Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Mkuu uzi ni wa mwaka 2018 lakini nina swali hapa.

Hivi ni nani anayehusika kubadiri maandiko kama wakiona kwamba kuna kitu hakiko sawa??
Au unapoandika "hawakuweka kitabu cha Enoch " unakuwa unarefer wakina nani hao??
Nakua na refer na watu wa kanisa la kwanza waliohusika na new testament canon yaani mfumo wa kutambua vitabu vya agano jipya mfano Council of Jamnia iliyokaa huko Judaeah miaka kadhaa baada ya Yesu kufariki possibly 120 AD.

Agano la kale though wayahudi wanadai ni fixed canon ya vitabu 39 ila kuna compilation mfano hao wa Alexandria miaka kadhaa kabla ya Yesu waliotafsiri Agano la kale kuwa ya kigiriki waliamua kuwa na vitabu kadhaa zaidi. Pia kuna councils za orthodox huko Ethiopia zikaamua kutafsiri Biblia kuwa na vitabu 84.

Kwahiyo naposema "walioamua" naongelea hizo council kma za Alexandria, Trent,Nicaea,Jamnia n.k na pia kanisa la kwanza chenye fathers kama polycarp,Ignatius,clement n.k ambao wangeweza influence inclusion ya baadhi ya vitabu kwa bible

Pia kuna reformist wakanisa kama Martin luther aliyejitenga na Roman catholic naye akaja na canon yake ambayo iliengua vitabu 6 vya deuterocanonical hivyo kuleta biblia ya vitabu 66, catholic wakabaki ma 72 bado Orthodox Tawahedo ya Ethiopia ikawa na 84, Eastern orthodox ina canon tofauti pia iwe vitabu 66 zingine mpaka 70.

Kwahiyo waasisi pia wa hizo sects nao nawahusisha kwenye kuhoji sababu wanaleta mkanganyiko usio na ulazima.
 
MKUU SIJAWAONA SHAKA YOYOTE NA ALLAH KAYASEMA HAYO AKIWA NA UHAKIKA KUWA SITAKUWA NA SHAKA,SIO MTU KUWA NA SHAKA TU PIA KAMA UNAHISI SIO KITABU CHAKE UMEPEWA RUHUSA YA KULETA KITABU KINACHOFANAN NA IYO QURAN WALAU AYA MOJA.....HALAFU HAKUNA KITABU KINAITWA BIBLE/BIBILIA KUNA TORAT ZABUR NA INJIL...HAIJAWAH TOKEA SHAKA HADI KUVIENDEA IVYO VIPANDE
maelezo yako si kweli mkuu, kurani kamwe haijitoshelezi na ndio sababu hata wewe hapo bado unakaririshwa tu kuwa kuna Torat, Zaburi na Injili lakini nikikuuliza nitajie hata aya moja iliyoko kwenye injili huna kwakuwa hujui lolote kuhusu vitabu hivyo. Kama naongopa nikosoe kwa kuniambia Injili kipo wapi, kinasomwa na nani na mfano wa aya yake ni ipi? Fanya hivyo na kwa Zaburi na Torat pia!
 
Waislam hatuwezi kusoma Bible ila tutasoma Injili, zaburi, taurati, na Qur'an tu. Sisi hatujui na wala hatuamini kuwa Bible ni kitabu cha Mungu.
Wee jamaa bhana umenichekesha sana, muislamu haifahamu torati, haifahamu zaburi wala haifahamu Injili zaidi ya kuambiwa tu kuwa kuna vitabu hivyo, hebu niambie kwa mujibu wa kuran, vitabu hivyo viko wapi, vinasomwa na nani? Kwa kunisaidia zaidi nitajie japo aya mbili katika kila kitabu kimojawapo!
 
Mkuu siri ni hyo kwamba kwanini baadhi ya vitabu vimetolewa kwa sababu X and Y na vingine vimebakizwa ilihali vina madhaifu hayo hayo ya X na Y hapo ndipo kuna siri ambayo natamani wote tui unlock hapa maana kuna uwezekano wachache wanaifahamu kwa gharama ya kupotosha wengine na hyo ndio SIRI inayozungumzwa hapa

Karibu tueleweshane
Sababu(upande Wa new testament) ni source of information... Wale church fathers walipokea mtu aliyekuwa direct mwanafunzi wa yesu au alijuana nao first hand bila hivi hata kama kitabu chake kinasound aje hawakutaka hata kukisoma...hii ndo ilikuwa criteria ya vitabu vya NT
Upande wa OT pia hiko kitu waliangalia lakn pia waliangalia theology inayofundishwa humo kama haiendani na theology ya rest of the book waliitupia kule

Kwamfano theology ya book of Enoch ni very strange na iko tofaut na rest of the bible...but hivi vya OT wana wa Israel walikuwa wanachambua na kuvitunza vile authentic,,,,,
All in all keep in mind shetani anajaribu kuingizia mafundisho yake ili kupotosha watu...beware
 
Ninakushukuru sana wewe,pamoja na "Sala na Kazi" kwa namna mlivyoweza kujibu hoja nyingi zilizojibandika katika uzi huu. Mmetumia maelezo ya kisomi sana kuhitimisha mjadala.Kwa kuwa uzi umekwisha kufika mbali, mimi nitaleta uzi pekee kueleza ni nani alifanya nini kuhusu Biblia na ni akina ni bendera fuata upepo tu linapokuja suala la Biblia na ni akina nani wanazalisha mambo ya kizushi kwamba kuna Injli hii au ile ilikataliwa tu lakini na yenyewe ilifaa kuingizwa katika Biblia.

Kuna watu kwa sababu ya kufichwa historia,wanaamini kuwa wanaifahamu sana Biblia, kumbe wanakimbia na vipande vya Biblia tu huko waliko.Na kwa kuwa wameendelea kupiga mayowe muda mrefu na wanafanya hivyo wakifikiria wao ndio wenye ukweli,basi muda si mrefu tutaweka mambo hadharani.Na nina imani ukweli huo utakapowekwa hadharani hawatabaki salama huko waliko.
majisifu ya nini mkuu, we mwaga nondo zisomwe tu, ni ngumu mno kumrudisha mprotestant catholic kuliko kumchomoa mkatholic kwenda protestant, ni ngumu kama mpini wa jembe kupenya katika tundu la sindano.
 
Sababu(upande Wa new testament) ni source of information... Wale church fathers walipokea mtu aliyekuwa direct mwanafunzi wa yesu au alijuana nao first hand bila hivi hata kama kitabu chake kinasound aje hawakutaka hata kukisoma...hii ndo ilikuwa criteria ya vitabu vya NT
Upande wa OT pia hiko kitu waliangalia lakn pia waliangalia theology inayofundishwa humo kama haiendani na theology ya rest of the book waliitupia kule
Kwamfano theology ya book of Enoch ni very strange na iko tofaut na rest of the bible...but hivi vya OT wana wa Israel walikuwa wanachambua na kuvitunza vile authentic,,,,,
All in all keep in mind shetani anajaribu kuingizia mafundisho yake ili kupotosha watu...beware
mkuu, kitabu cha henoko kimewiana na vitabu vya biblia kwa kiwango kikubwa sana mzee. pitia tena.
 
Biblia kwenye sayans ya leo ime fail sana kwa sayans ya kawaida kabisa...kina sehem inasema dunia ni duara kuna sehem inasema dunia tambarare ukikubaliana na hoja zote inamaana dunia ipo kama disc.!

Sent using Jamii Forums mobile app
kamwe biblia haijawahi kusema dunia ni duara as globe, ila ni duara kama disc! hivi ndivyo wanasayansi hata wa sasa walivyothibitisha, na kufuta uongo uliopenyezwa kwa miaka mingi kuwa dunia ni duara linalozunguka mile 1000 kwa saa.None sense!
 
Sababu(upande Wa new testament) ni source of information... Wale church fathers walipokea mtu aliyekuwa direct mwanafunzi wa yesu au alijuana nao first hand bila hivi hata kama kitabu chake kinasound aje hawakutaka hata kukisoma...hii ndo ilikuwa criteria ya vitabu vya NT
Upande wa OT pia hiko kitu waliangalia lakn pia waliangalia theology inayofundishwa humo kama haiendani na theology ya rest of the book waliitupia kule
Kwamfano theology ya book of Enoch ni very strange na iko tofaut na rest of the bible...but hivi vya OT wana wa Israel walikuwa wanachambua na kuvitunza vile authentic,,,,,
All in all keep in mind shetani anajaribu kuingizia mafundisho yake ili kupotosha watu...beware
Nimekuelewa mkuu sasa basi kama kwa mfano Book of Enoch ipo strange ni kwanini hao church fathers wakiache kitabu cha Yuda kwenye Bible ambacho kimenukuu baadhi ya mistari kutoka kitabu cha Enoch??

Pia ni kwanini church fathers waliacha kitabu cha Yoshua kilichonakili na kuacknowledge kabisa kuwa Kitabu cha Yashari ndio kina content kuhusu mambo ya wayahudi na imani yao kwa Mungu, ilihali church fathers wamekikataa kitabu cha Yashari kuwa kwenye Old testament. Kwanini hii contradiction??

Yaani Mimi zitto junior sijawekewa book of jasher na Enoch kwa bible kwa hoja X and Y ila Mtume Yuda na Yoshua wamevinakili kabisa na kuvitambua na hakuna church father aliyefuta vitabu vyao kwenye Bible. Huoni kuna double standard mkuu kwenye hoja yako.

2. Kuna vitabu vina theology tofauti kidogo mfano song of solomon na kwenye Old Testament kinahesabika kama pseudepigrapha kama tu Book of Enoch ila cha kushangaza chenyewe kiliwekwa ila Enoch/Jasher vilikataliwa why tatizo hilo hilo ila hukumu tofauti??

Karibu
 
maelezo yako si kweli mkuu, kurani kamwe haijitoshelezi na ndio sababu hata wewe hapo bado unakaririshwa tu kuwa kuna Torat, Zaburi na Injili lakini nikikuuliza nitajie hata aya moja iliyoko kwenye injili huna kwakuwa hujui lolote kuhusu vitabu hivyo. Kama naongopa nikosoe kwa kuniambia Injili kipo wapi, kinasomwa na nani na mfano wa aya yake ni ipi? Fanya hivyo na kwa Zaburi na Torat pia!
Sina haja yakuvisoma hivyo sabab quran inajitosheleza....Kuzidi sana nitasoma Sunnah.Kutajiwa vitabu hivyo hainamaana natakiwa kuwa navyo mana vishachakachuliwa.

Mimi kutajiwa hivyo vitabu ni ili kufaham kwamba vilishawah kutoka zama za mitume waliotangulia na yanipasa kusadiki hayo.Naifaham Biblia ambayo imetengenezwa kwa kuchanganywa sehem za vitabu hivyo na kwa kutolewa na kuongezwa waliyoona wao yanafaa kuwepo.Zaidi yakupasa uzijue matoleo (version) ya iyo biblia na utajua kipi kimeongezwa na kipi kimetolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana kwenye Qur'an huwezi kuona makosa mengi kama kwenye biblia ambayo ni ya wazi sana kwenye agano jipya,, najiuliza tu kwanini waislam hawana agano jipya inamaana wao hawakuwa na agano before?

Hebu acha vituko; Qur'an gani isiyo na makosa? Hii hii iliyobuniwa na Marehemu Muhammad?
 
Nimesoma kidogo the book of enock!kinapingana na sayansi ya shule kuhusu Rotation of the earth na unajimu!pia uundwaji wa silaha,uchawi ulivokuja duniani,uganga na mengine sana ambayo yametofautiana sana na uongo wa shuleni tuliomezeshwa!!!NADHANI NDO MAANA KILIONDOLEWA KWENYE BIBLIA ZETU HIZI!!!HAO WANASAYANSI NI WAONGO SANA!!!!
 
Pia kwenye the book of jubilees ukisoma !utaona pia urithi wa NUHU KWA WATOTO WAKE!inasomeka Ham alipewa maeneo yd joto,Shem alipewa maeneo baridi sana,jafeti alipewa maeneo yenye wastani sio joto wala baridi!Na vita Zilianza kupiganwa kipindi hicho wana wa ham walipoanza kuhamia kwenye maeneo ya nduguze!!!PIA NUHU KABLA HAJAFA ALIANDIKA DAWA ZA KUTIBU MAGONJWA YOTE DUNIANI NA HICHO KITABU AKAMPA MWANAE MKUBWA SHEM!!!INA MAANA WAZUNGU WANAJUA TIBA ZOTE KWASABB WALIACHIWA NA NUHU BABA YAO AMBAE NI SHEM!KUMBUKA SHEM RANGI YAKE NI NYEUPE,JAFET MWEKUNDU,HAM NI RANGI NYEUSI ILIYOUNGUA!!!!!
 
Nimependa uandishi wako mkuu umeandikwa kiuchunguzi sana,Nikweli kwa dunia ya sasa kuna biblia nyingi sana na ambazo zimeandikwa kwa mujibu wa DOCTRINE ya hao walioiandika,hapa namaanisha kama ukikuta biblia ya kisabato,kikatoliki,kulutheri nk basi inaandikwa kwa mujibu wa iman yao na sio kwa mujibu wa imani au DOCTRINE YA MUNGU.


Ukisoma biblia nikweli kuna vitabu takribani 6-8 ambavyo vilitolewa kwa sababu za hao waliokuwa wanatafasiri haya maandiko kutoka kwenye lugha za kiyunani,kiebrania na kigiriki,ukisoma ndani ya biblia ile ya kiprotestant yenye vitabu 66 kuna baadhi ya manabii wameerejea unabii au wamenukuu unabii katika baadhi ya vitabu ambavyo haviko ndani ya hiyo biblia ya vitabu 66 na kama kweli wakati wanaandika vitabu vyao walikuwa wanaongozwa na Roho mtakatifu basi Roho mtakatifu asingewapa reference katika maandiko ambayo hayana Pumzi ya Mungu au hayakuandikwa kwa muongozo wa Roho mtakatifu mwenyewe! mfano ukisoma kwenye KJV Joshua 10:13 (Joshua amerejea kitabu cha yashari) lakini kuna baadhi ya biblia za kiswahili hawajatafasiri hili rejeo la kitabu cha Yashari! inamaana kama Yoshua aliweza kusema" kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari" na alikuwa anaongozwa na Roho mtakatifu katika uandishi wake basi kitabu cha Yashari kinapaswa kuwepo katika biblia ya vitabu 66!

Kitabu kingine ni Kitabu cha Henoko! Nabii Yuda katika kitabu chake pia aliweza kurejea kitabu cha Nabii Henoko wakati wa uandishi wa kitabu chake pia Yuda 1:14,sasa huu unabii amabo Yuda ameunukuu hapo haupatikani katika kitabu chochote ndani ya biblia ya vitabu 66 isipokuwa unaupata kwenye kitabu cha Henoko mwenyewe! inamaana Yuda alisoma kwenye kitabu cha Henoko ndio akaweza kukirejea kama ambavyo Yesu alivyokuwa anajaribiwa na Shetani alikuwa namjibu shetani "IMEANDIKWA" then ananukuu kitabu fulani na Bwana Shetani akawa anaelewa kweli kuna mahali pameandikwa hivyo ndio kitu hicho hicho hawa mitume walikuwa wanavirejea hivi vitabu ambavyo leo hii kwenye biblia havipo tunaambiwa ni 66 tu!

USHAURI WANGU
Maandiko yoote matakatifu yameandikwa kwa msaada wa Roho mtakatifu inahitaji uwe na roho yule yule aliyeandika haya maandiko kuweza kukufunulia maana yake na uhalisia wa hivi vitabu na nini cha kufanya! na hujakatazwa na mtu kusoma hivyo vitabu vya ziada mwenyewe katika biblia yangu ninayotumia ina vitabu zaidi ya 66 unaweza nunua hapa

Amazon product ASIN B00KGF44DS
 
Sina haja yakuvisoma hivyo sabab quran inajitosheleza....Kuzidi sana nitasoma Sunnah.Kutajiwa vitabu hivyo hainamaana natakiwa kuwa navyo mana vishachakachuliwa.Mimi kutajiwa hivyo vitabu ni ili kufaham kwamba vilishawah kutoka zama za mitume waliotangulia na yanipasa kusadiki hayo.Naifaham Biblia ambayo imetengenezwa kwa kuchanganywa sehem za vitabu hivyo na kwa kutolewa na kuongezwa waliyoona wao yanafaa kuwepo.Zaidi yakupasa uzijue matoleo (version) ya iyo biblia na utajua kipi kimeongezwa na kipi kimetolewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
wee ni mjinga sana,hata huo usilam huujui.

wenzako wanapolingania injili wanamaanisha,wewe unakuja kusema huna haja ya kusoma maana quran imejitoshereza,wewe ngamia kweli rafiki yangu.
 
wee ni mjinga sana,hata huo usilam huujui.

wenzako wanapolingania injili wanamaanisha,wewe unakuja kusema huna haja ya kusoma maana quran imejitoshereza,wewe ngamia kweli rafiki yangu.
Eeee umepanic eee...Embu taratib tuanzie hapa..Ni nani anayelingania Injili katika waislamu,namaanisha nataka kumjua uyo shehk alinganiaye injil,kama utakuwa na video au audio walau maandishi kama ushahidi wako itakuwa vyema zaidi.Huenda ukakosa huo ushahidi basi nipe rejea uyo shehk anakoegemea.

Nikupe darsa kidogo mjinga mimi
Ipo iviiii katika nguzo za imani katika uislamu moja wapo ni kuviamini vitamu vya Allah ambavyo ni Torat, Zabur,Injili na Quran kwamba hivi vitabu vya mwenyezi Mungu vilishuka katika za mitume katika zama zao.Vitabu vyote ivyo vya mwanzo wanaadamu wametia maono na fikra zao na kuzusha humo yasiyokuwepo na kutoa waliyoona hayaendani na maslahi yao.

Allah alipotumiliza Quran ni ili kulisafisha neno lake na kisha kuilinda dhidi ya mikono ya wanaadam.Na quran imekusanya yaliyo katika vitabu hivyo na kuotoa muongozo mpya ambayo Quran ndio Chakufuatwa baada ya hivyo vingine kuharibiwa.Mimi kama muislamu yanipasa kuamini kwa kweli kuna vitabu hivyo vya awali lakini sio kuvifuata tena katika hukumu na mafunzo wala rejea yoyote humo bali yanipasa Kufuata Quran na Hadithi kama rejea ya mambo yote.

Labda pia nikuage kwa kisa hiki zama za mtume.
 
Back
Top Bottom