Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Mkuu hii mada niliweka Rai yangu mapema kabisa kuwa nachokoza mada ili kupata maarifa na wala sikusema biblia imekosewa au ina mapungufu ila nimehoji kwamba kwanini sababu zilezile zilizopelekea vitabu nilivotaja kutolewa hazijatumika kuvitoa vingine vyenye kasoro hizo hizo??

Ni vizuri tusome kwansa historia ya Biblia kabla hatujaanza kukosoa maana unaposema kilivuviwa nani amesema hakijavuviwa??? Nachohoji nini kilipelekea ile kamati ya Constantinople kupunguza hivyo vitabu ilihali kasoro walizoainisha ndio hizo hizo zimepatikana kwenye biblia

Hapa ndio mzizi wa mada, ni vizuri tuijadili kwa utulivu na kueleweshana kuliko kuanza kuitana WAFUASI WA SHETANI kisa kuhoji tu hatutafika kwa kweli tujifunze kujihusisha na mjadala ya faida kuliko ushindani.

Ni hayo tu
Bwana @zittojunior nafahamu namna unavyoheshimika hapa jf kwa mada tata na vikirishi ila nikusaidie kitu kimoja cheza na mipaka yako katika mambo yanayomuhusu Mungu yaani hapa sizungumzii dini wa dhehebu.

Sijaona utata katika vilivyoandikwa katila bibli kwakua ni vitu vya kiimani na si kisayansi kwamba vinahitaji scientific proof.... Huweizi pata.
Ninauhakika hujisoma biblia ukaielewa nnauhakika hii hoja umeiokota.... Ni kwamba mi si muandishi mzuri ila nishakutana na hoja hizi wakati nafuatilia imani zilizo kinyume na Mungu.....

Ukisoma biblia Agano la kale na jipya limetofautiana kimapokeo tuu lakini kusudio la Mungu lilikua moja tu na bado liko vile vilehata sasa.

Tambua baraza lilipata mamlaka ya kipi kiingie kipi kitoke kutoka kwa Mungu (uvuvio) na huo ndio mpaka wangu wa kuhoji kibinadamu zaidi ya hapo najitahidi nifike peponi nikamuulize Mungu mwenyewe.
 
Wee unahisi ni siri ipi endapo huku utakosa majibu
Nachohisi ni kwamba kuna baadhi ya mambo tunafichwa na kikundi cha watu wachache maana kuna vitabu vilitolewa kwa sababu A na vingine vyenye kasoro hiyo hiyo viliachwa. Nahisi ni cover up, uzi ujao ntaongelea Injili ya Yuda Iskariot na Barua ya paulo kwa laodecia nafikiri utapata picha nachodai tunafichwa ni kipi.
 
Mkuu siri ni hyo kwamba kwanini baadhi ya vitabu vimetolewa kwa sababu X and Y na vingine vimebakizwa ilihali vina madhaifu hayo hayo ya X na Y hapo ndipo kuna siri ambayo natamani wote tui unlock hapa maana kuna uwezekano wachache wanaifahamu kwa gharama ya kupotosha wengine na hyo ndio SIRI inayozungumzwa hapa

Karibu tueleweshane

Nadhani hapo sio Siri Bali ufafanuzi maana kusema vitabu vimetolewa sio universal set ya mjadala kwa sababu Catholic na baadhi ya Orthodox wanaamini havijatolewa engine tunaamini havina sababu ya kuwepo kwa sababu ya hizo za kwenye mfano na nyingine ngoja zinazotumiwa na Muslim kuponda bibilia kuwa inacontradictions. Hivyo sioni kama kuna elements za Siri Bali kila upande utoe ufafanuzi.

Kuhusu tofauti ya versions sioni kama ni utata ukubwa ikiwa wazo kuu ni Moja. Na pia sio ukweli kwamba mkusanyaji wa kwanza wa bibilia ni Jerome. Mfano Erasmus alitafsiri kutaka kwenye origin na sio Vulgate. KJV vile vile.

Kuhusu kuwemo kwa apokrifa kwenye Vulgate ya Jerome. Jerome had anafanya makusanyo hayo hakuwahi kuyahesabu au kuyapa hadhi sawa na maandiko mengine matakatifu.

Kanisa Katoliki ndoo liliamua kuyatakatifisha na true baadae akatii maamuzi yao licha ya ukweli kwamba hata wayahudi mwenyewe ambayo ni wahusika wakuu hawakuwa wanayaona kama ni matakatifu zaidi ya kuchukuliwa kama makusanyo ya kihistoria zaidi.

Nimeweka nyama kidogo kuchochea mjadala mkuu.
 
Kuhusu bible ni kitabu kipana sana yani tukisema waweke kila jambo ambalo lilikuwa linafanyika hicho kitabu kisingekuwa na uwezo wa kubebeka kwa mfano mathayo angesema aandike yote aliyoyaona wakati yuko na yesu kile kitabu chake kisingeishia pale hivyo hivyo kwa mitume wengine kina Paulo, Luka, Marko n.k

Kutofautiana kwa matukio ni kutokana na uandishi wa kila mwandishi kutokana na uandishi wake lazima tukumbuke kuwa bible haijapangwa SERIALLY kusema imeanza tukio la kwanza hadi la mwisho ndio maana utashangaa kitabu cha Ayubu kilianza kuwekwa kwenye bible kabla ya vitabu vitano vya Musa sasa hapa ndipo panapochanganya watu wengi wanadhani wakisoma bible mwanzo hadi ufunuo basi wanajua matukio yote yamepangwa kama unavyoangalia series au tamthiliya ya jumba la dhahabu ila bible haipo hivyo na hii ni kwa sababu ina waandishi mbali mbali kwa mfano wakati Luka anaandika hakuweza kumwambia mathayo kuwa mi naandika hiki we endelea sehemu fulani haikuwa hivyo kila mtu aliandika kivyake baada ya miaka mingi kupita Yale maandiko yakaja kukusanywa maana mengi hayakuwa kwenye karatasi yalikusanywa yakawekwa pamoja hata hivyo sio yote maana yangekuwa mengi sana imagine kitabu kimoja cha Marko kingekuwa kama 'chand' ya physics hapo bado cha Luka, Mathayo, Musa, n.k so kuachwa kwa vitabu sio jambo la ajabu ingewezekana kuviweka vyote
 
Bahati yako, nimechoka.

Nakuahidi, nitaleta uzi wa kweli kutoka katika wanatheolojia sahihi.

Achen kupotosha watu.
Toka kuumbwa kwa ulimwengu. biblia sahihi ni ya

King james version na ambayo imeandikwa na waandishi wapatao 40 yaan mitume na manabii.
Na biblia hii ina vitabu 66 .

Acha mbwembwe....
Mnadanganya wasojua ukweli nakutaka kuufatilia na maandiko yenu ya porojo.

Sasa siku nitaletea HISTORIA SAHIHI YA BIBLIA, MPAKA KING CHARZ WA UFARANSA ALIOJARIBU KUIFUTILIA MBALI LKN AKASHINDWA .
 
Hata wakikoment X 1,000 hawawezi kujibu hoja zako zaidi ya kusema ni suala la kiimani/fumbo la imani

Sasa imani gani inakuwa na mafumbo kama maneno ya kwenye khanga ?
haha Haa na kwanini iwe na mafumbo" wakati mungu anataka umjue"?? yaani mafumbo kibao" kushinda hata vitendawili bwana
 
Bwana @zittojunior nafahamu namna unavyoheshimika hapa jf kwa mada tata na vikirishi ila nikusaidie kitu kimoja cheza na mipaka yako katika mambo yanayomuhusu Mungu yaani hapa sizungumzii dini wa dhehebu.

Sijaona utata katika vilivyoandikwa katila bibli kwakua ni vitu vya kiimani na si kisayansi kwamba vinahitaji scientific proof.... Huweizi pata.
Ninauhakika hujisoma biblia ukaielewa nnauhakika hii hoja umeiokota.... Ni kwamba mi si muandishi mzuri ila nishakutana na hoja hizi wakati nafuatilia imani zilizo kinyume na Mungu.....

Ukisoma biblia Agano la kale na jipya limetofautiana kimapokeo tuu lakini kusudio la Mungu lilikua moja tu na bado liko vile vilehata sasa.

Tambu baraza lilipata mamlaka ya kipi kiingie kipi kitoke kutoka kwa Mungu (uvuvio) na huo ndio mpaka wangu wa kuhojik

Yaani wewe jamaa ni wa hovyo, kelele nyingi ila unashindwa kutoa ushahidi wa kupinga hoja ya mtoa mada.. Ni bora ukapige goti usali..
 
Hakuna tofaut kati ya vitabu vya hekaya kama alfu lela ulela na hivi vitabu(biblia,Quran nk) vyote ni hadith za kutunga tunga tu
Wizi mtupu" uwongo mwingi" mnooo" kuna jamaa yangu mmoja majuzi aliniambia eti Muhammad alikuwa na miujiza hakuwahi kuwa na kivuli" Aisee ilibaki kidogo nimzabe makofi" ila bahati yake tulikuwa tuna chat watsaap"" yaani mtu amedanganywa" Kama chizi kiasi kile
 
Wewe unaisi Ni mambo Gani ayo tunayo fichwa
Tunafichwa content yote iliyopo kwenye hivyo vitabu vilivyotolewa mfano life of Adam and eve nimekisoma kinaongelea kwa mapana yaliyotokea kuanzia uumbaji hadi kifo cha Adam....

Ama Kitabu cha Henoko kinavyoeleza muingiliano kati ya wanadamu na elimu ya kucontrol Roho zingine za mbinguni na kuzimu,miujiza,na sayansi zingine za kiroho ama ukweli juu ya maisha ya Yesu kwenye Injili ya Yuda ukivisoma hivi vitabu vina concept nyingi sana ila kwakuwa hazitambuliwi na Biblia wengi hawavisomi hivyo kuacha yaliyozungumziwa humo kufanyiwa kazi na wachache

Sijui unapata concept yangu mkuu
 
Bahati yako, nmechoka.

Nakuahidi ,nitaleta uzi wa kweli kutoka katika wanatheolojia sahihi.

Achen kupotosha watu.

Toka kuumbwa kwa ulimwengu. biblia sahihi ni ya

King james version na ambayo imeandikwa na waandishi wapatao 40 yaan mitume na manabii.

Na biblia hiii ina vitabu 66 .

Acha mbwembwe....

Mnadanganya wasojua ukweli nakutaka kuufatilia na maandiko yenu ya porojo.

Sasa siku nitaletea HISTORIA SAHIHI YA BIBLIA, MPAKA KING CHARZ WA UFARANSA ALIOJARIBU KUIFUTILIA MBALI LKN AKASHINDWA .
kulikuwa hakuna haja ya kejeli na dharau, unaweza kuwa na hoja ukaileta wote tujifunze bila vitisho.Anyway kwa kuwa utakuja na majibu basi usisahau yafuatayo

Nategemea utakuja na ushahidi kuwa Isaya,wakolosai na nyinginezo ziliandikwa wakati mmoja na sura zingine maana unasema napotosha wakati wanatheolojia wengi wanakubaliana kuwa kuna utata kwenye issue ya waandishi na muda uliotumika kuandaa kitabu husika

pia nategemea uje na jina la alieandika kitabu cha waebrania

Pia uje na ushahidi kuwa source ya KJV ni ya zamani zaidi kuliko NIV na version zingine

Pia uje na taarifa kwanini biblia inaquote Pseudipigrapha zingine kma book of jasher na book of enoch ila kwenye biblia haviwekwi

Pia utanisaidia kwanini baadhi ya taarifa kwenye biblia zinakinzana ama misplaced iwe KJV au NIV....

Ntashukuru kwa hayo
 
Mkuu,

Mungu alishaona jinsi vitabu vyake vinavyochezewa na mikono ya waandishi... ukimpa mwanadamu kazi ya kujadili maandiko jua shetani nae hatocheza mbali nao,lazima atie fitina zake ndio kama hivyo inavyothibitishwa..

Mungu kwa kuliona ilo akaleta kitabu kingine na kuahidi kukilinda kutoka ktk mikono ya waandishi naam yametimia quran hata utoe "a" inagundulika maana iko memorized ktk vichwa yaani humdanganyi mtu...

pia quran hata ikatafsiriwa ktk lugha gani lazima uiambatanishe na lugha yake ya asili."hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu"(quran 2:2)."hakika sisi ndio tulio teremsha ukumbusho huu, na hakika sisi ndio tutao ulinda."(quran 15:9)

Chakuzingatiwa watu wasome historia za mambo mengi yamefunikwa kwa maslahi yaaa.......
 
biblia haijakosewa hata nucta moja tatzo umegoogle tafit zisizofikiwa muafaka
Mkuu wapi kunahitaji google mkuu?? Hapo nimeweka NIV imefuta mistari zaidi ya 100 ya KJV ikisema imechakachuliwa sasa google inaingiaje hapo?? Na wapi nimesema biblia imekosewa?? Labda ungehoji hao NIV walivyofuta hiyo mistari walifanya hivyo baada ya kugoogle pia? !!!
 
Sasa napata mwanga inawezekana roman catholic wapo sahihi asilimia kubwa na vitu wanavyovifanya maana hivyo vitabu hawakuvitenga sana...........
 
Sasa napata mwanga inawezekana roman catholic wapo sahihi asilimia kubwa na vitu wanavyovifanya maana hivyo vitabu hawakuvitenga sana...........
Kuna mambo mengine unaweza kuta yanafanywa na kanisa katoliki lakini kwenye bible hayapo, wanapoyatolea ni huko huko kwenye vitabu vingine(Wanaita Mapokeo)
 
Duh mkuu nimedanganya tena??? Mbona nimeweka hoja zao..... Ni hivi NIV walitumia texts za nyuma zaidi ila KJV imetumia more recent scripts sasa basi hao NIV wakasema KJV sio credible ndio wakafuta ile mistari sasa unaposema nia yao sielewi unauliza nini maana walikuja na ushahidi wa kihistoria kisayansi na kihoja ndio maana biblia yao imekubalika kutumika hata leo ndio maana nikaleta hoja humu ili sasa kama unajua chochote ukimwage humu ila kuanza kusema nadanganya mara sijui NIA YAO, unakuwa hutendei haki huu uzi.

Eleza unachokifahamu kwa faida ya wote tuache shutuma na kejeli, karibu
Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inafafanuliwa na shirika la wazazi wa Mashahidi wa Yehova (Shirika la Mnara wa Doria) kama "tafsiri ya Maandiko Matakatifu yaliyotoka moja kwa moja kutoka kwa Kiebrania, Aramaic na Kigiriki katika Kiingereza cha kisasa na kamati ya mashahidi waliotiwa mafuta wa Yehova." Tafsiri Mpya ya Ulimwengu ni kazi isiyojulikana ya "Kamati ya Tafsiri ya Biblia Mpya ya Ulimwengu." Tafsiri Mpya ya Ulimwengu ni ya kipekee kwa kitu kimoja — ni jitihada za kwanza za utaratibu wa kuzalisha tafsiri kamili ya Biblia iliyohaririwa na kurekebishwa kwa madhumuni maalum ya kukubaliana na mafundisho ya kikundi. Mashahidi wa Yehova na Shirika la Mnara wa Doria waligundua kwamba imani zao zilikuwa kinyume na Maandiko. Kwa hivyo, badala ya kufuata imani zao kwa Maandiko, walibadilisha Maandiko kukubaliana na imani zao. "Kamati ya Tafsiri Mpya ya Biblia ya Ulimwengu" ilibadilisha Andiko lolote ambalo halikubaliana na Teolojia ya Mashahidi wa Yehova. Hii inaonyeshwa wazi kwa ukweli kwamba kama matoleo mapya ya Tafsiri Mpya ya Ulimwengu yalichapishwa, mabadiliko zaidi yalifanywa kwenye maandiko ya kibiblia. Kama Wakristo wa kibiblia waliendelea kuelezea Maandiko ambayo yanaelezea waziwazi uungu wa Kristo (kwa mfano), Shirika la Mnara wa Dori lingechapisha toleo jipya la Tafsiri Mpya ya Ulimwengu na Maandiko hayo yamebadilishwa. Ifuatayo ni baadhi ya mifano maarufu zaidi ya marekebisho ya kimataifa:

Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inatafsiri neno la Kigiriki neno staurós ("msalaba") kama "kigingi cha mateso" kwa sababu Mashahidi wa Yehova hawaamini kwamba Yesu alisulubiwa msalabani. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu haitafsiri neno la Kiebrania sheol au maneno ya Kigiriki hades, gehenna, na tartarus kama "jahannamu" kwa sababu Mashahidi wa Yehova hawaamini kuzimu. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inatoa tafsiri "uwepo" badala ya "kuja" kwa neno la Kigiriki parousia kwa sababu JW anaamini kwamba Kristo amekwisha rudi mapema miaka ya 1900.

Katika Wakolosai 1:16, Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inaweka neno "ingine" licha ya kuwa halipo kabisa kutoka kwa maandishi ya Kigiriki ya awali.Inafanya hivyo kutoa maoni kuwa "vitu vingine vyote" viliumbwa na Kristo, badala ya kile ambacho maandiko inasema," vitu vyote viliumbwa na Kristo." Hili ni kukubaliana na imani yao kwamba Kristo ni mtu aliyeumbwa, ambayo wanaamini kwa sababu wanakana Utatu.

Tafsiri Mpya ya Ulimwengu haitafsiri maneno sawa ya Kigiriki mahali pengine katika Injili ya Yohana kwa njia sawa. Ni wazi kabla ya kuona tu, kukataa uasi wa uungu wa Kristo ambao unalazimisha Shirika la Mnara wa Doria kutafsiri kikizani maandishi ya Kiyunani, hivyo kuruhusu kosa lao kupata mfano halali kwa wale wasiojua ukweli.

Ni waza kabla ya kuona tu ya Mnara wa Doria, imani ya uasi ambayo iko nyuma ya tafsiri isiyo na uaminifu na kizani ambayo ni Tafsiri Mpya ya Ulimwengu. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu kwa hakika sio toleo sahihi ya Neno la Mungu. Kuna tofauti ndogo kati ya tafsiri zote kuu za Kiingereza za Biblia. Hakuna tafsiri ya Kiingereza iliyo kamili. Hata hivyo, watafsiri wengine wa Biblia hufanya makosa madogo katika kutafsiri maandiko ya Kiebrania na Kigiriki kwa Kiingereza; Tafsiri Mpya ya Ulimwengu kimakusudi hubadilisha tafsiri ya maandiko ili kuendana na teolojia ya Mashahidi wa Yehova. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu ni upotovu, sio toleo la Biblia.
 
Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inafafanuliwa na shirika la wazazi wa Mashahidi wa Yehova (Shirika la Mnara wa Doria) kama "tafsiri ya Maandiko Matakatifu yaliyotoka moja kwa moja kutoka kwa Kiebrania, Aramaic na Kigiriki katika Kiingereza cha kisasa na kamati ya mashahidi waliotiwa mafuta wa Yehova." Tafsiri Mpya ya Ulimwengu ni kazi isiyojulikana ya "Kamati ya Tafsiri ya Biblia Mpya ya Ulimwengu." Tafsiri Mpya ya Ulimwengu ni ya kipekee kwa kitu kimoja — ni jitihada za kwanza za utaratibu wa kuzalisha tafsiri kamili ya Biblia iliyohaririwa na kurekebishwa kwa madhumuni maalum ya kukubaliana na mafundisho ya kikundi. Mashahidi wa Yehova na Shirika la Mnara wa Doria waligundua kwamba imani zao zilikuwa kinyume na Maandiko. Kwa hivyo, badala ya kufuata imani zao kwa Maandiko, walibadilisha Maandiko kukubaliana na imani zao. "Kamati ya Tafsiri Mpya ya Biblia ya Ulimwengu" ilibadilisha Andiko lolote ambalo halikubaliana na Teolojia ya Mashahidi wa Yehova. Hii inaonyeshwa wazi kwa ukweli kwamba kama matoleo mapya ya Tafsiri Mpya ya Ulimwengu yalichapishwa, mabadiliko zaidi yalifanywa kwenye maandiko ya kibiblia. Kama Wakristo wa kibiblia waliendelea kuelezea Maandiko ambayo yanaelezea waziwazi uungu wa Kristo (kwa mfano), Shirika la Mnara wa Dori lingechapisha toleo jipya la Tafsiri Mpya ya Ulimwengu na Maandiko hayo yamebadilishwa. Ifuatayo ni baadhi ya mifano maarufu zaidi ya marekebisho ya kimataifa:

Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inatafsiri neno la Kigiriki neno staurós ("msalaba") kama "kigingi cha mateso" kwa sababu Mashahidi wa Yehova hawaamini kwamba Yesu alisulubiwa msalabani. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu haitafsiri neno la Kiebrania sheol au maneno ya Kigiriki hades, gehenna, na tartarus kama "jahannamu" kwa sababu Mashahidi wa Yehova hawaamini kuzimu. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inatoa tafsiri "uwepo" badala ya "kuja" kwa neno la Kigiriki parousia kwa sababu JW anaamini kwamba Kristo amekwisha rudi mapema miaka ya 1900. Katika Wakolosai 1:16, Tafsiri Mpya ya Ulimwengu inaweka neno "ingine" licha ya kuwa halipo kabisa kutoka kwa maandishi ya Kigiriki ya awali.Inafanya hivyo kutoa maoni kuwa "vitu vingine vyote" viliumbwa na Kristo, badala ya kile ambacho maandiko inasema," vitu vyote viliumbwa na Kristo." Hili ni kukubaliana na imani yao kwamba Kristo ni mtu aliyeumbwa, ambayo wanaamini kwa sababu wanakana Utatu. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu haitafsiri maneno sawa ya Kigiriki mahali pengine katika Injili ya Yohana kwa njia sawa. Ni wazi kabla ya kuona tu, kukataa uasi wa uungu wa Kristo ambao unalazimisha Shirika la Mnara wa Doria kutafsiri kikizani maandishi ya Kiyunani, hivyo kuruhusu kosa lao kupata mfano halali kwa wale wasiojua ukweli. Ni waza kabla ya kuona tu ya Mnara wa Doria, imani ya uasi ambayo iko nyuma ya tafsiri isiyo na uaminifu na kizani ambayo ni Tafsiri Mpya ya Ulimwengu. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu kwa hakika sio toleo sahihi ya Neno la Mungu. Kuna tofauti ndogo kati ya tafsiri zote kuu za Kiingereza za Biblia. Hakuna tafsiri ya Kiingereza iliyo kamili. Hata hivyo, watafsiri wengine wa Biblia hufanya makosa madogo katika kutafsiri maandiko ya Kiebrania na Kigiriki kwa Kiingereza; Tafsiri Mpya ya Ulimwengu kimakusudi hubadilisha tafsiri ya maandiko ili kuendana na teolojia ya Mashahidi wa Yehova. Tafsiri Mpya ya Ulimwengu ni upotovu, sio toleo la Biblia.
Mkuu usichanganye New International Version na New World Translation ni vitu viwili tofauti kabisa, NIV inatumika na protestants ila NWT ndio inatumika na Jehovah witness.

So bado swali linasimama je NIV na KJV ipi ni sahihi??? Na kama NIV imekubalika kuwa sahihi nini hatma ya waliotumia biblia iliyochakachuliwa kwa miaka zaidi ya 2000?? Na credibility ya biblia haipo mashakani kama tumeshajua kuna uwezekano wa kuwepo mistari iliyoongezwa?? Kumbuka pia maneno zaidi ya 64,000 yamefutwa na mistari zaidi ya 100 imefutwa sasa basi hatma ni ipi kwa uhalali wa biblia kama kitabu muhimu kwa rejea za wakristo
 
Back
Top Bottom