri ya the New Oxford Annotated RSV pia ni nzuri pamoja na kwamba haijanukuu ila inaendana nayo.
 
hivi ni kina nani hasa waliokaa chini na kuviingiza vitabu vyote vile? tungewajua na kujua historia zao huenda tungepata mwanga
Roman Empire - Later Roman Catholic Church
Ni kweli mkuu sijakataa kina hekima sasa kama NIV inasema KJV imechakachuliwa tuchukue lipi tuache lipi?? Nani ni sahihi kati yao na biblia zote mbili zinatumika??
Bila kupoteza maana halisi Mungu ni kweli, Yesu Kristo ni kweli. Ila kuna genge la watu fulani mahali fulani waliamua kuchakachua nyaraka mbali mbali zilizoandikwa na waliotangulia kwenye imani... kwa nia ovu kabisa ya kupotosha au kuleta sintofahamu inayoendelea leo... madhehebu lukuki kitabu kimoja kila mtu ana mafunuo yake kwa wakati wake. Mungu mmoja Yesu Kristo mmoja... Bado waumini hamshtuki kuhisi something isn't OK?
 
[/QUOTE]
Mkuu nimekusoma ila nina maswali machache unaposema haina madhara hizo tafsiri kutofautiana nnapata kigugumizi kidogo mfano za juu ni KJV na chini ni NIV
Luke 4:4
KJV Man shall not live by bread alone, but by every word of God.
NIV Man does not live on bread alone.

Mt 25:13
KJV Ye know neither the day nor the hour wherein the Son of man cometh.

NIV You do not know the day or the hour.

Mt 18:11
KJV For the Son of man is come to save that which was lost.
NIV: wamefuta

Ac 23:9
KJV:Let us not fight against God.
NIV: wamefuta

Rom 13:9
KJV:Thou shalt not bear false witness.
NIV:wamefuta

1Pe 1:22
KJV:Ye have purified your souls in obeying the truth through the Spirit.

NIV:you have purified yourselves by obeying the truth.

Hii ni mifano tu ila keywords nyingi zimefutwa kwenye NIV sasa kwa mistari kama hii huoni inaleta tofauti nzima kwenye baadhi ya mafundisho ya Biblia??

2. Sikulazimisha kuwa NIV imetumia original texts bali vyanzo vya NIV ni vya zamani zaidi mfano dead sea scrolls hivyo kwa wengi tutakubali earlier texts are more credible kuliko later texts?? Ikimaanisha NIV kma madai yake ni halisi ni kwamba textus receptus na source zingine walizotumia KJV huenda zina mashaka ndio maana mistari yake imefutwa ndio najengea hoja kwamba kama NIV wanadai kwa ushahidi wa kinyaraka kuwa KJV ilitumia vyanzo vilivyochakachuliwa je credibility ya kuvitoa pseudepigraphi na apocrypha kutoka kwenye bible wanatoa wapi??

3. Kingine nilieleza kwamba wanatheolojia 80% wanakubali kuwa kuna barua za paulo ziliandikwa na mikono tofauti kwa gap la miaka mingi ikimaanisha kuna uwezekano kilieditiwa na wanafunzi wake ndio maana wanaviita disputed letters ambazo zina uzito sawa na wanavyoviita pseudepigraphi zingine, pia Isaya 56 hadi 66 kiliandikwa baadae sana baada ya kutoka utumwani na unknown source bila kusahau jeremiah to mention a few. Sasa nachouliza kama wana ushahidi kuwa isaya au Jeremiah kilichakachuliwa na kuongezwa maneno kinyemela kivipi wakakitoa Esdras 4 kwa hoja hiyo hiyo au Book of Abraham kinachoelezea hatma ya maisha ya Cain na jinsi kizazi chake kilivyopona gharika?? Bila kusahau nature ya misri kukaliwa na watu weusi??

Napenda kujua kwanini kuna dalili za double standards hapa, ukinielewesha hapa utakuwa umenitoa kwenye sintofahamu kubwa sana
 
Yohana anamshudia hivi.
12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;

13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.

14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
 
MKUU SIJAWAONA SHAKA YOYOTE NA ALLAH KAYASEMA HAYO AKIWA NA UHAKIKA KUWA SITAKUWA NA SHAKA,SIO MTU KUWA NA SHAKA TU PIA KAMA UNAHISI SIO KITABU CHAKE UMEPEWA RUHUSA YA KULETA KITABU KINACHOFANAN NA IYO QURAN WALAU AYA MOJA.....HALAFU HAKUNA KITABU KINAITWA BIBLE/BIBILIA KUNA TORAT ZABUR NA INJIL...HAIJAWAH TOKEA SHAKA HADI KUVIENDEA IVYO VIPANDE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…